Dawa ya UKIMWI yagunduliwa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dawa ya UKIMWI yagunduliwa?

Discussion in 'JF Doctor' started by Tasia I, Jul 14, 2010.

 1. T

  Tasia I JF-Expert Member

  #1
  Jul 14, 2010
  Joined: Apr 21, 2010
  Messages: 1,226
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Monday, 12 July 2010

  [​IMG] [FONT=Tahoma,Calibri,Verdana,Geneva,sans-serif]
  B[/FONT]endera ya Marekani nchi ambayo wanasayansi wake wanadaiwa kuwa wamegundua dawa ya Ukimwi

  Leon Bahati

  WANASAYANSI nchini Marekani wamegundua chembechembe za kinga ambazo zinauwezo mkubwa wa kupambana na kuua virusi vya ugonjwa wa Ukimwi ambao hadi sasa hauna chanjo wala tiba ya uhakika.

  Ugunduzi huo tayari umethibitishwa na wataalamu mbalimbali, ikiwemo Mamlaka ya Chakula na Dawa ya Marekani.


  Vyombo mbalimbali vya habari vya kimataifa vimeripoti kuhusu ugunduzi huo ambao unaelekea kutoa mapambazuko mapya kwa ugonjwa huo hatari ambao umekuwa ukiathiri nguvu kazi sehemu mbalimbali duniani, hususan nchi zinazoendelea.


  Wanasayansi hao wa Taasisi ya Magonjwa ya Kuambukiza na Mzio (Niaida) walieleza katika taarifa yao ya wiki iliyopita kuwa kwenye utafiti huo wamebaini aina mbili za chembechembe zinazoweza kumsaidia binadamu kupambana na virusi vya ukimwi.


  Mkurugenzi wa Niaida, Dk Anthony Fauci alizitaja chembechembe hizo za kinga kuwa ni VRCO1 na VRCO2 ambazo utafiti wake umeonyesha kuwa zinaweza kuua virusi vya ukimwi kwa asilimia 90.


  Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) dawa huthibitishwa pale uwezo wake wa kupambana na ugonjwa unapozidi asilimia 60.


  Dk Fauci alisema hayo ni mafanikio makubwa ya kisayansi tangu wataalamu mbalimbali duniani waanze kufanya utafiti wa namna ya kutibu ugonjwa huo.


  Alisema chembechembe hizo za kinga hizo VRCO1 na VRCO2 zinaweza kutumika katika kubaini aina mpya ya chanjo ambayo itamuwezesha binadamu kuwa na kinga dhidi ya virusi vya Ukimwi.


  Kwa namna chembechembe hizo zinavyofanya kazi, alisema, zikitumika kama chanjo, mwili wa anayechanjwa unajenga kinga ambayo inavishambulia virusi vya Ukimwi na kuviua.


  “Kwa sasa soko lina dawa za kupunguza nguvu na kasi ya virusi vya Ukimwi kuathiri chembechembe nyeupe za kujikinga na maradhi na hakuna tiba,” alisema Dk Fauci.


  “Lakini utafiti huu ni njia mpya ya kuelekea kupata ufumbuzi wa kudumu katika utaalamu wa tiba.”


  Hata hivyo, alisema utafiti huo unaweka matumaini zaidi katika kutoa chanjo ingawa baadaye utawezesha kusaidia kupatikana kwa tiba kamili.

  Jinsi walivyoendesha utafiti huo, Dk Faci alisema walichukua sampuli mbalimbali za damu zenye virusi vya ukimwi kutoka maeneo mbalimbali duniani.


  Katika sampuli hizo, alisema waliweza kupata aina karibu 200 za virusi vya ukimwi na walipozipambanisha na chembechembe za kinga za VRCO1 na VRCO2, virusi vilikufa bila kuathiri chembechembe nyingine za damu.


  Hali hiyo aliilezea kuwa inathibitisha kuwa VRCO1 na VRCO2 zina uwezo wa kupambana na aina zote za virusi vya ukimwi.

  Haya jamani habari njema ndo hizo, ila kwa me navoijua Africa hi sasa itaweka kiburi cha kuafanya ngono zembe kwa kiasi kikubwa hata hata kama chembechembe hizi zitakua na uwezo wa kuua kweli virusi vya ukimwi.

  Matokeo yake yatakua kuri kwa kasi kwa yale magonjwa ya zinaa ya zamani kama kswende na gonorea na mengine, mimba kibao zisizotarajiwa, na matokeo yake watotot zaidi wa mtaani, vibaka, mateja n.k
   
 2. M

  Mkandara Verified User

  #2
  Jul 14, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Hizi habari za dawa kupatikana zinatangazwa Bongo tu au?.......
   
 3. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #3
  Jul 14, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Ngoja tusubiri tuone ...Kakini Dawa kubwa ya ukimwi ni kuacha ngono zembe
   
 4. M

  Mkandara Verified User

  #4
  Jul 14, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Kwa sura nayoiona hapo juu itakuwa kazi kubwa kuacha ngono zembe hasa ukizingatia hiyo signature yako maanake tuisha katazwa hiana....Haaa haaa haaa!
   
 5. Bourgeoisie

  Bourgeoisie JF-Expert Member

  #5
  Jul 14, 2010
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 611
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Kugunduliwa kwa tiba hii hakuji kutangua amri ya "MSIZINI".
   
 6. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #6
  Jul 14, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,771
  Likes Received: 218
  Trophy Points: 160
 7. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #7
  Jul 14, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Sijui kwa nini hii habari imeletwa kwenye jukwaa la Siasa!
  Anyway,
  Kwa mujibu wa habari hiyo, sidhani kama ni dawa kama dawa hasa ila nafikiri ni kama ARV ambayo inapunguza tu makali ya virusi vya ukimwi na si kutibu.
  Itakuwa ni good news kama itapatikana dawa ambayo itatibu kabisa.
   
 8. R

  Rayase Member

  #8
  Jul 14, 2010
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 82
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
 9. jossey1979

  jossey1979 Senior Member

  #9
  Jul 14, 2010
  Joined: Apr 28, 2008
  Messages: 168
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hii habari nimeisikia asubuhi. Lakini presentation ya hii habari bado haieleweki vizuri kama ni kinga, Chanjo au inatibu kabisa.

  But kama ni kweli hawa jamaa watakuwa ma-billionaires
   
 10. mujusi

  mujusi JF-Expert Member

  #10
  Jul 14, 2010
  Joined: Jan 22, 2010
  Messages: 237
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Kinga kubwa ya Ukimwi ndio kuacha ngono dawa ya ukimwi hakkuna hadi sasa samahani kwa kuiweka sawa sentense yako.
   
 11. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #11
  Jul 14, 2010
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,918
  Likes Received: 2,068
  Trophy Points: 280
  Hivi ni 'dawa' ya UKIMWI au 'kinga' dhidi ya VVU?
   
 12. Mlalahoi

  Mlalahoi JF-Expert Member

  #12
  Jul 14, 2010
  Joined: Aug 31, 2006
  Messages: 2,065
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Hii habari inachanganya,na kwa mtizamo wangu kinachochangia mkanganyiko huo ni matumizi ya neno DAWA. Angalia habari excerpt hii
  SOURCE

  Na wakati Waziri Mwakyusa amefuata mkumbo wa kupongeza upatikanaji wa "dawa" hiyo,huko Marekani the latest news ni kama HII ambapo suala la "ugunduzi wa tiba" haligusiwi kabisa.

  Wakati kila mmoja wetu anatamani tiba ya ukimwi ipatikane hata leo ikiwezekana ni muhimu taarifa hizi za kitaalam zikafafanuliwa kitaalam pia.Habari kamili ni hii hapa chini


  SOURCE
   
 13. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #13
  Jul 14, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,771
  Likes Received: 218
  Trophy Points: 160
  FL1, Yango na yango ndiyo jadi yetu waafrika, kinga unayoongelea wewe ni nadharia ya kwenye vitabu na mdomoni tu lakini kiukweli kama na hii si dawa basi space za kuzikia tutakosa.
   
 14. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #14
  Jul 14, 2010
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,918
  Likes Received: 2,068
  Trophy Points: 280
  Weneyewe waliofanya utafiti wametoa taarifa hii hapa(NIH-Led Scientists Find Antibodies that Prevent Most HIV Strains from Infecting Human Cells):

   
 15. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #15
  Jul 14, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  yote tisa.. kumi ni kuzingatia mahubiri ya mtumishi mpakwa mafuta NABII NA MTUME TITO,,


   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 16. PhD

  PhD JF-Expert Member

  #16
  Jul 14, 2010
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 3,819
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  uuhhhh afadhali kula vitu kwa kwenda mbele sasa.
   
 17. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #17
  Jul 14, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,945
  Likes Received: 2,090
  Trophy Points: 280
  Mimi sijaipenda dawa au kinga hii kwani ugonjwa huu kwa asilimia 99 ni wakujitakia! Sasa sample zilikuwa 200 je, hii sample ni representative? Je, kama kuna aina ya 201, itakinga au kutibu? Mungu hajaribiwi!
   
 18. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #18
  Jul 14, 2010
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,313
  Likes Received: 5,605
  Trophy Points: 280
  Dalili nzuri na yenye mafanikio poleni sana wataalaam mnaokesha....ngoja ifanyiwe majaribio ya kutosha kwa mabara yotendio waipitishe
   
 19. K

  Kanyafu Nkanwa JF-Expert Member

  #19
  Jul 14, 2010
  Joined: Jul 8, 2010
  Messages: 812
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  AIDS Breakthrough!!III


  Jul 8, 2010 6:12pm by James Grimes

  This is great news!! Hopefully this will be able to help a lot of people before the AIDS epidemic kills more people.


  Amplify’d from www.foxnews.com

  U.S. researchers discovered two powerful antibodies that neutralize more than 90 percent of all known strains of the HIV virus in the lab, new research released Thursday showed.
  NIH-led scientists discovered the antibodies known as VRCO1 and VRCO2 that prevent most HIV strains from infecting human cells. The find is a potential breakthrough for advancing HIV [SIZE=+0]vaccine[/SIZE] design, and antibody therapy for other diseases.
  The authors, whose work was due to be published in the July 9 issue of Science, were also able to demonstrate how one of these disease-fighting proteins [SIZE=+0]gets the job[/SIZE] done.
  “The discovery of these exceptionally broadly neutralizing antibodies to HIV and the structural analysis that explains how they work are exciting advances that will accelerate our efforts to find a preventive HIV vaccine for global use,” said Dr. Anthony Fauci, director of the National Institute of Allergy and Infectious Diseases (NIAID), National Institutes of Health.
  “In addition, the technique the teams used to find the new antibodies represents a novel strategy that could be applied to vaccine design for many other infectious diseases,” Fauci stressed in a statement.
  The team of virologists found that the two antibodies were produced naturally and found in the blood of HIV-positive people.
  They were able to isolate these antibodies using a new molecular device they developed. It zeroes in on specific cells that make antibodies against HIV. The device is an HIV protein scientists modified to react only with antibodies specific to the site where the virus binds to cells it infects.
  Leading two research teams were NIAID scientists Peter Kwong, Ph.D., John Mascola, MD, and Gary Nabel, MD, Ph.D.
  “We have used our knowledge of the structure of a virus — in this case, the outer surface of HIV — to refine molecular [SIZE=+0]tools[/SIZE] that pinpoint the vulnerable spot on the virus and guide us to antibodies that attach to this spot, blocking the virus from infecting cells,” explained Nabel.
  Mascola added that: “the antibodies attach to a virtually unchanging part of the virus, and this explains why they can neutralize such an extraordinary range of HIV strains.”
   
 20. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #20
  Jul 14, 2010
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,323
  Likes Received: 1,788
  Trophy Points: 280
  Bwana wewe AIDS is still a threat..imagine mtu maskini anayeugua AIDS kule kwetu Kayenze, pembeni mwa ziwa victoria,ambaye hata dawa za malaria tu bado ni issue, atawezaje kupata faida ya reaserch hizi zilizoko lab za Marekani? Hapa we talk something of months or years before we get the benefit.
   
Loading...