Dawa ya michepuko imepatikana,kama ni wewe ungefanyaje?

Dawa ya michepuko imepatikana,kama ni wewe ungefanyaje?

Idd Ninga

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2012
Posts
5,539
Reaction score
4,856
Jamaa fulani jina linahifadhiwa kapuni alifunga ndoa juzi juzi na mtoto mmoja mrembo tena kabinti cha ukweli.Wiki mbili tu baada ya ndoa jamaa aliamua kudhihirisha kuwa yeye ni mtaalamu mwenye diploma ya kuchepuka.

Aliamua kwenda klabu na kumtafuta mtoto wakike kisha kwenda kupiga kilevi a.k.a tungi.Baada ya kulewa sana, jamaa na mchepuko mwenzake waliamua kwenda guest house na kulala mpaka hasubuhi.

Palipokucha jamaa kushtuka kutoka usingizini kakutana amelala na bonge la kidume.Jamaa bila ya kuuliza wala nini,kahamka kitandani, kavaa suruali tu na kuondoka kifua wazi,miguu peku peku hadi nyumbani huku analia.

Mke akamuliza kuna nini mume wangu mbona unalia na jana ulilala wapi? Kama ni wewe mwanaume ungefanya nini na kama ni wewe mwanamke ungemwambia ukweli.
 
Hadithi,hadithi.Hadithi njoo,uongo njoo utamu kolea!!
 
Back
Top Bottom