Pagan Amum
JF-Expert Member
- Aug 28, 2015
- 1,932
- 4,400
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye amesema wizara yake inaunga mkono mapambano dhidi ya madawa ya kulevya kwani kwa namna moja ama nyingine yanadhoofisha nguvu kazi ya vijana. Kama Wizara Tunaunga mkono juhudi za kupambana na jambo hili.
Lakini ni Vizuri tukaangalia tunalifanya katika namna ambayo inalinda haki ya mtuhumiwa ya kumpa room ya kesho na keshokutwa kama ikithibitika kwamba hahusiki bado atakuwa na heshima ambayo alikuwa ameitengeneza. Mateja ni wengi sana mtaani ambao yaani huhitaji rocket sayansi ya kwenda kuwachukua.
Ukienda Temeke utawakuta, wapi utawakuta Manzese Sinza utawakuta, Uwanja wa fisi wapo wengi tu. Kama kweli unataka kujua madawa yanatoka wapi, get this people, wapo tu mtaani wengi tu.
Hizi ni baadhi ya nukuu za Nape:
=> 'Lazima itumike busara, tusiwahukumu watu kwa tuhuma,kutengeneza brand ni kazi kubwa sana wakati kuibomoa ni jambo la sekunde tu'
=> 'Kama Wizara tunaunga mkono juhudi za kupambana na dawa za kulevya, tatizo ni namna ya kushughulika na wahusika ikiwemo busara'
=> 'Tunaunga jitihada za mapambano lakini ni vizuri lifanywe katika namna ya kulinda haki ya mtuhumiwa ili heshima yake isipotee'
=>'Nakiri kwamba tatizo la dawa za kulevya ni kubwa, watumiaji ni wengi lakini wanaoonekana zaidi ni wale wenye majina makubwa'
=> 'Muhimu sana kulinda haki na suala la utaratibu uliotumika kwa watuhumiwa wa madawa niiachie jamii iendelee kujadili na kuamua'