View attachment 107671View attachment 107672
Source: Dar Master Plan-2012-2032-kwa msaada wa post ya EMT ndani ya uzi huu.
The Boss, wazo lako ulilolitoa kwenye post 1 ya uzi huu...linaweza kutekelezeka kwa ufanisi endapo...mfumo wa barabara ulioonyeshwa kwenye ramani hapo juu utakuwa umejengwa vizuri na kukamilika.
Kwa mazingira ya Sasa ...wazo lako hilo litakuwa gumu kutekelezeka.
Mengi yameishaelezwa na wanajamvi...ila kwa nyongeza....ni kudhibiti misafara ya viongozi ambao ulazimisha kufungwa baadhi ya barabara ili waheshimiwa hao wapite.
Udhibiti huo unaweza kuwa wakutoa taarifa mapema mahali gani viongozi hao watapita...ili kama kuna mtu ana gari lake asipite maeneo hayo au abadili ratiba kabisa....na kama ki-usalama haiwezekekani kutoa taarifa mapema basi...viongozi hao...watumie usafiri wa Helkopta (wengine mnaita Chopa), au hata boti ndogo mahala panapowezekana...mfano kutumia boti kutoka feli kwenda Bagamoyo.
Nina imani wanahesabu wakilinganisha gharama za matumizi ya helkopta kwa viongozi wafunga barabara na gharama wanayosababisha kwa kuzuia watu barabari kwa zaidi ya masaa mawili....sina shaka..helkopta itakuwa nafuu sana.
Hoja yangu hapa imelenga kwenye msogamano wa magari barabarani.