Dawa za kulevya: Watanzania watatu wakamatwa India, mmoja afariki

EMT

Platinum Member
Jan 13, 2010
14,483
15,308
Kuna taarifa kuwa Watanzania wawili wamekamatwa na dawa za kulevya nchini India na kwamba mmoja wao amefariki dunia. Taarifa zinadai kuwa Watanzania hao, ambao walikuwa watatu, waliwasili katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa Chatrapati Shivaji juzi asubuhi na Ethiopian Airlines Flight 610.

Baada ya kutua uwanjani hapo, maafisa kutoka uwanjani hapo waliwakamata Watanzania wawili kati ya watatu kwa mahojiano zaidi baada ya kutonywa (tip-off) kuwa walikuwa wamebeba dawa za kulevya. Baada ya kuhojiwa kwa muda wa masaa matano, Watanzania hao walikataa katakata kuwa walikuwa "punda" wa dawa za kulevya.

Taarifa zinadai kuwa maafisa hao waliamua kuwapa Watanzania hao chakula na maji kama trick ya kujua kama walikuwa wamebeba dawa za kulevya. Kwa kawaida, mtu aliyemeza vidonge vya dawa za kulevya hali wa kunywa ili kuepukana na kifo. Hivyo basi, kama mtuhumiwa akipewa chakula na kukataa kula inaweza kuwa ni dalili kuwa amemeza vidonge vya dawa za kulevya.

Hivyo basi, baada ya kupewa chakula na maji, Mtanzania mmoja alikataa kula wala kunywa. Hata hivyo, Mtanzania wa pili alikubali kula chakula alichopewa. Baada ya hapo, Watanzania wote watatu walipelekwa mahakamani, lakini yule aliyekubali kula alikataa na kutaka kukukimbia. Baada ya purukushani katika eneo la mahakama, yule aliyekubali kula chakula alifariki baada ya kuzidiwa na vidonge vya cocaine kama 120 alivyokuwa amemeza.

Hali ya Mtanzania wa pili ilizidi kuwa mbaya na alipelekwa katika hospitali ya JJ. Baada ya kufanyiwa X-ray na CT-scan alikutwa amebeba vidonge vya cocaine kama 100 hivi. Kwa mujibu wa maelezo ya mkuu wa hosipitali hiyo, hali yake ni mbaya lakini hajapelekwa ICU.

Mtanzania wa tatu, ambaye ni mwanamke wa makamo, bado anahojiwa na vyombo husika. Mwanamke huyo hakukutwa na dawa zozote lakini alikuwa ameongozana na wanaume hao wawili. Upelelezi bado unaendelea kujua kama alikuwa mmiliki wa hizo dawa za kulevya.

Habari kwa mujibu wa India Today, The Times of India, Daily News India
 
Taarifa zinadai kuwa maafisa hao waliamua kuwapa Watanzania hao chakula na maji kama trick ya kujua kama walikuwa wamebeba dawa za kulevya. Kwa kawaida, mtu aliyemeza vidonge vya dawa za kulevya hali wa kunywa ili kuepukana na kifo. Hivyo basi, kama mtuhumiwa akipewa chakula na kukataa kula inaweza kuwa ni dalili kuwa amemeza vidonge vya dawa za kulevya.

Mkuu lakini kisheria huwezi kumlazimisha abiria yoyote kula wala kunywa. Miaka michache iliopita nilikataa kula wala kunywa, tena niliwaambia sitaki kusumbuliwa, na ilikuwa ni flight from AMS - LAX. Hakuna alienilazmisha wala kunishuku. Je ni kwanini hawakudhania mimi ni drug mule? Naomba kuelimishwa, manake isijekuwa wanawanyima hawa vijana haki zao kama abiria
 
Huenda ni baada ya kushuka, ikiwa abiria anakuwa suspect akishakuwa chini ya police nadhani anakuwa treated sio "abiria like" bali kama suspect

Nchi yetu watu hatukomi aisee, hizi dhambi mbaya tuache jmn. Ukimwi upo lkn watu hatuachi mgegedo, hawa ni wa kuwahurumia tu sio kuwa condemn
 
Baada ya kushuka, abiria anakuwa suspect kwa kigezo gani? Kwa kuwa alikataa kula au kunywa chochote?
 
Masogange na mwenzake, yule jamaa wa marekani na laptop wote walikuwa ndio wanatoka kwenye ndege. Mpk mtu asachiwe maana yake ni kuna dalili ambazo ziko. Hata wasingewaambia wasile at the end of the day wangezitoa tu.
 
Kwenye airport Za watu tunasachiwa balaa mpaka vya tumboni vinatambulika,ila hapa kwetu ukifika Julius Nyerere international airport mida ya usiku utakuta wamelala tu,nilishangaa majuzi baada ya kumwona mmama mbele yake kuna computer anachapa usingizi mpaka anakoroma
 
Dah hatari sana, ni kutowajibika ambako ni kaugonjwa ka taifa.
 
Mkuu lakini kisheria huwezi kumlazimisha abiria yoyote kula wala kunywa. Miaka michache iliopita nilikataa kula wala kunywa, tena niliwaambia sitaki kusumbuliwa, na ilikuwa ni flight from AMS - LAX. Hakuna alienilazmisha wala kunishuku. Je ni kwanini hawakudhania mimi ni drug mule? Naomba kuelimishwa, manake isijekuwa wanawanyima hawa vijana haki zao kama abiria

wangeweza itwist vizuri wanaweza komaa kuwa jamaa ndio wamemuua, kwa vile walimlazimisha kula na hivyo kumuua.Halafu km CCM hazitodanganya basi waendelee kudai hata hizo dawa nazo pia ni matokeo ya kulazimishwa kula na kumeza ,na hivyo hao polisi waeleze walizipata wapi dawa na chakula.
 
Inna Lillahi wa inna Illahi Rajjun!!!. Mola atuepushe na aibu za kufa vifo vyenye fedhea kubwa kwa familia zetu!
Sasa Serikali ya India ilipataje hizo taarifa? Kwanini Serikali ya TZ isishirikiane nao ili wakamatwe huku huku?
 
Baada ya kushuka, abiria anakuwa suspect kwa kigezo gani? Kwa kuwa alikataa kula au kunywa chochote?

Kua suspect ni very subjective, na sio mbaya mtu akachagua randomly nani atahojiwa na nani asihojiwi. Hawawezi kumfunga mtu kabla ya kua na a minimum evidence kua kahusika katika titu kibaya. The scan was enough evidence, they should have started there.
Ila Kuwalazimisha kula na kunywa wamechemka. Na hapo ni wazi kua matendo yao yamesababisha huyo suspect kufa, na mwenzie kuweka maisha yake hatarini. HApa lazima serikali na familia za marhem wawajibishe hao border police.
 
Kukataa kula onboard kunaweza kutafsiriwa kwa namna nyingi. Ndio maana kuna stickers za do not disturb na wake me up for meals only. Inaeleweka kama abiria amechoka ama ana shida zingine kama kutapika etc. Wewe haukulazimishwa kwa sababu hakukuwa na sababu ya ziada kukushuku.

Hao kwanza wameshukiwa. Pili wamehojiwa kwa muda mrefu. Lakini kigezo cha kuwapeleka mahakamani sio kukataa kula. Hiyo ya kuwalazimishia or rather kuwaencourage kula ni sehemu ya kuwastress tu kwa ajili ya confession.

Just a general question. Hivi ukikutwa na drugs, ni better kufariki dunia ama kutiwa hatiani na kulipa kwa dhambi yako?
Mkuu lakini kisheria huwezi kumlazimisha abiria yoyote kula wala kunywa. Miaka michache iliopita nilikataa kula wala kunywa, tena niliwaambia sitaki kusumbuliwa, na ilikuwa ni flight from AMS - LAX. Hakuna alienilazmisha wala kunishuku. Je ni kwanini hawakudhania mimi ni drug mule? Naomba kuelimishwa, manake isijekuwa wanawanyima hawa vijana haki zao kama abiria
 
Ipo njia hii salama
........... X-ray na CT-scan alikutwa amebeba vidonge vya cocaine kama 100 hivi.

Je kwanini itumike hii
waliamua kuwapa Watanzania hao chakula na maji kama trick ya kujua kama walikuwa wamebeba dawa za kulevya. Kwa kawaida,.................
Hapa kuna kesi ya kujibu
 
Kua suspect ni very subjective, na sio mbaya mtu akachagua randomly nani atahojiwa na nani asihojiwi. Hawawezi kumfunga mtu kabla ya kua na a minimum evidence kua kahusika katika titu kibaya. The scan was enough evidence, they should have started there.
Ila Kuwalazimisha kula na kunywa wamechemka. Na hapo ni wazi kua matendo yao yamesababisha huyo suspect kufa, na mwenzie kuweka maisha yake hatarini. HApa lazima serikali na familia za marhem wawajibishe hao border police.

Kama unaingia china basi unapelekwa moja kwa moja hospitali kwa ajili ya x-ray na hawana mchezo. Sema hawa polisi walichemka kuwalisha chakula wangeliwapeleka kwa x-ray moja kwa moja, hata hivyo kitendo cha kugomea chakula kilianza kuwatia wasiwasi polisi na kama walikataa kula wakiwa kwenye ndege basi ikawa kwisha habari yao.
 
Suala la kukataa kula sio kithibitisho cha kubeba madawa tumboni. Je kama mimi ni muislam nahisi vyakula vyao vimechanganywa na nguruwe, inakuaje hapo?
Au kama mimi ni mKristo na nahisi chakula hicho kimechanganywa na nyama ya ngamia, inakuaje hapo?
 
Back
Top Bottom