DC aangua kilio kikaoni, pata tukio zima katika picha

Kuna mtu aliniambia huyo DED ni mtendaji mzuri sana.Mwenye ufahamu zaidi atujulishe
Huyu DED alikua afisa mipango rufiji na ni mtu makini sana ila katika kazi kuna mambo yanapinda na kusanuka palepale sasa kama mtu analia kwa ajili yake sijui kimetokea nini
 
  • Thanks
Reactions: SG8
badala ya kuchukua hatua yeye analia kikubwa alichotawiwa ni kumuwajibisha mkurugenzi na kama hawezi amuripoti kunakohusika kulia hakusaidii tena ni mkoa wa mtoto wa mkulima aliyelia bungeni
 
Huyu siyo fisadi moyoni mwake, angekuwa fisadi asingeona uchungu mkubwa hivo. Tatizo tu analilia uozo wa kulindana wa serikali yake. Kuwa kama angekuwa ni uwezo wake angewatimua kazi na kuwafunga jela na wakitoka walambwe mboko.

alikuwa analia kwa furaha si kwa uchungu.Kipindi tulichonacho cha viongozi hakuna mwenye uchungu
 
kwenye msafara wa "mamba" na "makenge" wamo-yawezekana ndugu huyu ni "kenge"-pole sana mkuu!
 
The Nkasi District Commissioner, Mr Idd Kimanti, has blasted and blamed the Nkasi District Council's Executive Director, Ms Saada Mwaruka and her head of departments for failure to deliver, causing the council to perform poorly in most of its key projects.

Idd-Kimanti.jpg

The Nkasi District Commissioner, Mr Idd Kimanti, was in tears yesterday
 
Ukuu wa wilaya ni jukumu ambalo lina changamoto nyingi maana kila kukicha ni kukimbizana na wanavijiji. Kuna wengine wameanza kujuta kwa kuteuliwa kwao kwasababu baadhi wanagomewa na viongozi wa vijiji!

Kweli nchi hii kuna vibweka,baada ya kulia alichukua hatua gani? aliishia hapohapo nakuacha waendelea na uozo?,yetu macho
 
Kumbe ni kawaida ya haya majamaa kulia lia hovyo?Hapa anamuiga mizengwe mpindo alipoangua kilio mjengoni akiunusuru u pm,liwalo na liwe!!!

Yap, wamefanya ni kamtindo flan, Ingawa wengine huwa wanalia wakikosa mgao wa ten percent na kujifanya wanawalilia wananchi kumbe ni machozi ya fungu..!
 
Aache kulia, aje huku CDM kwa majembe kuendeleza mapambao. Ukiwa CCM utalia sana, maana mauozo ni mengi sana!
 
Huyo DC anadhani akilia ndiyo atabadilisha hali ya mambo? Utendaji huo mbovu ni kwa halamashauri nyingi hapa nchini. Na wenye ndevu za waya naamaanisha waliowaweka madarakani wakurugenzi wa aina hiyo wanaona hakuna shida. sasa we DC unaanza kulia ili iweje, kama una uwezo piga chini hao watendaji!
 
Haka katabia ka-kuigiza alikaanzisha pinda,sasa wengine wameanza ku-copy na ku-pest,ujanja wa viongozi dhaifu
 
Ni kweli inatia uchungu kwa mtu mzima mbele ya kadamsi ya watz kupitia vyombo hivi vya habari'kwani hata familia yake nafikiri inajuta kwa nini Baba mtu alikubali post hiyo.
Natoa POLE,lakini na ushauri kwa Mkuu hapo utaendelea kulia tu INJI hii utageuziwa kibao wewe subiri tu
naogopa kukushauri hatua za kuchukuwa kwa sababu hayo mambo huenda yalishafikishwa mahakamani,ILA
shauri langu hamia CDM penye wenye uchungu kamili na NCHI hii na siyo INJI hii.
 
Huyu DED alikua afisa mipango rufiji na ni mtu makini sana ila katika kazi kuna mambo yanapinda na kusanuka palepale sasa kama mtu analia kwa ajili yake sijui kimetokea nini
Nafasi ya DED ina vishawishi vingi sana. Huyu si yule uliyemfahamu akiwa Rufiji. She is a different mama today.
 
We mbaba we siuna mke na watoto sasa kinachokuliza mbele ya kadamsi kwaajili ya ako kamama kenye uso mkavu ni nini? mpe nako au jiuzulu usituletee uchuro hapa! mwanaume huwa halii anafanya vitendo bwana! MPE KITU CHA M4C
 
CHADEMA hatutaki vijibaba vya kulialia abaki hukohuko mabwepande na mwenzie PINDA huku ni kazi tu hatuna kliniki ya watu wazima mkuu
 
Mwanaume anatakiwa afanye maamuzi magumu na si kulia huku wanawake macho makavu. Haitakiwi kuongoza kwa emotion bali kwa akili , hekima na busara. Kutoa machozi ni ishara kuwa uwezo wa kufikiri umeishia hapo ikabidi kulia
 
...Wakuu, tusimdhihaki mheshimiwa wetu. Kuna taarifa za kuingia na kusambaa kwa ugonjwa mbaya unaojulikana kama 'Pindaizm Machoziizim' ambao unasemekan kumpata mtu anayetaka kuonewa huruma. Jambo jema ni kwamba dawa ya ugonjwa huo ni kuwa Mgumu tu na kutafuta ufumbuzi wa tatizo lililokufanya utoe machozi....!
 
...Wakuu, tusimdhihaki mheshimiwa wetu. Kuna taarifa za kuingia na kusambaa kwa ugonjwa mbaya unaojulikana kama 'Pindaizm Machoziizim' ambao unasemekan kumpata mtu anayetaka kuonewa huruma. Jambo jema ni kwamba dawa ya ugonjwa huo ni kuwa Mgumu tu na kutafuta ufumbuzi wa tatizo lililokufanya utoe machozi....!
 
Back
Top Bottom