MKANDARA wrote:
zote zinaandikwa na watu wenye chuki ya kimakundi, wapo washabiki wa Zitto kina Omar na wapo washabiki wa upande wa pili. Vita hii inafanana kabisa na vita ya Mwakyembe na Mwakalinga
Maslahi ya chama always. Maslahi ya chama hayawezi kuwa juu ya maslahi ya taifa. CHADEMA walikuwa sahihi kumvua uongozi Kafulila, ni vema hilo jimbo la Kigoma kusini wakalikosa kuliko kulipata kwa gharama ya kuvuruga chama.
Kaulimbiu ya siasa za bongo ya" Ukimwaga mboga sisi tutamwaga ugali" sasa pia yatawala vyama vingine nlidhan ni CCM tu kumbe umekua ni upupu poleni CHADEMAKafulila kafukuzwa au kaachia ngazi mwenyewe? Moja linaloonekana hapa, kama ilivyokuwa kwa marehemu Wangwe, tatizo ni lile lile, Mbowe na Ruzuku. Hivi haya hayatatuliki kukiokoa chama?
kwani Zanzibar sio Tanzania? ni sawa na mtu aseme CHADEMA ina wabunge wengi kutoka Kilimanjaro na haina mbunge hata mmoja kutoka Zanzibar. Wanapopiga kura bungeni haijalishi ni mbunge wa kutoka Mtwara Corridor au Kanda ya ziwa, Kutoka nyanda za juu kasikazini au nyanda za juu kusini, ni idadi ya wabunge wa bunge la JMT. Kwa hiyo ninachosema hapa ni kuwa Makakati wa kuongeza wabunge bungeni ungekuwa ni mkakati wenye tija kwa CHADEMA na unaotekelezeka.
Mfano kama CHADEMA mwakani wanapata wabunge asilimia 60 na Mh. JK Nashinda kwa asilimia 60 kwenye nafasi ya urais. Je hoja ya kuwa na waziri Mkuu kutoka Chadema haitakuwa na nguvu? Au uundwaji wa serikali ya mseto hautakuwa bayana? Kama unafuatilia sana matamshi ya viongozi wa CHADEMA utaona kabisa ni nani anaona mwenendo wa CHADEMA kwa kipimo sahihi na anaweka mikakati sahihi, ni huyu Mh. Anayekataa siasa za kuvizia na anapenda siasa za kujipanga. Ndio maana kwa hili naungana naye kuwa Inawezekana CHADEMA hawana mkakati wa kushika dola. Hata Mzee mwanakijiji ameshawaonya several times kwenye masuala mbali mbali kuwa haoneshi kama wapo serious kutaka kushika dola kweli.
Asante mkuu lakini kwanini unadhani ime-expire? ha ha ha ili niifanyie maboreshoSorry iff of point "Elizabeth Gupta - BBA Revolution, Mwaka huu ni wetu pia " Naona signature yako kama ime-expire vile!!!
hawawezi kulikosa jimbo kwa sababu ya Kafulila!!! Winners never quit and Quiters never win!!!!!!!! Kafulila kwa kuondoka CHADEMA amefulila na hataweza kushinda as he has quited! watch out this space.Maslahi ya chama always. Serikali inaogopa kumchukulia hatua Rostam kulinda maslahi ya chama. Waziri wa utawala bora anawafyatukia wenzake ili kulinda maslahi ya chama. Maslahi ya chama hayawezi kuwa juu ya maslahi ya taifa. CHADEMA walikuwa sahihi kumvua uongozi Kafulila, ni vema hilo jimbo la Kigoma kusini wakalikosa kuliko kulipata kwa gharama ya kuvuruga chama.
UMEKIPIMA KWA KIGEZO KIPI?.....Jambo moja kubwa nalo ni kuwa CHADEMA ni chama kikubwa .
Asante mheshimiwa, Inawezekana mumelewa sifa sasa, kwa hiyo hamfikirii njia mbadala za kusolve matatizo ya CHAMA kwa amani bila kutoa ufa wa kukikosesha nafasi yakuvuna wanachama wengine na pia kupata wabunge wengi bungeni. Umesoma post zangu tatu za nyuma kwenye hii thread? Mumebeba ajenda za watanzania, Mumebeba matumaini yetu, tunawajadili kwa kuwa tunaawamini kuwa ninyi ndio ukombozi wa kweli kujadili kwetu huku ni kutokana na kuwa upepo unaovuma unaonyesha mwelekeo usio kuwa sio. Tunajaribu kuwakumbusha msilewe sifa za kuwa na washabiki wengi, kuweni na mkakati madhubuti wa kuweza kuabadirisha hali ya nchi, nayo ni kuliteka bunge, ndoto inayoweza kutimia kirahisi kabisa (bila hata bajeti ya helkopita,)maana kwa kufanya hivyo mtaibeba ajenda ya watanzania sawa sawa. Umenipata?
Kigezo kilichotumika na hata kwa kuangalia , anayesemwa sana na watu ndio anajulikana hata kama anasemwa kwa ubaya ama uzuri -lengo letu ni kuwatumikia watanzania , na tuliingia humu tukijua kuwa kuna challenge nyingi na dawa sio kuzikimbia ila kuzikabili.
hawawezi kulikosa jimbo kwa sababu ya Kafulila!!! Winners never quit and Quiters never win!!!!!!!! Kafulila kwa kuondoka CHADEMA amefulila na hataweza kushinda as he has quited! watch out this space.
UMEKIPIMA KWA KIGEZO KIPI?
Asante mheshimiwa, Inawezekana mumelewa sifa sasa, kwa hiyo hamfikirii njia mbadala za kusolve matatizo ya CHAMA kwa amani bila kutoa ufa wa kukikosesha nafasi yakuvuna wanachama wengine na pia kupata wabunge wengi bungeni. Umesoma post zangu tatu za nyuma kwenye hii thread? Mumebeba ajenda za watanzania, Mumebeba matumaini yetu, tunawajadili kwa kuwa tunaawamini kuwa ninyi ndio ukombozi wa kweli kujadili kwetu huku ni kutokana na kuwa upepo unaovuma unaonyesha mwelekeo usio kuwa sio. Tunajaribu kuwakumbusha msilewe sifa za kuwa na washabiki wengi, kuweni na mkakati madhubuti wa kuweza kuabadirisha hali ya nchi, nayo ni kuliteka bunge, ndoto inayoweza kutimia kirahisi kabisa (bila hata bajeti ya helkopita,)maana kwa kufanya hivyo mtaibeba ajenda ya watanzania sawa sawa. Umenipata?
Na ndio maana chama kinaendelea na program zake kama kawaida, tuchangie ili tuweze kuwafikia watanzania ambao hawawezi kuingia kwenye huu mtandao nawe andika neno CHADEMA tuma kwenda 15710 na hii ni mitandao ya voda na zain tuu.
Mpaka Kieleweke,
Pesa yetu mnaitaka lakini;Kwa nini msirekebishe haya kabla ya kuja kutuchomoa?
- Ushauri wa matumizi hamsikilizi
- Uwazi wa matumizi unaolalamikiwa haupo
- Wanaosaini Check lazima iwe ni Mbowe na Komu na mara chache Dr.Slaa, why?
Ulitaka nani asaini cheque?
Wanaosaini si wanasaini kwa vyeo vyao? kama leo yuko Komu ndio mkurugenzi wa fedha ulitaka asaini afisa habari? ama mkurugenzi wa mambo ya nje?
Mbona hujiulizi kwanini Makamba anasaini cheque? sio kwa sababu yeye ni Makamba ila ni cheo chake.
Na anayesema eti Lipumba hasaini cheque ni muongo wa kutupwa na hajui, ukweli ni kuwa anasaini na ipo account moja inaitwa ya uchaguzi ambayo wanaosaini ni Lipumba na Maalim tuu.