David Kafulila: Rais 2015 Lazima Atokee Kigoma

Status
Not open for further replies.
Ushauri wa bure kwa Mh Kafulila. Napendekeza uende kwa Mh Zitto ukamwambie kuwa kama anataka kugombea urais basi mapema kabisa atafute chama kingine na sio CDM. Huku CDM pameshajaa, hakubaliki na wala asijidanganye. Nasikia kuna CHAUMA kimeanzishwa, sasa akimbilie huko haraka bila kupoteza muda kwani anaonekana ana usongo sana. Kwa nini Kigoma ni lazima atoke Rais???? huu sasa ndio ukabila. Baba wa Taifa alisema kuwa hatumchagui mtu kutokana na ukabila wala dini yake.

MTU ANAYEKIMBILIA IKULU NI WA KUOGPWA KAMA UKOMA.
 
Sasa ni lazima CDM mcheze karata vizuri or else mtakuwa nikupiga kelele tu. vijana tunahitaji kulikomboa taifa hili. kama tunataka twende ikulu "we must not gamble".

Tumuweke kijana, msomi na mwenye vision nzuri na nchi hii. some one who is likable. Nafikiri kijana Zitto akipewa nafasi kurusha bendera yetu tutakwenda ikulu.

Sasa hivi tujaribu tu kumuuza kijana huyu tutafute wanachama vijana wote wa nchi hii ambao watatupigia kura na si kulumbana maana muda umekwenda. ni hayo tu.
 
kafulila amewahi kumhakikishia machali kwamba kulikuwa na pesa ya kutosha toka nje ya nchi kufanikisha mpango wa kumng'oa mbatia kwenye uenyekiti wa nccr ili kusafisha njia ya zitto kutimkia huko na jeshi kubwa la mamluki wake. Lazima ataharuki anapoona vijana wake wanamkana. Malengo ya hawa watu wa nje wanaotoa pesa yao ndiyo yanayotisha. Tuliyoyaona kwenye utawala wa kikwete yanatosha.

ndiyo maana zito analazimisha umri wa kugombea uraisi ushushwe kutoka miaka 42 hadi 40 ili 2015 atimize kigezo.what a shame!
 
Nasubiri wamalize tu na mimi nianze kumpigia debe Mwakyembe...maana naona kikwete ameufanya urais uwe urahisi
 
sasa ni lazima cdm mcheze karata vizuri or else mtakuwa nikupiga kelele tu. Vijana tunahitaji kulikomboa taifa hili. Kama tunataka twende ikulu "we must not gamble". Tumuweke kijana, msomi na mwenye vision nzuri na nchi hii. Some one who is likable. Nafikiri kijana zitto akipewa nafasi kurusha bendera yetu tutakwenda ikulu. Sasa hivi tujaribu tu kumuuza kijana huyu tutafute wanachama vijana wote wa nchi hii ambao watatupigia kura na si kulumbana maana muda umekwenda. Ni hayo tu.

mamlaka ya takwimu tanzania inatambua kuwa mtu aliye na umri mpaka miaka 55 bado ni kijana sasa unaongelea kijana wa umri gani?
 
Wote wanaoongelea urais mida hii ni punguani wa akili, tuongee mambo ya uchumi wa nchi hii; kuhusu rais ikifika 2015 January, mtu aanze kuweka nia yake ya kugombe urais, sasa hivi tunahitaji kuona wachapakazi kadhaa ili tujue ikifika 2015 nani atatusaidia kulingana na hali yetu muda huo na mahitaji yetu muda huo. Sasa ama zitto ama slaa ama mbowe ama Lissu haina maana sana. Maana kiukweli ndani ya CDM mfumo ndo utaendesha nchi sio mtu kama ilivyo ndani ya CCM.

Sio lazima hao tajwa tu, inaweza ikatokea hata mtu mwingine akapata nafasi hiyo; Please tujadili mambo mengi kama mfao ya wafanyakazi, wizi wa mali ya umma, madini, uchumi, utamaduni wetu, usalama wa raia Ulimboka etc.
 
Wasukuma wanatoka miakoa ya Shinyanga, Mwanza , Geita na Simiyu baadhi ya sehemu za Tabora na Singida maeneo ya kina mwigullu nchemba wanatabia ya kuhamia sehemu zenye rutuba ili waweze kufanya kilimo na ufugaji lakini kinachowapa nafasi ya kukubalika ni upole wao na ukarimu wao na jinsi wanavyoweza kushirikiana na kabila lolote tanzania kikubwa zaidi ni wawazi si wanafiki wanao uwezo wa kusema NO. penye dhuruma.Kumbe hawa wanautambulisho wa kabila lao.

Kwa upande mwingine kabila la WAHA wantoka kigoma inasemekana wanasifa ya ubishi na ubinafsi hawana ushirikiano na kabila lolote zaidi ya wao kwa wao yaani waha.Kumbe ubinafsi ni sifa yao inasemekana eneo lao linarutuba sana lakini wasukuma imeshindikana kuingia eneo hilo kwa sababu ya ubinafsi wa jamaa wale.Kwa hiyo CDM hii hali itawatesa na kijana msimulaumu kwani naye kazaliwa kaikuta hali hii toka kwa babu zao.Huwezi kumlaumu kwani si yeye bali ni GENE ya clan.Msameheni bure
Ndiyo maana msukuma na ng'ombe na kilimo hata asome vipi lazima afanye hiyo shughuli direct or indirect
 
Siasa za ukabila, ukanda na udini hazina nafasi katika jamii tunayoishi kwa sasa labda 2100 kama tukiwa wazima
 
wasukuma wanatoka miakoa ya shinyanga, mwanza , geita na simiyu baadhi ya sehemu za tabora na singida maeneo ya kina mwigullu nchemba wanatabia ya kuhamia sehemu zenye rutuba ili waweze kufanya kilimo na ufugaji lakini kinachowapa nafasi ya kukubalika ni upole wao na ukarimu wao na jinsi wanavyoweza kushirikiana na kabila lolote tanzania kikubwa zaidi ni wawazi si wanafiki wanao uwezo wa kusema no. Penye dhuruma.kumbe hawa wanautambulisho wa kabila lao.

Kwa upande mwingine kabila la waha wantoka kigoma inasemekana wanasifa ya ubishi na ubinafsi hawana ushirikiano na kabila lolote zaidi ya wao kwa wao yaani waha.kumbe ubinafsi ni sifa yao inasemekana eneo lao linarutuba sana lakini wasukuma imeshindikana kuingia eneo hilo kwa sababu ya ubinafsi wa jamaa wale.kwa hiyo cdm hii hali itawatesa na kijana msimulaumu kwani naye kazaliwa kaikuta hali hii toka kwa babu zao.huwezi kumlaumu kwani si yeye bali ni gene ya clan.msameheni bure
ndiyo maana msukuma na ng'ombe na kilimo hata asome vipi lazima afanye hiyo shughuli direct or indirect

hutu + tusi = wahapahapa (aka waha)
 
maneno ya kafulila jana jioni hapa dodoma

" huu mjadala watu kukana hauna maana kabisa. wote wanaokana ndio wapiga debe wakubwa. waliyasema haya wanayoyakana. ni unafiki ndio unaowasumbua na uoga. kabla ya kuondoka, wote tulikaa pale sinza na kwa pamoja wakasema wanamuunga mkono, tukafika Kigoma wakarudia maeno yale yale ya kumuunga zitto. Iweje leo wanakana? Asilimia 85% ya wabunge wanamuunga mkono zitto kugombea urais. Wana kigoma tumeonewa sana. Muda umefika kuwepo usawa katika uongozi wa hii nchi. Hatuwezi kuwa wasindikizaji siku zote, wakati uwezo tunao. Tunaungwa mkono kila kona ya nchi na hata nje ya nchi, na kama ni demokrasia 2015 rais na makamu wake lazima watokee Kigoma. Rais wa Tanzania, Afrika Kusini, ujerumani na Malaysia wote wanataka umuona rais kijana Tanzania.Vyama vyote vya siasa humu nchini wanamtaka rais kijana, Kikwete mwenyewe anamtaka atakayemrithi awe kijana"



----------------------------------
Edward Lowassa For President 2015

Oh CCM-MAMA hapa tu umetunga kwani haiwezekani mtu mwenye akili timamu akatamka maneno haya, labda awe amepagawa na pepo wa kuupenda urahisi.

Lakini kama ni maneno ya Kafulila kweli nadhani wote waliomfukuza kwenye vyama vyao wapo sahihi.
 
Mimi sioni mantiki ya ukabila,kama tukiendekeza ukabila basi wasukuma watawala milele!
Tukijadili mambo ya msingi inakuwa tunaleta UKABILA na UDINI? Ukweli uko pale pale nenda KIGOMA ndio utajua nazungumzia nini. Wapeni URAIS muone.
 
Tunachokifanya hapa ni sawa na mtu anajiandaa na mtihani lazima nondo zote uzipitie kabla ya paper, wanaosema wanagombea ni sawa kusema mapema ili tuwajadili, kwa leo tumeweza ku-exhaust kila lililo kwa zitto pros na cons tumeziweka hapa na mwisho wa siku mzani huuuuuuuuuuo unaelekea kuwamwaga zitto na kafulila tayari tumepata madhaifu ya zitto.Huyu kajimaliza tusubiri mwingine ajitokeze
 
Kama mnakumbuka mwaka 1995 KUTOKA CCM MTU WA KWANZA kutangaza nia alikuwa mzee Pius Msekwa tena litangaza mapema sana baada ya hapo walikuja BOYS 2men LAKINI BEN ze Nkapa alikuwa wa mwisho na ndiyo alikuwa chaguo la wenye chama chao.Jamani hivi vyama vina wenyewe whether u like or not wanawajua wagombea waadilifu muda ukifika mtaona yawezekana hata dr.slaa asigombee lakini wakafanya kazi ya kumtengeneza mgombea anayekubalika kama alivyofanywa Ben ze nkapa.chezea chama weyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee
 
sasa ni lazima CDM mcheze karata vizuri or else mtakuwa nikupiga kelele tu. vijana tunahitaji kulikomboa taifa hili. kama tunataka twende ikulu "we must not gamble". tumuweke kijana, msomi na mwenye vision nzuri na nchi hii. some one who is likable. nafikiri kijana Zitto akipewa nafasi kurusha bendera yetu tutakwenda ikulu. Sasa hivi tujaribu tu kumuuza kijana huyu tutafute wanachama vijana wote wa nchi hii ambao watatupigia kura na si kulumbana maana muda umekwenda. ni hayo tu.
Kama Zitto anakubalika kwa Kikwete, hakubaliki kwangu.
 
maneno ya kafulila jana jioni hapa dodoma

" huu mjadala watu kukana hauna maana kabisa. wote wanaokana ndio wapiga debe wakubwa. waliyasema haya wanayoyakana. ni unafiki ndio unaowasumbua na uoga. kabla ya kuondoka, wote tulikaa pale sinza na kwa pamoja wakasema wanamuunga mkono, tukafika Kigoma wakarudia maeno yale yale ya kumuunga zitto. Iweje leo wanakana? Asilimia 85% ya wabunge wanamuunga mkono zitto kugombea urais. Wana kigoma tumeonewa sana. Muda umefika kuwepo usawa katika uongozi wa hii nchi. Hatuwezi kuwa wasindikizaji siku zote, wakati uwezo tunao. Tunaungwa mkono kila kona ya nchi na hata nje ya nchi, na kama ni demokrasia 2015 rais na makamu wake lazima watokee Kigoma. Rais wa Tanzania, Afrika Kusini, ujerumani na Malaysia wote wanataka umuona rais kijana Tanzania.Vyama vyote vya siasa humu nchini wanamtaka rais kijana, Kikwete mwenyewe anamtaka atakayemrithi awe kijana"



----------------------------------
Edward Lowassa For President 2015

Hapa mimi sijaelewa!!!!!! kwa hiyo Kafulila anataka kusema LAZIMA rais atoke kigoma?? Au anamaanisha Mgombea wa CDM katika nafasi ya Urais lazima atokee Kigoma?? Maana huyo m"kigoma" anaweza kuteuliwa na CDM, sisi tukampigia m"songea" au m"Tanga" aliechaguliwa na CHAUMMA.

Kwani kuteuliwa na chama ndo kushinda uchaguzi???

Haya bwana...tulazimisheni.
 
maneno ya kafulila jana jioni hapa dodoma

. Tunaungwa mkono kila kona ya nchi na hata nje ya nchi, na kama ni demokrasia 2015 rais na makamu wake lazima watokee Kigoma. Rais wa Tanzania, Afrika Kusini, ujerumani na Malaysia wote wanataka umuona rais kijana Tanzania.Vyama vyote vya siasa humu nchini wanamtaka rais kijana, Kikwete mwenyewe anamtaka atakayemrithi awe kijana"

Kweli hili limekuwa BUNGE la watu WAPUUZI, wanahitaji maombezi.

RAIS, MAKAMU WA RAIS wote watoke KIGOMA? I'm mouth open and speachless!

Hivi Kafulila amejihangaisha hata siku moja kusoma KATIBA ya JMT?

Kama Wabunge wetu ni mbumbumbu wa katiba kiasi hiki, huko vijijini hali iko je?
 
aisee dhambi ya ubaguzi wa kikanda itatumaliza. loh! zitto & zo wajiangalie sana, Ikulu sio sehemu ya maonyesho ya umri sura au umbo, ni utumishi tu kwa wana wa inchi hii, tusizidi kujiroga watanzania.
 
Nilikuwa namheshimu na kumtetea Kafulila kuwa wanamuonea.leo nimeona aibu sana,kumbe haka kajamaa kana ukabila wa hivi?Sasa raisi akitoka Kigoma ndio itakuwaje?Hivi Zito wanamuona wa maana sana kiasi cha kumfikiria uraisi?mbona hana jipya?Kwanza ajitathmini ndio aseme maneno ya hivyo,ana quality gani ya ajabu?hakuna mtanzania mwenye busara anayeweza kumpa uraisi NDUMILAKUWILI,tumeisha msoma na kumjua ni opportunist lakini ameshindwa kupima uwezo wake.Anyway time will tell,I am sure anatumiwa
 
Status
Not open for further replies.
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom