Dawa za Kulevya: Nape aasa "Tusiwahukumu watu kwa Tuhuma, kubomoa brand ya mtu/taasisi ni sekunde"

Hahahaa..mkuu watanzania kama wewe mpo wengi sana..no easy money...
Endelea kusema no easy money, kama unataka kujua kuna easy money nenda ITV wewe mwenyewe umtangaze Wolper anajihusisha na madawa ya kulevya uone yatakayokukuta. Usijifiche kwenye mgongo wa msafisha viatu fanya mwenyewe uone!!
 
Makonda amefanya jambo kubwa sana.
Tuwe wakweli kabisa amethubutu.
Hata kama wataachiwa lakini hata jamii inayotoa taarifa imekua na imani naye.
Ni rahisi kwa mtu kumpelekea taarifa kwa sasa mana anauhakika kuwa zitafanyiwa kazi.

Nawashangaa baadhi ya wapinzani uchwara wanamponda Makonda lakini hao hao siku zote wamekua wakiwatuhumu baadhi ya askari kuwa wanashirikiana na wahalifu. Leo Makonda amewataja hadharani halafu wanageuka tena na kusema kuwa ni vidagaa.
Hivi polisi 12 wa vyeo tofauti mpaka kamishna ni vidagaa. Walitaka atajwe nani?
Na kama kuna aliyeachwa basi wamtaje au wampelekee Shujaa wetu Makonda ili awataje.
Walizoea kumtaja Lowasa tu kuwa ni fisadi ili kujipatia umaarufu wa kisiasa. Sasa wawataje hao mapapa. Kama walimtaja waziri mkuu sasa wanamuogopa nani tena? Wamsaidie Makonda na IGP kuwataja hao mapapa!
Makonda aendelee na kazi yake na wananchi tumezidi kujenga imani kubwa kwake. Ni mtu wa vitendo. Kuna wakati mkuu wa nchi aliyepita alipelekewa majina kama hayo lakini alishikwa na kigugumizi kuwataja hadharani. Hao aliowataja makonda ni Mwanzo tu na ameweza kuonyesha mfano wa kuweka woga pembeni.

Makonda ametumia mbinu ya hali ya juu kuwataja hao wanaotuhumiwa. Kwa sasa ndio watu watajitokeza kwa wingi kuwataja wahusika wote .

Ikiwezekana Makonda ateuliwe kuwa Mbunge kabisa ili ateuliwe kuwa Naibu waziri wa Mambo ya ndani amsaidie Mwigulu kuendesha wizara hiyo.

Wanaomponda wanasahau kuwa Makonda pia ni binadamu na mwanasiasa. Akisubiri kila kitu akifanye kwa usahihi basi hatafanya kitu chochote.
 
Sasa umeanza kunielewa...!

Yani itakuwa ni aibu kubwa kwa Mkuu wa mkoa kama atakiri kwamba aliwaita hao watu kituoni kwakuwa wanatumia dawa za kulevya(huu utakuwa upuuzi wa kiwango cha lami)
Ivi unajua nchi hii ina watu wangapi wanatumia dawa za kulevya???

Na itakuwa ni aibu kubwa kwa RC kama atasema niliwaita ili waeleze ni wapi wanapata huo unga wanao tumia..! Kwaaababu njia za kipelelezi za polisi ziko wazi za namna yakupata taarifa za wahalifu...bado njia hizo zingeweza kutumika kwa wasanii hao hao bila kuharibu utu wao...!

Hapa RC ili awe salama ni lazima aseme hawa watu ni wafanya biashara wa dawa za kulevya na lazima awapeleke mahakamani kwakuwa unaposema mtu anafanya biashara fulani maana yake una ushahidi na vidhibiti vya kutosha kumtia hatiani..!
Sasa wewe unapata wapi uhakika kama huyo RC hana vithibiti na ushahidi wa kutosha?
Mbona wakimbilia kuwatetea watuhumiwa bila kujua RC ana ushahidi au lah?
Kwenye hili huoni na wewe unatenda kosa hilo unalolihubiri la kuhukumu pasipo ushahidi?
Maana ni dhahiri ninyi wote watetezi wa hili tayari mnamuhukumu RC kwa kuwatuhumu hawa bila kujua kuwa anao ushahidi au lah.
 
Endelea kusema no easy money, kama unataka kujua kuna easy money nenda ITV wewe mwenyewe umtangaze Wolper anajihusisha na madawa ya kulevya uone yatakayokukuta. Usijifiche kwenye mgongo wa msafisha viatu fanya mwenyewe uone!!
Kwa mawazo yako hiyo easy money kwa makonda ataipata??Jifariji..halafu ukiona mtu anatoka sana mapovu ni team sepenga.Makonda anakwambia alifanya uchunguzi wake kajiridhisha kuwataja..sasa mi nimtaje wolpa nimemchunguza kwa lipi na kwa kazi gani?co kazi yangu...makonda kaza usilegezee...
 
yeye Nape alipomtaja Lowasa kama fisadi mkuu alikuwa na ushaidi gani? huyu nape kawaida ya kuona wivu kwa wapiga kazi.
 
Makonda mnafiki mkubwa

sawasawa na mnawinda porini mara baada ya kuwaona wanyama wanachunga mbugani .......anazuka makonda kutoka nyuma kwa sauti ya juu kabisaa

naomba bundukiii

naomba bundukiii

jamani yeeee, naomba bundukiiii


wanyama wanasikia kilele za makonda...bila ajizi wanyama wanakimbia nakutoweka kwa kasi machoni.....nyoote mnapigwa na butwaa maana kelele za makonda zimewajulisha wanyama kwamba kuna hatari......kuna hatariii.....kimbieni mkajifiche...nao wakakitoa.


Vita yoyote hupiganwa kwa strategies je maload wa dawa za kulevya

hawajasikia makelele ya makonda?

hawajaficha ushahidi?

hawajaandaa utetezi?

Makonda nibwege nambari moja na kwa hakika alichokifanya anakifaham 100% kwa faida yake

Vita sio lelemama na haipiganwi hivo.
Kwa hoja hii nakubaliana na wewe. But kwa hoja ya kuchukua hatua hata kama ni ndogo lakini ikiwa na lengo la kuikumbusha jamii kuhusu janga la madawa ya kulevya bado nitamuunga makonda mkono
 
Vita vya madawa ya kulevya havina universal principals za kufuata ndio maana huko Philippines kwa Raisi duterte , MTU kama wema sepetu Leo angekuwa ameshazikwa ....


Na kwa taarifa yako.... Vita dhidi ya madawa ni Kuua tu... Hakuna nchi iliyofanikiwa kutokomeza kama si kupunguza drugs bila kutumia RISASI...


Huku kufuata protocols na michakato ndiko kunatoturudisha nyuma Africans... Vita hii watu wapotezwe tu
Absolutely true
 
Na hapo bado chibu dangote anapeta uraiani, siku akitiwa mbaroni sijui hali itakuwaje kwa wanasiasa wetu.Go Makonda go taifa zima liko nyuma yako, wewe ndio Jemedari wa hii vita!
 
Kwahili, JPM mteue Makonda kuwa mbunge kabisa, kafanya kazi nzito yenyekuhitaji pongezi, tena amwongezee na ulinzi.

Tundu Lissu alimtaja Lowassa mara kadhaa ila mateja kashindwa kutaja hata viluwiluwi.

Kaka Makonda komaa nao tu hapo uliposhika ndio penyewe kabisa.
 
Ipo siku sitashangaa kuona Makonda na mkuu wa polis wakiburuzwa mahakamani labda waathirika wawe na akili za mbayuwayu.
 
Always ukimsikiliza Makonda Ana nia nzuri ila anakosa utafiti WA kutosha.
kwann?

tuanze Na suala la nauli bure kwa walimu, sasa ivi ndio kweli ingekuwa Safi walimu kupewa smart card free ya kusafiria kuliko kubana vyombo binafsi.

swali zipo daladala toka kimara Adi kariakoo Na posta walim huenda bure, lakin akipanda mwendokasi sio tena 400 Bali 650 je tatizo la kulipia nauli toka 400-650 je limempunguzia Mwl mzigo au limemuongezea gharama? hapa ndio leadership ionekane, vp ushawishi wake ukubalike kwa vyombo binafsi halaf yeyr akiwa yupo serikalini asifaninikishe walim kusafiri bure# 1st challenge.

kulikuwa Na suala la wakazi WA dar kupaka rangi nyumba. ngoja kwanza nicheke hahahahaha. MTU hajui atakula nn apake nyumba rangi. hivi tunaxingatia reality ya maisha ya mtanzania kweli. mm kuna nyumba nilipanga miaka nennda rudi HT ndani kwenyewe hakuna rangi Leo apige rangi nje.hii nayo haijufanyiwa utafiti kwenye ground

mwisho ni suala la sembe, bangi. hivi mtaani kila mahala vimeenea, mateja HT ukikaa stwndi wapiga debe kibao ni mateja. nauliza kuna tofauti gn ya mpiga debe na celebrity ltk kutumia sembe.

tunataka list of drug dealers sio drug users.

ukimkamata mtumiaji wakati supplier anadunda utakuwa unafanya nn? we need high profile drug dealers,politicians and businessmen watajwe.


Usionewe wala usionee watu, haki iwe ndio muongozo wetu.
 
Aseme kama ni miongoni mwao,Maana anataka iwe siri kuwajibisha wakati kila mtu anajua fulan anatumia na fulan hatumii
 
Back
Top Bottom