Dawa za Kulevya: Yusufu Manji afikishwa Mahakamani Kisutu, aachiwa kwa dhamana

Manji yupo hapa Tanzania miaka nenda rudi, babu na baba yake walikuwepo miaka yote.. Manji huyu kwa namna moja au nyingine ameisaidia sana CCM na watu wake, Manji huyu amefanya sana biashara zake kwa kusaidiwa na CCM, Manji huyu amekuwa diwani kupitia chama hiki cha CCM, Manji huyu ni mwenyekiti wa moja ya timu kubwa na kongwe hapa tanzania, Manji huyu ameshawahi kuingia kwenye kinyang'anyiro cha Ubunge kupitia CCM.. Eti leo Serikali ya CCM inamtuhumu Manji ni Mharifu na mtumiaji wa Madawa ya kulevya.

Hivi hamuoni hata aibu kwa haya myafanyayo dhidi ya huyu Manji, hamtutetei Manji ila tunazishangaa mamlaka zetu na kuhofia usalama wa taifa hili dhidi ya mizaha hii kwa watu hawa ambao ni marafiki na wafadhili na wadau wa mifumo yetu..
Aibu nyingine tuzifiche ili kiasi cha upumbavu wetu kisijulikane.....
 
Manji kaikosea nini ccm? japokuwa siwezi kumtetea, ila kiuhalisia Manji ameonewa Sana, utajiri wa Manji ni wa kurithi vizazi na vizazi.
Duh tutasikia mengi sana safari hii.
Kumbe atapandishwa kizimbani kwa kosa la UTAJIRI....
Aiseeeee........
 
Kwa hiyo kuanzia leo na manji tutegemee atawekwa chini ya uangalizi
Mtumiaji dawa ya kulevya hawezi kuacha kwa kushitakiwa ama kuwekwa chini ya uangalizi, anatakiwa apelekwe hospitali na sio kwa kulazimishwa, mtumia madawa ya kulevya hawezi kuacha addiction kwa vitisho ila ni mpaka mwenyewe akubali kwanza ana tatizo, na kwa dhati mwenyewe ana nia ya kuchana na tatizo hilo, operation ya kutumia nguvu itasababisha waende under ground.
 
Habari wakuu JF

Mfanyabiashara mkubwa na mwenyekiti wa klabu ya YANGA Ndugu Manji leo atapandishwa kizimbani Kisutu kwa kesi ya kuhusika na matumizi ya dawa za kulevya.


Naomba tujuzane kila kinachoendelea...
Si vyema kuanzisha 'thread' wakati huna 'info' kuhusu kitu ulichoaanzisha. 'Unless' kama una swali na lazima 'thread' yako iwe kwenye mfumo wa swali sio kama ulivyooandika 'as if' una jambo la msingi la kutueleza
 
Makundi ya watu wanaomtetea Manji
1. wana yanga njaa
2. wenye itikadi moja naye nliwasikia watu wakisema jana nje ya msikiti mmoja kuwa ni mwana shia mwenzetu
3. wapinzani njaa ambao wao watapinga tu kwa kuwa kakamatwa na serikali hii
4. wasiojielewa
5. wauza,watumiaji madawa ya kulevya.

haya ni baadhi ya makundi ambayo yatasiama siku zote kumtetea na kujaribu kumsafisha. ukweli unabak the man is so dirty na ametuingizia taifa hasara nyingi sana.

Kumbe manji ni diwani wa upinzani? nilikuwa sijui
 
Gangongine,
Stupid is your president who is interfering with Courts of Law to kill opposition parties!
Hivi wewe hujui kuwa Lema yuko Mahabusu mwezi wa nne sasa kwa kunyimwa dhamana maksudi kwa MAELEKEZO TOKA IKULU???Pumbaf!
UNA USHAHIDI GANI WEWE
 
Mahakamani kama walivyopelekwa kina TID.Haki lazima itendeke kwa wote.ila kumbe tunapozungumzia mateja, tunawazungumzia watu kama manji. Nimejifunza jambo zito sana
Jifunzeni tofauti akina Tid walikiri na kukubali wakapata huruma ya kuwasaidia maana wamekiri na wametoa ushirikiana huyo jamaa kakataa ndio mana wakaenda hosptal so anakesi kasema uongo then anatumia.
 
Huyu aliapa kumshitaki makonda, kwahiyo wanakomaa nae ili kupoteza hilo lengo la Manji.

Kama TID na wengineo wanatumia, mbona wameachiwa?? Kwanini Manji?
Ilishasemwa mtumiaji anafungwa miaka mitatu, nafikiri hiyo kauli alilengwa huyu jamaa
 
Back
Top Bottom