Dawa ya kuondoa msongamano Dar...

The Boss

JF-Expert Member
Aug 18, 2009
49,140
116,064
- Eneo la Kariakoo liwe na bidhaa moja tu ya biashara, mfano bidhaa za nguo.

- Maduka ya simu na vifaa vya simu yahamishwe, mfano Pugu.

- Maduka ya vifaa vya ujenzi yote yahamie mfano Tegeta.

- Vipodozi yote yaende mwenge.

- Vifaa vya kilimo Tandika. Posta yoote kusiwe na maduka zaidi ya maofisi na maduka ya nguo tu.
maduka ya furniture yote yaende Keko..

Tukiweza hili misongamano na foleni zitakwisha Dar. Tuige nchi zingine basi, ingawa Madiwani na mameya wote waliopo ni mizigo.
 
Eneo la Kariakoo liwe na bidhaa moja tu ya biashara mfano bidhaa za nguo maduka ya simu na vifaa vya simu yahamishwe mfano Pugu maduka ya vifaa vya ujenzi yote yahamie mfano Tegeta Vipodozi yote yaende mwenge...... vifaa vya kilimo Tandika..... posta yoote kusiwe na maduka zaidi ya maofisi na maduka ya nguo tu... maduka ya furniture yote yaende Keko.. tukiweza hili misongamano na foleni zitakwisha Dar tuige nchi zingine basi..... ingawa Madiwani na mameya wote waliopo ni mizigo...
mkuu ni mawazo mazuri,lakini kama la kuhamisha makao makuu Dodoma linasuasua itachukua muda.
 
Aisee, kipi kimekufanya ufikirie hili?

Jana sababu ya hofu ya maandamano ya Sheikh Ponda
watu walifunga mapema maduka,
posta na Kariakoo
matokeo yake foleni ikawa nafuu mno
na wengine hawakukumbana na msongamano kabisa

so maduka ya kariakoo na posta ndo chanzo cha vurugu yote ya mifoleni
yakipunguzwa tu,mji utakuwa tofauti mno
 
The Boss, dawa ya kuondoa foleni ni KUYAONDOA MAGARI barabarani. Hili ni suala la MIUNDOMBINU. Nilikwishamuelimisha Mwakyembe kuhusu solution. Hebu Google "Kuala Lumpur Monorail" kisha nenda kwenye "images" uone jinsi wenzetu walivyofanikiwa. Kwao foleni wanaisikia kwenye vyombo vya habari tu!
 
Last edited by a moderator:

Hofu ya vurugu ILIYAONDOA MAGARI barabarani. Umeona hapo? Kumbe hujui kusoma kati kati ya mistari?
 
Hii ninayo suggest mimi inatumika miji mingi mno
Kuanzia China hadi Dubai..
kupanga maduka na maeneo kwa aina ya bidhaa...

right now Kariakoo ndo Centre ya mauzo ya jumla na rejareja
ya nchi nzima na nchi jirani kwa bidhaa hizi
1.nguo
2.simu na vifaa vyake
3.spare za magari
4.vifaa vya ujenzi
5.computers na vifaa vya ofisi
6.vyakula
7.vifaa vya kilimo..
8,furniture..
9.mengineyo

inatakiwa kufanyika plan mpya ya kuondoa maduka
ya bidhaa zote kasoro moja
na kuyasambaza kwenye kona zingine za jiji
 
Hofu ya vurugu ILIYAONDOA MAGARI barabarani. Umeona hapo? Kumbe hujui kusoma kati kati ya mistari?

Waajiriwa walibaki na magari yao
walioondoka walikuwa wafanya biashara
which proves my point,biashara zipunguzwe Posta na Kariakoo
 
The Boss, dawa ya kuondoa foleni ni KUYAONDOA MAGARI barabarani. Hili ni suala la MIUNDOMBINU. Nilikwishamuelimisha Mwakyembe kuhusu solution. Hebu Google "Kuala Lumpur Monorail" kisha nenda kwenye "images" uone jinsi wenzetu walivyofanikiwa. Kwao foleni wanaisikia kwenye vyombo vya habari tu!

Monorail ni gharama kubwa sana
hii nayoshauri mimi haifiki bilioni 50
ni kujenga maduka meengi mno na kuwaambia watu wahamie
mfani mnajenda maduka 2000 pugu na kuwaambia wenye maduka ya simu Kariakoo
wote wahamie huko
halafu unajenga maduka 2000 bunju na kuwahamishia wenye maduka ya spare za magari
 
Kwa maoni yangu mimi ni train ziwe kila upande wa dar es salaam..

Na then serikali iongeze bei ya ku park gari mjini mfano sh 5000 kwa saa na iwe strict kweli kweli uone watu wangapi wataenda na magari binafsi mjini....
 
Nakubaliana nawe boss tatizo kubwa la nchi yetu ni kuhakikisha sheria zinafuatwa. Mamlaka zote husika zimeshindwa kabisa kusimamia sheria mbali mbali ndio maana mingi ya majiji/miji yetu imekithiri kwa uchafu ndio maana maadili nchini yanazidi kuporomoka kila kukicha. Sheria za kuhakikisha usafi wa miji/majiji zipo wazi lakini mamlaka husika zimeshindwa kabisa kusimamia sharia hizo. Hili ni wazo zuri sana lakini litawagusa pia baadhi wa wanene wengi ndani ya chama na Serikali hivyo watalipotezea tu ili kuhakikisha biashara zao zinaendelea kuwepo katika maeneo uliyoyataja.
 
Last edited by a moderator:
Kwa maoni yangu mimi ni train ziwe kila upande wa dar es salaam..

Na then serikali iongeze bei ya ku park gari mjini mfano sh 5000 kwa saa na iwe strict kweli kweli uone watu wangapi wataenda na magari binafsi mjini....

Treni ukitaka zifike Mbezi beach hadi Bunju
utalazimika kufanya bomoaboma na kuwalipa watu fidia
na mahakama itahusika na zoezi litachukua miaka
hii nayo suggest ni rahisi mno
ni kujenga maduka ya bidhaa moja eneo moja
kama wauza vinyago walivyohamishiwa Mwenge zamani
sasa tunaweza ondoa wauza spare za magari Kariakoo na kuwahamishia PUGU
halafu wauza simu na vifaa vyake wakahamishiwa kunduchi...
 
... Kaka, nasupport wazo lako. Nyongeza ya mbinu nyingine katika kupunguza msongamano ni kuwepo kwa shift pattern kwa wafanyakazi kwenye ofisi nyingi za serikali zilizopo central district na hata kwenye kampuni binafsi. Mfano, pawepo watu wanaofanya kazi kuanzia saa 2 asubuhi, wengine saa 4 na wengine saa 6 mchana.
Nina imani kwamba mpangilio kama huo ukiwepo karaha ya foleni za kuelekea mjini asubuhi au kutokea mjini nyakati za jioni itapungua.
 
... Kaka, nasupport wazo lako. Nyongeza ya mbinu nyingine katika kupunguza msongamano ni kuwepo kwa shift pattern kwa wafanyakazi kwenye ofisi nyingi za serikali zilizopo district centre na hata kwenye kampuni binafsi. Mfano, pawepo watu wanaofanya kazi kuanzia saa 2 asubuhi, wengine saa 4 na wengine saa 6 mchana.
Nina imani kwamba mpangilio kama huo ukiwepo karaha ya foleni za kuelekea mjini asubuhi au kutokea mjini nyakati za jioni itapungua.

Mimi ningeweza ningesema wale ambao hawajaajiriwa
mfano wamama wa ferry watoke saa tatu
wakati wenzao wa serikalini wakiwa tayari wao maofisini
na vyuo pia vianze saa tatu
so wa asubuhi wanakuwa ni wafanyakazi zaidi..
kuliko now,unakuta mtu wa benk na mama ntilie wa ferry wote wako saa kumi na mbili barabarani
full vurugu..
 
Kupunguza foleni Mandela hadi Mbezi malori yatoke bandarini kuanzia saa nne usiku

hili pia ni maamuzi tu
au wanaweza kuhakikisha hakuna lori linaingia mjini
mizigo yote itolewe bandarini kwa treni mpaka nje ya mji...hivi
mfano Pugu ndo malori yaanzie hapo
 
Mimi ningeweza ningesema wale ambao hawajaajiriwa
mfano wamama wa ferry watoke saa tatu
wakati wenzao wa serikalini wakiwa tayari wao maofisini
na vyuo pia vianze saa tatu
so wa asubuhi wanakuwa ni wafanyakazi zaidi..
kuliko now,unakuta mtu wa benk na mama ntilie wa ferry wote wako saa kumi na mbili barabarani
full vurugu..

... Soko la samaki Ferry lihamishiwe Msasani bhana. Serikali inunue kiwanja kimojawapo huko ufukweni hata kwa billioni 5 hivi na kujenga soko jingine huku waki phase out shughuli za pale Ferry. Pale pabakie kivuko tu. Walipoamua kuimarisha lile soko kwa mamilioni walifanya makosa kwa maoni yangu, walitakiwa walifunge. Na ile incident ya moto nayo ingelitumika kama sababu ya kulifunga jumlajumla na kuondoa shombo la samaki eneo sensitive kama pale.
 
sio Msasani mi naona Kawe au Kunduchi kabisa
au lihamie Kigamboni jirani na daraja jipya
ni aibu mno kuweka shombo loote lile Ikulu pale
na daladala zinapita huku watu wamebanana hadi mlangoni..
asante kwa kunikumbusha hili...
 
Back
Top Bottom