Dawa za Kulevya: Nape aasa "Tusiwahukumu watu kwa Tuhuma, kubomoa brand ya mtu/taasisi ni sekunde"

Kwani ameambiwa kina makonda hawana busara? Nadhani aviachie vyombo vya dola vifanye Kazi Wasanii wako chini ya Wizara yake lakini alikaa kimya sasa anajitia kusema
 
Victoire Na wewe uza madawa makonda akukamate kama Wewe tukuone kama utalipwa Wema mnamtetea bure ni mhusika subiri mziki wake
 
Kwa dunia hii ya sasa na kwa mtu mwenye akili timamu huwezi chagua kiongozi eti sababu ya kuwapo wasanii katika kampeni, mfano mzuri ni uchaguzi wa Marekani, mbali nakuwa na msafara lukuki wa wasanii Mama Clinton bado alipoteza........ Kinachoangaliwa ni nani anataka kutuongoza, ana sifa zipi, ana maadili gani na ana sera zipi zinazotupeleka mbele na zina maslahi yapi kwa Taifa. Maisha ya kijinga kijinga hayana nafasi karne hii, kila mtu lazima afuhate sheria za nchi hata kama wewe ni msanii nguli namna gani.
Akili za wamerakani si zawabongo wewe.
 
Makonda aendelee na kazi. Hata kama wanasema anadeal na dagaa si haba. Hata ukimuondoa dagaa katika uhalifu unakuwa umepunguza effect katika jamii. Huyo Papa unatafuta namna ya kudeal naye kimyakimya.

Hata Escobar alitafutiwa namna ya kummaliza. It is just a matter of time and courage to do so.

Nape analitazama hili katika kuiharibu status quo ya mtu. Je, amejiuliza kama hizi status quo zitakuwa zimetokana na uhalifu ambao umeharibu jamii kubwa mbali na kusaidia kumtengenezea mtu mmoja jina?

Hii nchi ni ya Watanzania. Si ya mtu mmoja mmoja. Mtu mmoja mmoja anyenyekewe na wanaofaidi toka kwake. Kwa Watanzania, jamii pana ndiyo kipaumbele chetu.

Hata Makongoro Nyerere alikwenda kupigana vita ya Kagera ili kuwalinda watanzania. Mwalimu angethamini uthamani wa mtu mmoja mmoja, basi asingeruhusu mwanaye akapigane. Ndivyo nionavyo juu ya hii issue ya Brands na Names zinazoonekana kuwa zitaharibiwa kwa tuhuma at the expense of Tanzanians (men, women, youth and children).

Tuhuma hazijatoka hewani. Ni yangu imani source ya tuhuma ni wahusika ama watumiaji ama intelijensia ama wauzaji wenyewe.

Aache taratibu zifuate mkondo wake. Angekuwa anathamini brands and names, angesha hakikisha Ray C na Chid Benz (walioharibu brands and names zao kupitia madawa) wanasaidiwa kwa kuwakamata wale wanaowauzia.

What is a brand and those big names to him? Watanzania wa chini wabaki wanaumia kisa brands and names? What a joke to Tanzanians?
Asante mkuu,naona umeweka HOJA.
 
Uchunguzi wa nini wakati tayari polisi wanao ushahidi? Hivi wewe hujui Mkuu wa mkoa ni mwenyekiti wa kamati na ulinzi wa mkoa? Yaani hujui usalama wa taifa na polisi wapo chini yake? Hivi wewe unadhani Makonda kakurupuka tu?? Nape naona hapa anaropoka hajui alisemalo.
Nape kama nayeye unasema amekurupuka basi ujue huko kwenye serikali hakuna mawasiliano mazuri.kila mtu inaonekana anataka kupamba vichwa vya magazeti na blogu
 
CCM oyee, CCM oyee, HAPPY BIRTHDAY to you! Jamani, jamani njooni huku leo ni nderemo na vigelegele. Lile vuvuzela la ugambani lililostaafu (ambalo halikuwahi kuonesha hata chembe ya busara) leo kwa mara ya kwanza, baada ya kushikwa pabaya, linasema "Lazima itumike busara, tusiwahukumu watu kwa tuhuma,kutengeneza brand ni kazi kubwa sana wakati kuibomoa ni jambo la sekunde tu." Haya ni mageuzi yanayostahiki nderemo. CCM oyeee, Kigumu chama cha mapinduzi.
 
Ishu ya majambazi aliamka usiku wa manane akiwa amevaa gwanda za polisi tayari ndani ya nusu saa. Hakungoja muda wake wa kuongea ufike.

But hili la madawa wasema ataongea muda wake ukifika. Really?

Issue ya madawa ya kulevya inahitaji utulivu wa ubongo na uwindaji wa mikakati na mbinu stahiki sio kupiga kelele na kucheza na media maana hutapata mtu wala ushahidi.
Kwa kelele zilizokwishapigwa sidhani kama don yoyote anaweza kukamatwa na ushahidi.Kesi imeshavurugika.
 
Hii ni mifano hai kwamba mtu maarufu ukimdhalilisha bila ushahidi sio sawa.Huyu alishawahi kuwa Miss Tanzania.Baba yake ni mtu maarufu sana nchini.Lazima ujiridhishe kabla ya kumdhalilisha.
Watu kama hawa ilitakiwa wakamatwe wakati ushahidi usio na shaka umeshapatikana na moja kwa moja anafikishwa mahakamani.
Hii ya kusema upelelezi unaendelea ina maana ushahidi bado haujakamilika na huenda akawa hana hatia.

Naunga Mkono sana Kauli ya nape kwamba Watu waliojijengea umaarufu kwa gharama kubwa wafanjiwe utafiti wa kina kabla ya kutangazwa hadharani.
Farudume so unaamini Makonda alilala usiku akaota WEMA wako anahusika na dawa za kulevya ndipo akamuita?
 
Baba Rizi aliwahi kukiri mara kadhaa kukabidhiwa orodha ya majina ya hawa watu lakini ndio kama hivyo akapotezea hadi leo.

Moja kati ya wapambanaji ambao nyota yao ilizimwa ghafla baada ya kuingia kwenye hii vita ni Amina Chifupa (Rest In Eternal Peace) na hadi leo yale majina yaliyo kabidhiwa pale magogoni hatusikii chochote.

Baba Rizi sio kwamba alipotezea bali alideal nayo kwa njia stahiki na wengi walikamatwa na kushughulikiwa ila Amina alikurupuka kwa kutaka sifa kwenye media mwishowe ndio yakamkuta yaliyomkuta.
 
Hoja ni hii: mateja mbona si wa kutafuta. Yaani wapo tu kama wslivyo watumiaji wa shisha na masister du. Hao mastar wanaofanya wanachofanya kwa kujificha ni kioo cha jamii na huwezi kuwatangaza hadharani kwa tuhuma pekee. Eti "inasemekana wanatumia". It's absurd, in the real sense of the word!
Wasitajwe wao kina nani? Taifa linaangamia unaleta ustaa mpaka kwenye ngada? Kafanya vizuri kuwatangaza kwa kuwa wao ndio kioo cha jamii na walitakiwa wewe mfano bora kwa jamii. Safi sana mkuu wa mkoa.
 
Farudume so unaamini Makonda alilala usiku akaota WEMA wako anahusika na dawa za kulevya ndipo akamuita?

Swala sio kuota bali swala ni kwamba celebrity kama wale wanatakiwa wakikamatwa wanapelekwa Mahakamani moja kwa moja.Ina maana imeshadhibitika bila kuacha shaka kwamba ni drug dealer na ana kesi ya kujibu.Sio kuendelea na upelelezi.
 
Who knows? may be ni mateja hao hao wa Temeke,sinza,uwanja wa fisi ndio waliotoa ushirikiano mpaka hao jamaa wamechukuliwa....
TUENDELEE KUUNGA MKONO JUHUDI HIZI, ni ngumu lakini lazima jambo lifanyike,na ni lazima pawepo na wapiganaji mstari wa mbele.
 
Issue ya madawa ya kulevya inahitaji utulivu wa ubongo na uwindaji wa mikakati na mbinu stahiki sio kupiga kelele na kucheza na media maana hutapata mtu wala ushahidi.
Kwa kelele zilizokwishapigwa sidhani kama don yoyote anaweza kukamatwa na ushahidi.Kesi imeshavurugika.
Brother nikurudishe kwenye hoja kidogo. Tulikuwa tunazungumzia ukimya wa Mwigulu.
Naam so issue ya majambazi ndo inahitaji media bila utulivu wa ubongo lakini ya madawa inabidi ubongo utulie?
 
Back
Top Bottom