Duuu si ni UKawa hiyo hiyo,unatoka sebuleni unahamia chumbani
NJAA MBAYA! Vijana tusikimbilie siasa tu!
Ah wapiLowasa, Sumaye na Kingunge watarudi CCM.
Wewe ulitakaje? Au umeshajisaulisha kwamba Kafulila alikuwa hana mahusiano mazuri na viongozi wake wa NCCR? Kuhamia CHADEMA ni kama mwanafunzi kubadili sehemu anayokaa darasani lakini bado yumo kwenye darasa lilelile!Mpango wa chadema kuua NCCR,CUF unaenda kwa kasi sana.Kama NCCR ni ukawa kwanini ahamie Chadema ambao ni washirika katika ukawa?
Arudi tu
Kahamia kwa mkewe si unajua mkewe ni mbunge wa viti maalumu Chadema.Mama akiwa na kazi au nyumba mwanaume Ukawa huna kazi au nyumba kuhamia kwa mke ili maisha yaendelee si kitu cha ajabu.Na kila ukiamka huko ulikohamia lazima kila asubuhi umwamkie mke Shikamoo mke wangu maana ndie anakuweka mjini.
Lipo wapi hilo tatizo? Tatizo ni watanzania kuwa tumekaririshwa kwamba kuwa kwenye chama ni kama mtu umelishwa yamini kwamba ukitoka basi utakufa!!Tatizo lipo
Mkuu ccm ni zaidi ya chama cha SIASA????naona kwa mbalii Mamvi na Kingunge wanachanga karata zao. Lengo kuuwa cuf, nccr, act na kutengeneza chama kimoja cha upinzani chenye nguvu. Taadhali wajue tu kwamba CCM ni chama dola, ni zaidi ya chama cha siasa. Kukiwa na chama kimoja cha upinzani chenye nguvu kazi ni rahisi sana kwa CCM ku deal nacho.