Wabunge vijana mnatuabisha vijana wenzenu! hivi na nyie mmeshaingiwa na uchu wa madaraka kiasi hicho??siamini! yaani badala ya kujenga hoja bungeni za kuondoa umaskini, kuboresha elimu, miundo mbinu,kilimo, afya, umeme n.k nanyi mmeoga tope lilelile la ccm ya kupambana kugombea urais 2015??Kafulila ni akili yako kweli? kwanza una chama chako cha NCCR kwa nini uanze kupigia chapuo mgombea urais toka CHADEMA? halafu unadai Kigoma nanyi mnataka urais sawa lakini Tanzania ina mikoa mingapi? kila mkoa ukianza kudai urais Tanzania itakuwa na marais wangapi?? Tanzania tunataka rais ayajuaye matatizo yetu kwa dhati, mwenye mbinu na maono ya kuyatatua, sasa atatoka nguruka, kazira mimba, ujiji, mwandiga, mwanga, kasulu, kibondo, manyovu, ukerewe, mafia , kiembe samaki , kilacha kimaroroni, kwa pole, tegeta kibaoni au wapi sio issue! Issue tunataka mtu wa kutuondoa hapa mahali CCM na serikali yake walipotunasisha! Acheni mambo ya kitoto na kijinga tumikieni wananchi muda ukifika chukueni fomu muombe ridhaa ya vyama vyenu na ya watanzania wapiga kura!