Dawa za Kulevya: Yusufu Manji afikishwa Mahakamani Kisutu, aachiwa kwa dhamana

mcubic

JF-Expert Member
Mar 3, 2011
10,306
6,514
Mwenyekiti wa Yanga Yusuf Manji kupandishwa Mahakamani kesho kwa matumizi ya dawa za kulevya.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro amesema kuwa vipimo vya Mkemia Mkuu wa Serikali vimebaini mfanyabiashara mkubwa ambaye pia ni mwenyekiti wa klabu ya Yanga, Yusuf Manji hutumia dawa za kulevya.

Akizungumza leo na E-FM, Kamanda Sirro amesema kuwa hali ya Manji ambaye alilazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kitengo cha moyo, muda mfupi baada ya kuhojiwa na jeshi hilo inaendelea vizuri na kwamba kesho atafikishwa mahakamani akikabiliwa na kesi ya matumizi ya dawa za kulevya.

Kamanda Sirro ameeleza kuwa Manji ameruhusiwa kutoka hospitalini na kwamba amerudishwa katika selo za polisi akisubiri kufikishwa mahakamani.

“[Manji] yuko vizuri na kesho atapandishwa mahakamani kwa kosa la matumizi ya dawa za kulevya,” kamanda Sirro ameiambia E-FM.

“Nitawambia vizuri kesho kwa kuwa kesho ndio nakutana na waandishi wa habari. Kwahiyo wanivumilie, kesho nitawaambia hali halisi ilivyo na wajue mwenyekiti wao ni nani na ni mtu wa namna gani,” ameongeza.

Kamanda Sirro amefafanua kuwa ingawa mfanyabiashara huyo atapandishwa mahakamani kesho, haitamzuia yeye kutolea ufafanuzi tuhuma zinazomkabili.

Aidha, ameeleza kuwa mbali na Manji, Jeshi hilo linawashikilia wasanii kadhaa na watu wengine ambao watafikishwa kesho mahakamani wakikabiliwa na kesi ya matumizi ya dawa za kulevya.

Manji alifika katika kituo cha polisi Alhamisi iliyopita akiitikia wito wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda aliyemtaja kati ya watu kadhaa wanaotuhumiwa kujihusisha na dawa za kulevya.

Mwenyekiti huyo wa Yanga ambaye awali alikanusha vikali tuhuma dhidi yake, aliwasili katika kituo polisi cha kati jijini Dar es Salaam akisindikizwa na mashabiki wa timu hiyo. Alihojiwa na kufanyiwa vipimo kabla hali yake haijabadilika na kulazwa katika hospitali ya Muhimbili.






======

UPDATES

ytu.png


cdes.png
Dar es Salaam. Mfanyabiashara maarufu Yusufu Manji amepata dhamana baada ya kusomewa shtaka moja la kutumia dawa za kulevya aina ya heroine.

Manji amesomewa shtaka hilo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya wakili wake Alex Mgongolwa kuiomba dhamana na Jamhuri kusema haina pingamizi kwani shtaka hilo linadhaminika.

Hakimu Cyprian Mkeha amesema Manji atakuwa nje kwa dhamana kwa sharti la kusaini bondi ya dhamana ya Sh10 milioni na awe na mdhamini mmoja ambaye atasaini bondi ya Sh10 milioni.

Amedhaminiwa na Katibu Mkuu wa Yanga Charles Mkwassa.
 

Attachments

  • WhatsApp Audio 2017-02-15 at 20.48.00 (1) (online-audio-converter.com).mp3
    3.1 MB · Views: 169
Gwajima si alisema kuwa yeye na Manji walipopimwa Kwa Mkemia Mkuu walikutwa -ve.Imekuwaje tena yeye apandishwe mahakamani Kwa jambo ambalo Gwajima anasema jamaa hausiki nalo?

Gwajima ndio mkemia mkuu? Kama damu ya Manji isingeonesha kuwa anatumia madawa ya kulevya basi ingekuwa dhahiri rushwa imetembea. Huyu mbon anafahamika? Kwani wakati ule alipokimbizwa Nairobi tatizo lilikuwa nini?
 
Atakuwa kaomba msamaha hivyo anapelekwa mahakam apewe dhamana na movie akishapata dhamana ngoma inaandika "END"

Afu yanabaki yale maandishi meeengi yanayotokaga chini ya tv scrin kwenda juu pale ambapo mkanda umeisha.
 
Back
Top Bottom