Dawa na watengenezaji dawa za kupunguza uzito mitandaoni wana viwango?

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,557
21,511
Husika na kichwa cha habari,

Uzito wa kupitiliza umekuwa ni janga kwa watu walio wengi kuanzia vijana hadi wazee.

Hii yote ni kulingana na ulaji mbovu wa vyakula kama chips na wanga uliopitiliza.

Kingine ni uvivu wa kufanya mazoezi kwa watu walio wengi.

Ajabu ni kuwa pamoja na kuwa wavivu wa mazoezi wamekuwa wanakula hovyo.

Janga hili la uzito limekuwa ni kero hasa kwa wanawake walio wengi.

Hii imepelekea kutafuta njia za mkato za kupunguza uzito kwa watu mitandaoni.

Kumekuwa na wimbi la watengenezaji wa dawa za kupunguza uzito mitandaoni.

Nikawa na maswali sana je hawa watengenezaji wa dawa hizi wana viwango?

Pia dawa zenyewe zinazotengenezwa na watengenezaji hao zina viwango?

Nikawazua zaidi maana wimbi hili limekuwa kubwa na ni kwa muda sasa.

Mamlaka husika zinafanya kazi kufuatilia hawa watengenezaji au zimeacha tuangamie?

Dawa hizi zimekuwa zilitumia muda mchache sana kupunguza uzito.

Kuna wanaosema zinapunguza hadi 7 days na nyingine mwezi mmoja.

Nikawaza sana madhara ya dawa hizi yanaweza yakawa ni makubwa maana zinafanya kazi kwa haraka.

Tofauti na dawa za kutengenezwa pia kumekuwa na madawa mbalimbali kutoka nchi tofauti ambazo nazo zinapunguza uzito.

Je, dawa hizi zinafanyiwa uangalizi na mamlaka husika au zinaingizwa kihorera?

Kuna ambao wamekuwa wakijitangaza kuwa dawa walizotumia ndizo zimewapunguza huku ni waongo wanapiga pesa.

Na madhara yake kwa wahanga hao wanaotumia hasa wanawake wanaojifungua wanaambiwa wanaweza kutumia huku wananyonyesha.

Wanawake wamekuwa watu wa kulipukia tu midawa hiyo hata bila kujua madhara.

Mamlaka hisika tuomba ombi lifanyiwe kazi.
 
Wengi wao ni matapeli ila baadhi yao ni matapeli

Wengine wanauza majani ya chai wakidai yanapunguza uzito, wengine wanauza virutubisho ilimradi tu waseme vinapunguza uzito matokeo yake unaendesha balaa, unakuwa na trip nyingi sana za toilet hadi sio poa

Nadhani mamlaka husika ziangalie kiundani hizi dawa, afya za watu wengi zinadorora
 
Wengi wao ni matapeli ila baadhi yao ni matapeli

Wengine wanauza majani ya chai wakidai yanapunguza uzito, wengine wanauza virutubisho ilimradi tu waseme vinapunguza uzito matokeo yake unaendesha balaa, unakuwa na trip nyingi sana za toilet hadi sio poa

Nadhani mamlaka husika ziangalie kiundani hizi dawa, afya za watu wengi zinadorora
Matapeli wakubwa...

Udanganyifu mtupu...
 
Back
Top Bottom