Dawa ya michepuko au nyumba ndogo hii hapa

Dawa ya michepuko au nyumba ndogo hii hapa

NI MTAZAMO TU

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2014
Posts
1,203
Reaction score
1,001
Wadau JF salam,
Kimekuwa kilio cha wanadaoa wengi sana kwenye familia zao juu ya ujio wa michepuko au nyumba ndogo.. na niongeze kwa kusema imekuwa kama kamtindo fulani sasa kwa wanandoa..

Naomba niwarudishe kidogo kwenye asili ya mtu mwesi, kwa haraka nikifuatilia naona asili yetu kabla ya ujio wa wazungu au wakoloni na sera zao za mke mmoja kwa kila familia, babu zetu walikuwa na wake zaidi ya mmoja, hapa nisimung'unye maneno, yaani walikuwa na wake wengi sana..

Na kama msomaji wa mada hii, haukubaliani na nami hebu jiulize tafadhari, kwenye familia yako kama unafatilia histoa ya ukoo wako utagundua BABU YAKO WA BABU YAKO ALIKUWA NA MKE ZAIDI YA MMOJA,Maana yake wake wengi.

Sasa wadau mkubaliane na mimi kama tunaamini kuwa kuna magonjwa ya kurithi kwenye koo kwanini kusiwe na kurithi hizi tabia za MABABU ZETU WA KIAFRIKA ZA KUWA NA WAKE WENGI,,

Ninacho amini mimi nikuwa,tatizo la michepuo au nyumba ndogo lililo ingia sasa ni issue ya kurithi, ijapo kuwa tumeucha utamanduni wetu na kufuata wa kishenzi, namanisha wa kizungu wa kuwa na mke mmoja..

Lakini lengo la mzungu lilikuwa kupunguza idadi ya sisi kuzaliana wakati tu tegemezi..

Mtazamo wangu, inabidi mabinti walikalie kikao kulijadili kwa kina na haswa kwenye makicheni part, kuliko kuacha hali ilivyo sasa,na ufumbuzi wao waulete hapa JF na sisi wababa tutauchangia..

Karibuni sana wadau..!!
 
mimi sio mdau wa michepuko..! lakini pia sina tatizo na wachepukao wana sababu zao, tusiwalaumu tusiwahukumu
 
Ngoja, ngoja niwasubiri wahusika waje kufunguka
 
Kuna logic isipokua bado sikubaliani wewe, enzi za hao babu zetu rasilimali zilikua nyingi sana, hivyo hata wangekua na wake kumi kila mmoja na watoto 5 waliweza kuwa tunza.
Pia fedha ilikua na dhamani kubwa kuliko sasa mdau hivyo BAKI NJIA KUU.
 
Unajua kinachotia shaka kwa sasa, wadada wengi ukiwauliza wanakuambia wamechoka kulia kuhusiana na michepuko kwa wababa, sasa nao wanasema dawa ya moto ni moto, yaani jino kwa jino...

Sasa hiii ni hatari sana kwa mwanamke kulipiza kisasi ili kujilidhisha...ndio maana nina tamani watambue tulipotoka..wazungu tu ndio walitubadilishia mfumo wetu wa maisha wadau
 
kawaida sana, kuchepuka ni sehem ya maisha..
 
Qur-an ilisha turahisishia mambo,sisi ndo tunaojitia ujeuri kwa kufuata mambo ya kupangiwa na binadam wenzetu.kwanza tukumbuke wanawake ni wengi kuliko wanaume,sasa ikiwa kila mwanaume ataoa mke 1 hao wanawake anaobaki waende wap?haja zao atazitatua nani km co kusumbua ndoa za wenzao?
 
Enzi hizo unachukua mihogo na majani ya maboga shambani unakula na familia. sasa hivi maisha ni magumu hakunaga
 
mimi sio mdau wa michepuko..! lakini pia sina tatizo na wachepukao wana sababu zao, tusiwalaumu tusiwahukumu

Michepuko ni sawa na mtu kuacha kazi mahali fulani sababu ya kero na kuhamia kazi mpya isiyo kuwa na kero za awali!
 
Kuna logic isipokua bado sikubaliani wewe, enzi za hao babu zetu rasilimali zilikua nyingi sana, hivyo hata wangekua na wake kumi kila mmoja na watoto 5 waliweza kuwa tunza.
Pia fedha ilikua na dhamani kubwa kuliko sasa mdau hivyo BAKI NJIA KUU.
Unamaanisha kama una pesa za kutosha michepuko ruksa?
 
Babu zetu walifaidi neema za ALLAH. Hakukuwa na HIV kama kizazi chetu.
 
Umesema kweli, ngoja niolewe mke wa pili mie.
 
Babu zetu walifaidi neema za ALLAH. Hakukuwa na HIV kama kizazi chetu.

Hata sisi tukitaka kufaidi hizo neema za Allah inawezekana ila ni lazima tukubali kufuata maamrisho yake kikweli na sio kufanya usanii.
 
hakuna aliyekatazwa kuoa wake wengi.as long as wake wamekubali unaji mswati-sha jumanne inaitwa jumatano.maisha ndo yanabana watu wasioe wengi.zama za mababu hakukuwa na maswala yakuuziana viwanja,mke mahari anatoa baba,wanawake waliwapenda waume,ukikosa chumvi jirani anakupiga taff.kwa watoto sasa jeans za sikukuu,nauli ya shule,hela ya mihogo shule,baba rudi na pipi siku hizi wanaagiza mpaka I-PAD hazikuwepo......ukioa watatu kwa wastani wa watoto wa 5 kila mmoja.15 hao baadae unataka bodi ya mkopo ikuhudumie kusomesha..mweeee! yahitaji ujasiri
 
zamani michepuko ilikuwa inafanywa na wababa,ila sasa ivi ngoma droo na wamama michepuko kama kazi,baba anachepuka na mama anachepuka then wanakutana main road
 
Back
Top Bottom