Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 97,070
- 136,458
Jumapili njema raia.
Sasa bana, neno la leo ni kuhusu miadi ya makutano ya watu wawili walio na raghba ya kuja kuweza kuwa wenza hapo baadaye.
Mkaka na mdada wanawasiliana kwenye simu. Wanapanga muda na sehemu ya kukutana ili waweze kujuana vizuri.
Siku ya siku inafika na kila mmoja wao anajiandaa vile awezavyo. Mara nyingine hao wawili huongozana na rafiki zao huko kwenye miadi. Nadhani wadada ndo hupenda zaidi kufanya hivyo, jambo ambalo mimi huliona ni la kishenzi.
Mimi na wewe ndo tumepanga tukutane. Wewe unaleta gurudumu la tatu la nini? Ni ushenzi tu.
Hata hivyo, hiyo si hoja yangu kwa leo. Nilikuwa nachomekea tu kama Anko Magu.
Basi bana...mnafika sehemu ya mkutano wenu...mnasalimiana. Kama ni vinywaji mnaagiza halafu mnaendelea na yenu.
Cha kustaajabisha sasa....unakuta kila mtu ana simu....iwe ki Tecno (sijui ndo inaandikwa hivyo), Samsung kuukuu, au ki iPhone cha ajabu ajabu ambacho pengineo ni cha bandia.
Baada ya maongezi kidogo unastukia kila mtu kajiinamia na kibyongo chake. Kila mtu kama si anachati kwenye magrupu ya Whatsapp basi yuko sijui Instagram huko au Snapchat.
Unakuta mtu yuko kwenye rundo la magrupu. Hapo alipo kwenye kideti chake lakini huko kwenye magrupu anatongozana na wengine.
Au unakuta mwingine yupo kwenye hicho kideti lakini yupo kwenye magrupu huko anagombana na wenzake.
Ambacho sikielewi sasa...kwa nini watu muende kwenye miadi yenu halafu badala ya kuongea na kujuana vizuri mnaishia kuchati kwenye magrupu ya Whatsapp?