The boss wazo lako sio baya sana ila mimi ninachoona tatizo la foleni ni tatizo la mipango miji ambalo kama utalitazama vizuri basi utaweza kubaini kuwepo kwa mgawanyo mbovu uliopo katika mgawanyo wa huduma za kijamii zilizopo jijini Dsm.Dsm kama ilivyo ina manispaa tatu(3)yaani Ilala,Temeke & Kinondoni na katika Manispaa hizi kiukubwa kwa eneo ni Temeke ikifuatiwa na Kinondoni na mwisho ni Ilala ndio ndogo kieneo kuliko zote.Cha ajabu huduma zote za kibiashara,maofisi ya Serikali,Hospitali kubwa,Soko kubwa la Kariakoo,Wizara nyingi kama si zote,ikulu,Airport, maduka yote makubwa,mahoteli yote makubwa,mahukumbi makubwa yote na nyinginezo nyingi zipo katika Manispaa ya ilala.Kuwepo kwa huduma hizi tu katika eneo moja tena dogo kieneo ukilinganisha na manispaa nyingine hilo ni tatizo kubwa.Nini kifanyike,kwanza ni kuhamisha huduma zote muhimu kubwa katika manispaa ya ilala na kwenda katika manispaa nyingine za kinondoni na temeke,huduma kama vile kuwepo kwa shopping malls kubwa zenye kuchukua maeneo makubwa mf.century city iliyopo cape town,kuwepo kwa masoko ya kariakoo mengine katika manispaa hizi mbili,baadhi ya ofisi za Serikali kubwa zinatakiwa kuhamishwa hapo mjini(uchambuzi ufanyike zipi zihamishwe na zipi zibaki) etc
Pia kuanzishwe huduma ya kutoza kodi kwa magari yanayoingia mjini,hii itapunguza baadhi ya magari kuingia mjini na bila kusahau watu wahimizwe kutumia public transport kama dbrt itakapoanza.huo ni mtizamo wangu
Pia kuanzishwe huduma ya kutoza kodi kwa magari yanayoingia mjini,hii itapunguza baadhi ya magari kuingia mjini na bila kusahau watu wahimizwe kutumia public transport kama dbrt itakapoanza.huo ni mtizamo wangu