Dawa ya kuondoa msongamano Dar...

Kupunguza foleni Mandela hadi Mbezi malori yatoke bandarini kuanzia saa nne usiku

... Ahsante kwa wazo mkuu. Hii kitu haihitaji hela yoyote, ni maamuzi tu. I wish I could tag Mwakyembe in here. Kwa kweli msongamano mkubwa sana unasababishwa na malori barabara ile. Na kibaya zaidi huwezi ukatoka Buguruni mpaka Ubungo Mataa bila kukutana na lori lililo chomekwa-chomekwa matawi ya miti baada ya kuharibika kwa ku-jackknife, kuchomoka tairi, tanki la mafuta kulegea au container kudondoka!!
 
sio Msasani mi naona Kawe au Kunduchi kabisa
au lihamie Kigamboni jirani na daraja jipya
ni aibu mno kuweka shombo loote lile Ikulu pale
na daladala zinapita huku watu wamebanana hadi mlangoni..
asante kwa kunikumbusha hili...

... Inabidi serikali ifanya maamuzi magumu ya kupafunga pale, kama siyo sasa, basi siku ya ufunguzi wa DART. Jiji lilikuwa safi wakati wa ujio wa Obama, sioni tunashindwa vipi kuendeleza hali hiyo kwa kufanya maamuzi magumu (yanayoweza kuumiza wachache kwa muda mfupi bali kuwa na manufaa kwa jiji in the long-term).
 
Eneo la Kariakoo liwe na bidhaa moja tu ya biashara
mfano bidhaa za nguo

maduka ya simu na vifaa vya simu yahamishwe
mfano Pugu

maduka ya vifaa vya ujenzi yote yahamie mfano Tegeta

Vipodozi yote yaende mwenge......

vifaa vya kilimo Tandika.....
posta yoote kusiwe na maduka zaidi ya maofisi
na maduka ya nguo tu...
maduka ya furniture yote yaende Keko..

tukiweza hili misongamano na foleni zitakwisha Dar
tuige nchi zingine basi.....
ingawa Madiwani na mameya wote waliopo ni mizigo...

The Boss, Tandika ndio umetuona majirani na Pinda siyo? Ndio umtuona wakulima? Hahaa, ngoja waje wenyewe wabadilishe na kuweka maduka ya filamu za kibongo na bongo flavor.

Kimsingi, umefikiria jambo jepesi na rahisi sana kutekelezwa. Dar es Salaam ilipofikia hili linaweza kuwa jambo litakalosaidia kwa haraka kuondoa au kupunguza foleni na linatumiwa na nchi nyingi sana duniani. Litakuwa gumu kwasababu viongozi wetu "wamewekeza" kwenye maduka Kariakoo na Posta hivyo watapata hasara, ila liweke wazo lako atapatikana atakaekuja kulikumbuka.

Faida nyingine ya mpango wa namna hii ni kuwa na 'diversified city' ambapo muda si mrefu maeneo kama Pugu, Mbagala Tegeta (yaani ya pembezoni) yatakuwa na majengo yenye sura za JIJI siyo KIJIJI.

Kiukweli foleni ya Dar haisababishwi na wafanyakazi bali wafanyabiashara. Kuthibitisha hili, utashangaa ifikapo kati ya saa 4 hadi saa 8, bado kunakuwa na foleni hali ya kuwa magari mengi ya wafanyakazi yanakuwa yamepaki. Wazo zuri sana hili ila kwa nchi siyo.

... Soko la samaki Ferry lihamishiwe Msasani bhana. Serikali inunue kiwanja kimojawapo huko ufukweni hata kwa billioni 5 hivi na kujenga soko jingine huku waki phase out shughuli za pale Ferry. Pale pabakie kivuko tu. Walipoamua kuimarisha lile soko kwa mamilioni walifanya makosa kwa maoni yangu, walitakiwa walifunge. Na ile incident ya moto nayo ingelitumika kama sababu ya kulifunga jumlajumla na kuondoa shombo la samaki eneo sensitive kama pale.

Mimi nasema serikali iachane na hayo mambo ya kununua masoko ya bidhaa. Yenyewe ijikite kwenye dhima ya kusimamia sheria na taratibu na kupanga na kuchagua tu maeneo ya shughuli tofauti tofauti za kiuchumi na biashara.

Mambo ye kujenga hayo masoko iachiwe sekta binafsi.
 
... Inabidi serikali ifanya maamuzi ya magumu ya kupafunga pale, kama siyo sasa, basi siku ya ufunguzi wa DART. Jiji lilikuwa safi wakati wa ujio wa Obama, sioni tunashindwa vipi kuendeleza hali hiyo kwa kufanya maamuzi magumu (yanayoweza kuumiza wachache kwa muda bali kuwa na manufaa kwa jiji in long-term).

Ukichunguza sana utakuta hii tunayoshauri hapa
haizidi bilioni 50
wakati DART ni zaidi ya billioni 200
na still haitaondoa foleni

halafu kuna kuidhibiti NHC pia
wanaongeza msongamano kwa kuwauzia wahindi
majengo yao
jengo la ghorofa mbili linageuka la ghorofa kumi
Kariakoo NHC wanawapa wahindi wanajenga maduka zaidi kwenye jengo ambalo
zamani lilichukua maduka kidogo,
 
hili pia ni maamuzi tu
au wanaweza kuhakikisha hakuna lori linaingia mjini
mizigo yote itolewe bandarini kwa treni mpaka nje ya mji...hivi
mfano Pugu ndo malori yaanzie hapo

Hiyo itakuwa gharama za loading-unloading-loading. Kwa malori nadhani yaanze kutoka saa 4 usiku mwisho saa 11 alfajir yawe yameshapita Kibaha huko.
 
Mimi nasema serikali iachane na hayo mambo ya kununua masoko ya bidhaa. Yenyewe ijikite kwenye dhima ya kusimamia sheria na taratibu na kupanga na kuchagua tu maeneo ya shughuli tofauti tofauti za kiuchumi na biashara.

Mambo ye kujenga hayo masoko iachiwe sekta binafsi.

Na wakishirikisha sekta binafsi itakuwa better
ni kuamua tu kuwa maduka ya bidhaa fulani yatahamia eneo fulani
na sekta binafsi itaitwa ijenge hayo maduka eneo hilo
so hata bilioni 50 nilizo plan hazihitajiki
ni maamuzi tu na msongamano unaondoka fasta
 
The Boss, Tandika ndio umetuona majirani na Pinda siyo? Ndio umtuona wakulima? Hahaa, ngoja waje wenyewe wabadilishe na kuweka maduka ya filamu za kibongo na bongo flavor.

Kimsingi, umefikiria jambo jepesi na rahisi sana kutekelezwa. Dar es Salaam ilipofikia hili linaweza kuwa jambo litakalosaidia kwa haraka kuondoa au kupunguza foleni na linatumiwa na nchi nyingi sana duniani. Litakuwa gumu kwasababu viongozi wetu "wamewekeza" kwenye maduka Kariakoo na Posta hivyo watapata hasara, ila liweke wazo lako atapatikana atakaekuja kulikumbuka.

Faida nyingine ya mpango wa namna hii ni kuwa na 'diversified city' ambapo muda si mrefu maeneo kama Pugu, Mbagala Tegeta (yaani ya pembezoni) yatakuwa na majengo yenye sura za JIJI siyo KIJIJI.

Kiukweli foleni ya Dar haisababishwi na wafanyakazi bali wafanyabiashara. Kuthibitisha hili, utashangaa ifikapo kati ya saa 4 hadi saa 8, bado kunakuwa na foleni hali ya kuwa magari mengi ya wafanyakazi yanakuwa yamepaki. Wazo zuri sana hili ila kwa nchi siyo.

Mkuu Tandika now ni kama Kariakoo ya pili
na yenyewe itahitajika kufanyiwa plan upya ya haraka
maana kwa maduka ya nguo tu peke yake
inashindana na kariakoo..
 
Mkuu Tandika now ni kama Kariakoo ya pili
na yenyewe itahitajika kufanyiwa plan upya ya haraka
maana kwa maduka ya nguo tu peke yake
inashindana na kariakoo..
Ni kweli mkuu, tena tuna tatizo la msingi ambao litatugharimu muda si mrefu; ujenzi wa vijfrem vidogovidogo vya biashara badala ya kujenga malls zitakazokuwa na partition. Serikali ilitakiwa itoe mwongozo haraka katika hili, ujenzi ufanywe kwa ubia baina ya wafanyabiashara ili kuepuka kujenga stail za zamani za vijifremu. Dunia inakuwa kwa kasi sana, ukijenga jengo leo after 10 years hautalitamani.
 
Na wakishirikisha sekta binafsi itakuwa better
ni kuamua tu kuwa maduka ya bidhaa fulani yatahamia eneo fulani
na sekta binafsi itaitwa ijenge hayo maduka eneo hilo
so hata bilioni 50 nilizo plan hazihitajiki
ni maamuzi tu na msongamano unaondoka fasta

Mambo ya planning and zoning sisi zero kabisa.

Jiji kama la Dar linatakiwa liwe na restrictive zoning laws kali sana. Na juu ya hapo hizo laws ziwe zinatekelezwa to the letter.

Ona mabaa na magesti yalivyozagaa. Yaani vurugu tupu!

Mara nyingi nikiongea na watu huwa nawaambia msongamano wa magari Dar ni matokeo ya kukosa mipango mizuri tu. Dar sidhani kama ina magari mengi kihivyo.

Mji hauko spread out, vimiundo misingi vyake na vyenyewe ni viko hohehahe tu. Sasa ukiongezea na uendeshaji wa magari wa madereva ndio unapata hilo baa la msongamano.
 
Ni kweli mkuu, tena tuna tatizo la msingi ambao litatugharimu muda si mrefu; ujenzi wa vijfrem vidogovidogo vya biashara badala ya kujenga malls zitakazokuwa na partition. Serikali ilitakiwa itoe mwongozo haraka katika hili, ujenzi ufanywe kwa ubia baina ya wafanyabiashara ili kuepuka kujenga stail za zamani za vijifremu. Dunia inakuwa kwa kasi sana, ukijenga jengo leo after 10 years hautalitamani.

Sasa hiki unachozungumza ndo natamani
mkurugenzi wa NHC angekielewa
yeye anawapa wahindi majengo Kariakoo wanajenga tena 'bazaar shops'
badala ya kushusha malls za kufa mtu
 
Mambo ya planning and zoning sisi zero kabisa.

Jiji kama la Dar linatakiwa liwe na restrictive zoning laws kali sana. Na juu ya hapo hizo laws ziwe zinatekelezwa to the letter.

Ona mabaa na magesti yalivyozagaa. Yaani vurugu tupu!

Mara nyingi nikiongea na watu huwa nawaambia msongamano wa magari Dar ni matokeo ya kukosa mipango mizuri tu. Dar sidhani kama ina magari mengi kihivyo.

Mji hauko spread out, vimiundo mbinu vyake na vyenyewe ni viko hohehahe tu. Sasa ukiongezea na uendeshaji wa magari wa madereva ndio unapata hilo baa la msongamano.

Exactly
kukiwa na plan nzuri hakuna msongamano wala foleni
magari sio mengi kabisa...
 
Mkuu huhitaji hayo mambo yote hapo juu. Unachotakiwa kufanya ni kuwapa kazi wenye ujuzi wa hiyo fani watatue tatizo hilo na mambo ya siasa waachiwe CCM na CHADEMA etc. Siasa inapoingilia fani za wasomi ndio tatizo. Dar haina hata watu millioni 10 ni kamji kadogo sana ambako hakuna planning, ati majembe auctions ndio wanapewa kazi ya Highways. Pathetic!
 
Mimi ningeweza ningesema wale ambao hawajaajiriwa
mfano wamama wa ferry watoke saa tatu
wakati wenzao wa serikalini wakiwa tayari wao maofisini
na vyuo pia vianze saa tatu
so wa asubuhi wanakuwa ni wafanyakazi zaidi.
.
kuliko now,unakuta mtu wa benk na mama ntilie wa ferry wote wako saa kumi na mbili barabarani
full vurugu..
A good policy should not be in a way that some people become better-off by making others worse-off: Hii sikubaliani nayo kuathiri muda wa mtu katika kujiletea maendeleo yake. Nionavyo mimi, ikitokea hii ya business relocation, haya mengine natumai yatajiseti yenyewe.
 
Exactly
kukiwa na plan nzuri hakuna msongamano wala foleni
magari sio mengi kabisa...

Hivi bongo sisi tuna emissions control laws?

Maana kuna magari mengi sana bongo ambayo kama labda tungekuwa na emissions control laws wala yasingekuwa hata barabarani.

Kwa nchi za wenzetu kuna sehemu gari haiwezi hata kupata usajili bila ya ku-pass emissions test. Na usajili unatakiwa kila mwaka. Hivyo kila mwaka kabla usajili wa mwaka uliopita haujaisha muda wake ni lazima ifanyiwe testing tena na lazima i-pass ili iweze kupata huo usajili. Ikifeli haipati.

Na kama gari haina usajili basi ni kinyume na sheria kuiweka barabarani. Ukiiweka na ukikamatwa hiyo faini yake utajuta.

Utaratibu huo nao hupunguza uwepo wa yale magari mabovu mabovu yanayoongeza idadi ya magari mabarabarani na kuchafua mazingira.

Lakini by the looks of it, idadi ya mikweche iliyopo kwenye mabarabara ya bongo inanifanya nidhani hatuna kabisa sheria za namna hiyo.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Nadhani mwaka juzi Bongo walitaka kupiga marufuku magari yote yenye umri wa zaidi ya miaka mitano, hili lingesaidia sana katika kupunguza emissions level na kupunguza utitiri wa magari, lakini kama kawaida ya mamlaka zetu husika wakalipotezea hili kwa kuona wengi wangeathirika na sharia kama hii ikiwemo wao wenyewe wanene ndani ya chama na serikali. Hili la msongamano wa magari kwa kweli ni tatizo kubwa sana. Umbali ambao miaka michache iliyopita ulikuwa unahitaji 15 to 20 minutes sasa hivi unaweza kuchukua 2 or even more hours na kukitokea ajali au mheshimiwa anapita basi ndio hali huzidi kuwa mbaya sana. Watu, baadhi, wanaondoka majumbani saa 10 za usiku ili kuwahi kazini. Wengi breakfast kwenye gari na wakirudi majumbani ni kuanzia tatu za usiku na kuendelea. Hali hii ya maisha inakera sana na bado hii "Serikali sikivu" haijaweka mikakati yoyote ile madhubuti ili kuhakikisha msongamano wa magari Dar unapunguzwa kwa kiwango kikubwa. Nchi inaingia mabilioni ya hasara kila siku inayosababishwa na msongamano huo.

Hivi bongo sisi tuna emissions control laws?

Maana kuna magari mengi sana bongo ambayo kama labda tungekuwa na emissions control laws wala yasingekuwa hata barabarani.

Kwa nchi za wenzetu kuna sehemu gari haiwezi hata kupata usajili bila ya ku-pass emissions test. Na usajili unatakiwa kila mwaka. Hivyo kila mwaka kabla usajili wa mwaka uliopita haujaisha muda wake ni lazima ifanyiwe testing tena na lazima i-pass ili iweze kupata huo usajili. Ikifeli haipati.

Na kama gari haina usajili basi ni kinyume na sheria kuiweka barabarani. Ukiiweka na ukikamatwa hiyo faini yake utajuta.

Utaratibu huo nao hupunguza uwepo wa yale magari mabovu mabovu yanayoongeza idadi ya magari mabarabarani na kuchafua mazingira.

Lakini by the looks of it, idadi ya mikweche iliyopo kwenye mabarabara ya bongo inanifanya nidhani hatuna kabisa sheria za namna hiyo.
 
Kuongezeka kwa msongamano mijini kunahatarisha uchumi na maisha ya baadae ya mji husika. Kukukua kwa mji kunaongeza demand, lakini ukuaji huo unaweza kuwa hasara kwa mji kutokana na kuongezeka kwa msongamano.

Dar Es Salaam kuna msongamano wa magari na watu. Njia mojawapo ya kupunguza msongamano wa magari ni kuimarisha public transport. Hata hivyo, kutokana na Dar Es Salaam kuwa na public transport mbaya ni watu wachache sana wenye magari yao binafsi ambao watakubali kuyaacha nyumbani na kupanda daladala. Afterall, bado kuna baadhi ya watu ambao wangependa ku-show off what sort of a car they drive.

Kwa sasa hivi sioni concrete action yoyote inayotia matumaini makubwa katika kutatua tatizo sugu la msongamano jijini Dar Es Salaam. Badala yake, tatizo la msongamano linaendelea kuwa kubwa hasa baada ya kuingia kwa boda boda.

Lakini wakazi wa jiji nao wameshaliona tatizo la msongamano wa magari kama sehemu ya maisha yao. Mabadiliko ya jiji la Dar Es Salaam yataletwa na Wanadarisalama wenyewe kwa kukataa kufanya tatizo la msongamano kama sehemu ya maisha yao ya kila siku.

Mji wa Moshi siyo msafi kivile tuu. Wala barabara zake za mjini hazipigwi deki pindi tuu kunapokuwa na mgeni. Wao wameamua mji wao uwe msafi whether or not kuna mgeni. Afterall, usafi ni kwa manufaa ya wakazi husika. Wala haina maana kuwa wachaga ni wasafi sana maana wametapakaa pia kila kona ya Dar Es Salaam.

Hata hivyo, kuhusiana na suala zima la msongamano Dar, labda judadili kwa kuanzia na Dar Es Salaam Masterplan 2012 – 2032. Does it address the points you have raised? Will the new city planned be achieved by 2013?

Dar es Salaam Masterplan 2012 – 2032: Ministry of Lands, Housing and Human Settlements Development: http://www.planning4adaptation.eu/Docs/newsInfoMaterial/05-2013/08/FONTANARI_22_APRIL_2013.pdf
 
Nadhani mwaka juzi Bongo walitaka kupiga marufuku magari yote yenye umri wa zaidi ya miaka mitano, hili lingesaidia sana katika kupunguza emissions level na kupunguza utitiri wa magari, lakini kama kawaida ya mamlaka zetu husika wakalipotezea hili kwa kuona wengi wangeathirika na sharia kama hii ikiwemo wao wenyewe wanene ndani ya chama na serikali. Hili la msongamano wa magari kwa kweli ni tatizo kubwa sana. Umbali ambao miaka michache iliyopita ulikuwa unahitaji 15 to 20 minutes sasa hivi unaweza kuchukua 2 or even more hours na kukitokea ajali au mheshimiwa anapita basi ndio hali huzidi kuwa mbaya sana. Watu, baadhi, wanaondoka majumbani saa 10 za usiku ili kuwahi kazini. Wengi breakfast kwenye gari na wakirudi amjumbani ni kuanzia tatu za usiku na kuendelea. Hali hii ya maisha inakera sana na bado hii "Serikali sikivu" haijaweka mikakati yoyote ile madhubuti ili kuhakikisha msongamano wa magari Dar unapunguzwa kwa kiwango kikubwa. Nchi inaingia mabilioni ya hasara kila siku inayosababishwa na msongamano huo.
BAK, wazo la kuondoa magari kwasababu ya umri wake tu hata mimi sitoafikiana nalo. Siafikiani na wazo hilo maana roadworthy haitegemei umri wa gari; ni matunzo ya gari zaidi ndiyo huwa kigezo. Unaweza kuwa na gari la miaka minne lakini likawa linatoa moshi kuliko tairi la kuchoma kwenye maandamano! Lakini pia unawezakuwa na gari la miaka 12 ambalo limetunzwa na carbon emission yake ikawa chini sana. Hii inapelekea kukukumbushia moja ya jambo kwa wenzetu jinsi vile baadhi ya magari yaliyo 'antique' yanavyokuwa aghali kuliko mengi mapya.
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: BAK
Huduma zote za jamii zimewekwa sehemu moja POSTA !!! Banks,shule,ofisi,wizara,Ikulu etc,mfano mdogo tu bwana The BOSS pale POSTA bank ya NMB Ina matawi zaidi ya matatu wakati hawana tawi ata moja sehemu yenye watu wengi Kama KIgamboni,Leo hii mkazi wa Kigamboni/Mbagara ili aweze kupata service ndogo tu ya kuweka pesa bank au kuchange $10 lazima aende POSTA!!!uwekwe mda maalumu wa magari mkubwa ya mizigo kupita mjini.Makao makuu yapelekwe Dodoma ukifanya hivyo mji utapumua na utapangika,Nigeria walifanya hivyo Lagos ulibaki mji wa kibiashara shughuri za kiserikali zikapelekwa Abuja,UAE walipeleka shughuri zote za kiserikali Abu dhabi maana mabalozi wengi walipendelea kuishi Dubai.Dar es salaam haina magari mengi ila mipangilio na infrastructure zipo chini sana
 
Back
Top Bottom