DC aangua kilio kikaoni, pata tukio zima katika picha

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
DSC07021.JPG


Mkuu wa wilaya ya Nkasi , Idd Kimanta akiangua kilio jana akisikitikia na kuona uchungu utendaji wa ovyo wa Mkurugenzi na wakuu wa idara ya halmashauri hiyo mbele ya baraza la madiwani mjini Namanyere kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Nkasi , Saada Mwaruka.
DSC07023.JPG

Mkuu wa wilaya ya Nkasi, Idd Kimanta akiangua kilio jana akisikitikia na kuona uchunugu utendaji wa ovyo wa Mkurugenzi na wakuu wa idara ya halmashauri hiyo mbele ya baraza la madiwani mjini Namanyere. (Picha zote na Walter Mguluchuma)

Blogzamikoa
blogszamikoa.blogspot.com
 
Huenda anajua kuwa kwa utendaji kazi mbaya wa hao maofisa wake kibarua chake kiko mashakani ingawa anaweza kuwa ni design ya babake mkubwa wa kuangua vilio bungeni kutetea U-PM
 
Pole mkuu, siku nyingine USILIE bali uchukue hatua kulingana na ofisi yako, DC mzima unalia?? Hao wananchi wako wafanyeje??. Hujui kuwa ukilia mbele ya waliochini yako ni kuonyesha kuwa wee ni DHAIFU?? Wee mgeni nchi hii.?? Ukome kulialia ovyo, ama uwe unalia huku unachukua hatua zipasazo. POLEN WANANKASI.
 
Kuna mtu aliniambia huyo DED ni mtendaji mzuri sana.Mwenye ufahamu zaidi atujulishe
 
Analilia nini? au Ni katika hali ya kujipendekeza na kutafuta sifa (chati) angefanya kama yule DC kule Bukoba alipoamua kuwachapa viboko walimu aanzie na huyo mama mwenye uso mkavu na kitambaa walichotandikia meza kinaniumuza macho
 
Hicho kikao kimafanyikia bafuni au? maana hizo tiles sio za kwenye chumba cha mkutano na jinsi zilivyojengwa kama bafuni au chooni vile. Sorry kwa maneno magumu
 
Ukuu wa wilaya ni jukumu ambalo lina changamoto nyingi maana kila kukicha ni kukimbizana na wanavijiji. Kuna wengine wameanza kujuta kwa kuteuliwa kwao kwasababu baadhi wanagomewa na viongozi wa vijiji!
 
Back
Top Bottom