Dawa ya malaria kwa mama mjamzito

Dawa ya malaria kwa mama mjamzito

TUKO PAMOJA ADRENALINE ZISITUHARIBIE CLINICAL MEETING YETU!!!!

Kama angekuwa mgonjwa wangu mie nisingeanza na quinine.!!!! Wewe partner ungeanza nayo Quinine tena per os????!!!!!Kwa indicators zipi???!!!

kaka olesaidimu wewe ungeanza na dawa zipi?
 
Mchezo wa kukatisha dozi sio salama!!!!
Malaria ya kufuga kama hivyo itakuja kulipuka katika hali serious zaid! !!

Kuna ugumu gani wa kutafuta hospitali hata ya wilaya kama hapo ulipo panakuwa pagumu???!!

Ni kweli kaka ni kosa nililofanya lakini sikuweza kuvumilia kwa wakati ule...i was confused nikaona kama kukatisha dozi ndiyo suluhisho!!! nitampeleka mkuu...bali nilikuwa nimehitaji ushauri kwa ninyi wataalamu nijue nini cha kufanya katika nyakati kama hizi maana am new to such situation..hata hivyo yule daktari wa dispensary alitushauri tuanze kliniki kesho, hivyo nitajitahidi kesho nimpeleke wilayani!!!
 
Thanks for your concern...hizi sindano zapatikana kwenye dispensaries? na hutibu malaria kwa mjamzito wa mimba changa???

Zinapatikana hospitali za wilaya, jaribu kucheck nao, zinafaa kwa mimba zenye umri wa zaidi ya miezi mitatu
 
You have already recommended the first choices!

Sijakuelewa, katika hiyo literature zimetajwa dawa tatu, kati ya hizo chloroquine is no longer in the market, ACT ina high rates of miscariage, so among the three, iliyobaki ni Quinine, to me it is the first choice unless kuna contraindications kama za huyu wife wa Ponjoro, in this case I would have gambled, inakubalika kidaktari
 
Last edited by a moderator:
Mama mjamzito anafaa kupewa quinine kwa njia ya drip na sio kwa njia ya vidonge au sindano maana inaweza leta miscarriage wahi hosp hiyo dawa waineutrilize sawa. Ila cku zote quinine ndo dawa ya wajawazito kupitia drip
Kuna indications za kutoa dawa kwa njia ya drip, Quinine ikiwepo, ila ujauzito sio moja kati ya hizo indications, na sio kweli kuwa mama mjamzito hastahili kupewa vidonge au kuchoma sindano za Quinine, suala ku-neutralize hiyo Quinine sijui ulitaka kumaanisha nini, apewe anti dote ya Quinine au awekewe drip? Hivi vitu havipo. Kuhusu miscarriage, watu wanachanganya, malaria kama malaria ni moja kati ya magonjwa ambayo yanaongoza kwa kusababisha miscarriage, hivyo mjamzito akipata miscarriage baada ya kutumia Quinine hatuwezi kuhukumu moja kwa moja kuwa Quinine ndiyo sababisho, yaweza ikawa ni malaria in its own ikawa imesababisha hiyo miscarriage
 
Malaria ni maambukizi ya seli nyekundu za damu inayosababishwa na parasiti iitwayo Plasmodiumu. Plasmodiumu hawa husambazwa na mbu aina ya Anofelesi. Mbu hutoa parasiti za malaria katika damu ya mtu aliyeambukizwa anaponyonya damu 'chakula', na kisha kupitisha parasiti anapomwuma mtu mwingine. Parasiti hukua na kukomaa katika seli nyekundu za damu na mamilioni ya parasiti hukusanyika katika plasenta ya mjamzito.

Malaria inaweza kuwa kali zaidi kwa kina mama walio na magonjwa mengine. Malaria ni hatari zaidi kwa wajawazito kuliko watu wengine.

Dalili za malaria
Mama mjamzito anakuwa na dalili kama wagonjwa wengine ambao sio wajawazito. Dalili hizo ni kama vile


•Baridi (kuhisi baridi isiyo ya kawaida) na kutetemeka (vipindi vikali vya kutetemeka kwa dakika kadhaa na hudumu hadi saa 1), hii huwa dalili ya kwanza ya maambukizi
•Maumivu ya kichwa na udhaifu mara nyingi huandamana na baridi
•Joto jingi mwilini (halijoto ya juu); Joto jingi mwilini mara nyingi hufuatwa na baridi, na joto linaweza kwenda juu sana hivyo mtu anakabiliwa na deliriumu (kutokuwa katika hali sawa kiakili, kuona au kusikia mambo yasiyohalisi)
•Kutokwa na jasho joto lishukapo
•Katika baadhi ya hali zingine kuhara/kutapika kunaweza pia kushuhudiwa
•Dalili nyingine ya kawaida ni maumivu ya misuli/viungo.


Hata hivyo magonjwa mengine yanaweza kusababisha dalili kama hizi.

Vipimo vya malaria
Malaria huweza kugundulika kwa kutumia vipimo vya haraka au hadubini

Matibabu ya Malaria kwa Mama mjamzito
Ni muhimu kwa wajawazito kuepukana na malaria - au kutibiwa haraka wakiwa wagonjwa. Dawa za kutibu malaria zinaweza kuwa na madhara, lakini ni afadhali kuliko kupatwa na malaria. Ikiwa mama ana dalili za malaria, anapaswa kutibiwa mara moja.


Wiki 12 za awali za ujauzito
Kwa kina mama wajawazito ambao hawana malaria kali dawa inayotumika kutibu malaria katika kipindi hiki ni Kwinini na Clindamycin au Kwinini pekee iwapo Clindamycin haipatikani. Dawa hizi zikishindwa kutibu Artesunate hutumika katika matibabu kwa muda wa siku saba.


Muhula wa pili na watatu.
Dawa mseto jamii ya Artemisin zinaweza kutumika katika vipindi hivi kutibu malaria ambayo sio kali.


Madhara ya Malaria kwa Mama mjamzito
Mjamzito aliye na malaria yuko katika hali ya kupata anemia, kuharibika kwa mimba (kutoka kwa mimba pekee yake kabla ya wiki 24 za ujauzito), kuzaa mapema, kupata mtoto mdogo zaidi, kuzaa mtoto aliyekufa (mtoto kuzaliwa akiwa amekufa baada ya wiki 24 za ujauzito) au kufa yeye mwenyewe (kifo cha mama).


Kukinga na Malaria
Kukinga malaria inapaswa kuwa wajibu wa mtu binafsi na jamii.Mama mjamzito afanye kila awezalo kuepuka kuumwa na mbu.Hata hivyo matumizi ya vyandarua pamoja na kuangamiza mazalia ya mbu hupunguza kuenea kwa ugonjwa wa Kukinga malaria inapaswa kuwa wajibu wa mtu binafsi na jamii
 
Je, mama mjamzito akitumia dozi ya Malaria aina ys SP 'wakati akiwa na mimba ya week tatu kuna madhara yoyote?

Mke wangu alikuwa anasikia baridi akashauriwa na muhudumu wa duka LA dawa muhimu atumie SP HUKUAKIWA AMEELEZWA KUWA ANAUJAUZITO MCHANGA.

SASA TOKA SAA MBILI TUINGIE KULALA ANAHANGAIKA TUMBO LINA MSOKOTA HATAKI TWENDE HOSPITALINI.
NIMEMWAMSHA MAMA NASHANGAA WANANIAMBIA NIWAPISHE NIPO SEBULENI TAKRIBANI NUSUSAA SASA.
HIVYO NIMEONA BORA NIJE HAPA NIPATE MWANGA KUHUSIANA NA HILI.

MSAADA.
 
junior Recture, hamna chamimba tena hapo,hata kama ipo uyo mtoto atakaezaliwa atakuwa kimeo
 
Hiyo asp haina tatizo mama mjamzito akihudhuria kliniki lazima apewe asp kuzuia malaria.
 
Naombeni kujuzwa MKE wa rafiki yangu alipewa dozi ya maralia aina ya SP tumbo lilimuuma sana hadi kupelekea ujauzito wake kutoka tena wa miezi 6....sasa ningependa kujua ni dawa gani mwanamke mwenye ujauzito anaweza kupewa zaidi ya SP?
 
Ujauzito ukiwa na wiki 28 na 32 anapewa SP kumkinga na Malaria.

Akiugua malaria anapewa quinine.
 
Anatumia alu kama mimba imekamilisha myezi 3 na zaidi au quinine ambayo haina mipaka ya umri wa mimba..
 
Naombeni kujuzwa MKE wa rafiki yangu alipewa dozi ya maralia aina ya SP tumbo lilimuuma sana hadi kupelekea ujauzito wake kutoka tena wa miezi 6....sasa ningependa kujua ni dawa gani mwanamke mwenye ujauzito anaweza kupewa zaidi ya SP?

lbda alikua na tatzo jngne,mahosptal ya serikali yote znatoa sp kwa wajawazto wa miez 5 na kuendlea....pole yake i can feel the pain
 
Mkuu mpe pole shemeji lakini huwezi kuwa na uhakika sana kama kilichopelekea mimba kutoka ni matumizi ya SP.

SP imekuwa ikitumika kwa wajawazito wenye mimba ya zaidi ya miezi mitatu(zaidi ya wiki kumi na mbili au wiki ya kumi na nne) kama matibabu ya kinga.

mjamzito atakapougua malaria atatumia Quinine au ALU kama alivyogusia mdau hapo juu.
 
Samahanini,

Mimi ni mjamzito mimba ya mwezi mmoja na nusu, tumbo linanisumbua sana. Pia nimepima UTI, hakuna lakini nimekutwa na Malaria tatu.

Sasa nimepewa duphaston kwa ajili ya tumbo na dou-cotexin kwa ajili ya Malaria. Nimekunywa dawa usiku huu, nimetapika na mwili umeniishia nguvu.

Please nishaurini kama naweza pata dawa mbadala.

Natanguliza shukrani zangu kwenu.
 
Back
Top Bottom