maneno ya kafulila jana jioni hapa dodoma
" huu mjadala watu kukana hauna maana kabisa. wote wanaokana ndio wapiga debe wakubwa. waliyasema haya wanayoyakana. ni unafiki ndio unaowasumbua na uoga. kabla ya kuondoka, wote tulikaa pale sinza na kwa pamoja wakasema wanamuunga mkono, tukafika Kigoma wakarudia maeno yale yale ya kumuunga zitto. Iweje leo wanakana? Asilimia 85% ya wabunge wanamuunga mkono zitto kugombea urais. Wana kigoma tumeonewa sana. Muda umefika kuwepo usawa katika uongozi wa hii nchi. Hatuwezi kuwa wasindikizaji siku zote, wakati uwezo tunao. Tunaungwa mkono kila kona ya nchi na hata nje ya nchi, na kama ni demokrasia 2015 rais na makamu wake lazima watokee Kigoma. Rais wa Tanzania, Afrika Kusini, ujerumani na Malaysia wote wanataka umuona rais kijana Tanzania.Vyama vyote vya siasa humu nchini wanamtaka rais kijana, Kikwete mwenyewe anamtaka atakayemrithi awe kijana"
----------------------------------
Edward Lowassa For President 2015
Hii inasababisha niandike yafuatayo:
1. Kama Mdee na Nassari walisema hayo yanayodaiwa na Zitto na baadaye kuyakanusha basi wataumbuka, ila Zitto ajue kuwa kuanzia sasa wamemjua yuko vp, watakuwa adui zake kimtindo. Hawatamuunga mkono tena kwenye mambo yake, hata ya kijamii. Hata akina Ester na Deo watashtukia mialiko mingine ya 'Mwasiti'.
Na hata leo wakiibuka Mdee, Nassari, Ester B, Deo Filiku na kupaza sauti kuhusu urais, so what? WaTz watachagua wenyewe, si kuchaguliwa na wabunge hao au wengine wowote.
2. Hiyo 85% ya wabunge kumuunga mkono Zitto kugombea urais haiwezi kuaminika. Kwa uzoefu tu wale wa CCM watamuunga mkono wa kwao, hao tayari ni zaidi ya nusu ya wabunge. Sasa hiyo 85% imetokea wapi? Mapishi...
Na wabunge hao si ndio waliopitisha Sheria kandamizi ya kukataa kutoa michango ya wafanyakazi kwenye mashirika ya hifadhi (PPF, GEPF, NSSF, LAPF etc) hadi eti wafikie umri wa kustaafu hata ukiacha au kufukuzwa ukiwa na miaka 25, 30 etc? Tatizo la mashirika haya ni kutoa pesa za michango ya wafanyakazi kwa serikali kugharamia miradi yake ya kisiasa. Hawafai.
3. Tanzania imetoa marais kutoka mikoa minne tu (Mara, Mjini Magharibi, Mtwara & Pwani) kati ya mikoa 30 iliyopo, hivyo mikoa 26 haijatoa Rais. Kwangu hii sio issue sana, ila what's so special with Kigoma?? Kwanini wao ndio eti lazima watoe Rais 2015? Tena eti pamoja na makamu wake?? Mbona Mbeya, Morogoro, Kusini Unguja, Kaskazini Pemba, Lindi, Kagera, Dodoma, Tanga, Kilimanjaro, Singida, Simiyu, Arusha na mingine jumla yake 26 haijatoa rais wa jamhuri? Kafulila aache mambo ya 'umkoa'.
4. 'Rais kijana' si lazima awe Zitto. Na 'ujana' si lazima iwe ni 'a plus' kwa mgombea urais. Kuna uwezo, uadilifu, uchapakazi, uchungu na nchi n.k. Rais anaweza kuwa wa umri wowote ili mradi asiwe chini ya miaka 40 (kwa mujibu wa katiba ya sasa). 'Vijana' akina Ngeleja, Masha, Maige, Mwinyi mbona wamechemka?
5. Issue ya marais wa Tanzania (sic! ina maana Kikwete!), Afrika Kusini, Ujerumani na Malaysia kusema kuwa wanamtaka rais kijana Tanzania haina maana kwani wapiga kura wa Tanzania hawatafuata matakwa ya hao watu wanne. Inatakiwa chaguo la Watanzania kupitia kwenye kura.
Kama aliyezungumza ni kafulila basi kachemka kwani Malaysia haina rais bali ina mfalme na waziri mkuu mtendaji (mwenye madaraka, si kama wa Tz). Hawa ndio walitaka kutuuzia 'mvua ya Lowassa'.
Mbona Afrika Kusini haohao wanachagua wazee? Mandela, Mbeki, Zuma na kuwatosa vijana wasio na subira/ wenye papara akina Malema?
NOTE:
Watanzania tukumbuke kuwa wakati huu ni wa mapambano ya kuikomboa nchi yetu kutokana na udhalimu na ufisadi unaoendelea kuitafuna nchi yetu. Mambo ni mengi yanayohitaji nguvu ya umma kuyabadilisha kama hili jipya la sheria kandamizi ya Mashirika ya hifadhi kung'ang'ania michango yetu hadi tufikie umri wa kustaafu.
Hivyo kama Serikali hii haitaki kusikiliza wananchi basi wana haki ya kubadilisha uongozi. Hatuhitaji malumbano hasa ndani ya Chama kinachoonekana kama kinaleta matumaini ya kushirikiana na wananchi kuikomboa nchi yao.
Watanzania hawatamsamehe yeyote yule ambaye anatumika au atatumika kuvuruga harakati za ukombozi hasa kwa kujaribu kivuruga chama ambacho kimeleta matumaini kwa watanzania.
Aluta Continua...