Darassa -‘Nimewahi kwenda kwa Mganga wa kienyeji kueleza shida zangu’

STUNTER

JF-Expert Member
Dec 15, 2015
13,075
17,237
Msanii wa bongofleva Darassa ambaye jina lake limeongoza kwa kutajwa mara nyingi kwenye
namba kubwa za chati za Radio/TV Tanzania
kutokana na hit single ya ‘muziki‘ amekaa kwenye Exclusive Interview na Diva kwenye Ala za Roho CloudsFM. Diva amemuuliza Darassa maswali mbalimbali
ikiwemo ya maisha yake ya kimapenzi na maisha
ya mtaani kwa ujumla ambapo Darassa amekiri
kwamba aliwahi kwenda kwa mganga wa kienyeji
ili kutafuta suluhisho la maisha aliyokua anayapitia. Amesema ‘Nimeshawahi kwenda mganga zamani sana, ni miaka imepita na sababu ya kwenda
haikuhusiana na muziki bali maisha yangu binafsi,
kwenye maisha ya uswahilini ni vitu vingi
vinatokea na ilikua ni ushawishi wa watu
wengine…. sikupewa dawa wala sikuchanjwa
taratibu za mganga zilinifanya nisifikie huko‘ ‘Kwenye akili ya kujitambua unaambiwa vitu vingi kama kijana au mtu anaetafuta maisha unaweza ukachanganywa na vitu vingi sana lakini nakwambia Mungu ni wa ajabu sana, miaka ambayo nilikwenda kwa Mganga nilikua bado sijaiachia ‘sikati tamaa’ na sikuwahi kufanikiwa ‘ – Darassa
 
Mganga wa kienyeji mbona anadharaurika sana.Au mpaka tuwaite Waganga wa Tiba Mbadala.Mimi mwenyewe nilishawahi kwenda zamani sana enzi za kufukuzia vibinti vya kike.Cha kushangaza nilifanikisha zoezi la kupita naye niliyemuendea kwa Mganga.
 
Tatizo raia wanaamini ukitumia NDUMBA unafanikiwa kirahisi.....kitu amabacho baadae kinakuja kukugharimu..
 
Back
Top Bottom