Dawa ya swali 'Namba yangu umeitoa wapi?'

Dawa ya swali 'Namba yangu umeitoa wapi?'

Huu mtego wa kizamani utakamata fungo tu
Ukipewa namba na mtu mwingine ili kuepuka swali hili la kizushi (namba yangu umetoa wapi?) chakufanya mtumie muamala mfano 200,000/-
Baada ya dakika chache mpigie na kwa upole mwambie kuwa umekosea kutuma hela ukatuma kwenye namba yake. Mwambie unaomba akurudishie ILA katika hio 200,000 akurudishie 100,000 tu iliobaki abaki nayo kwa usumbufu uliotokea. Then harakati unaanzia hapo hachomoi huyo

Kwa kufanya hivi unakuwa umeonesha wewe ni mstaarabu na sio mbahili,sifa hizi zinawavutia Sana dada zetu
 
Mwanaume wa kweli hanunui upendo

Hii sio dawa wala

Kwako wewe, wengi wetu tutaishia kusema huyu baba ana roho nzuri! Kama hanijui kanipa laki akinijua je?

Kina baba basi msitume laki, fanyeni millioni kabisa.

Eeh! Unapiga simu dada/ mama kumwambia umetuma kwa bahati mbaya, ila sio kitu labda ni Mungu alipanga hiyo riziki iende kwa mlengwa. Mungu fundi bwana.

Baada ya hapo baba mind your business!
 
Usitu generalize. Unatakiwa uspecify hii njia wana tumia akina nani na kina nani hawapaswi kutumia maana kuna hatari ya watu kujaza pipa la Lita 150 machozi. Tunaona sana wana wanatuma nauli na hawaonekani ni gentlemen inakuwa imetoka; Leo u risk 200k, Hapana!

Mimi nakumbuka kuna broad aliwahi kuniuliza nimetoa wapi namba yake, and I said, "Vodacom wamenipa kama zawadi kwa sababu natumia sana huduma zao". She laughed na kilichofuata ni history.!

Muda mwingine sio hela. Hela inamfanya acheke/afurahi. If you can make her happy, your chances of getting her are alive than the number of people who have died.
Mind you: Ukianzisha mahusiano kwa hela bai basi pattern isibadilike. Ikibadilika tu, You lose her.
 
Back
Top Bottom