Darasa; Mambo ya Kuzungumza na Mchumba Kabla ya Ndoa

Nicas Mtei

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2010
Posts
11,556
Reaction score
7,113
black-couple-talking.jpg

Baada ya kuvishwa pete ya uchumba, wasichana wengi huona kwamba kilichoko mbele yao ni kupanga harusi tu. Hujishughulisha kwa hali na mali kuhakikisha harusi inakuwa sawa na ile anayoiwaza siku zote, na kusahau kuwa baada ya harusi kuna maisha ambayo ndiyo haswa yanayopaswa kupangiliwa kwa umakini. Baadaye wanajikuta wameingia kwenye ndoa huku mambo mengi yakiwa hewani na hivyo kupelekea migogoro isiyoyalazima mara tu baada ya ndoa.

Kuna mambo muhimu sana ambayo wachumba wanapaswa wayaongelee na kufikia muafaka kabla ya kuunganika na kuwa mwili mmoja. Yanaonekana ya kawaida sana lakini yanaweza kuleta msuguano na kuharibu kabisa furaha ya ndoa. Tuyaangalie kwa uchache:

1. Mahali pa kuabudu.

Binti anaabudu katika kanisa kubwa na ndiye kiongozi wa sifa na muongozaji wa nyimbo karibia zote za kwaya, na kijana anaabudu kwenye kanisa dogo linaloanza na ndiye mwenyekiti wa vijana na mwalimu wa shule ya jumapili. Hapa nani anamfuata nani? Bila kukaa chini na kujadiliana kwa pamoja jambo hili linaweza kuleta mvutano. Ni vyema mkaangalia kwa mapana na marefu option zote kisha kwa pamoja mfikia muafaka kulingana na huduma ya kila mmoja wenu.

2. Jinsi ya Kuishi

Waafrika ni kawaida yetu kuishi pamoja na ndugu zetu na kusaidiana katika mambo mbalimbali ya maisha. Sio jambo geni kumkuta kijana au msichana anaishi na wadogo zake na kuwasomesha. Linapokuja suala la ndoa ni vyema jambo hili likawekwa sawa mapema. Je mtaweza kuishi na ndugu wangapi? Na wa upande upi na kwa kigezo gani? Je wataanza kuishi nanyi muda gani baada ya kuoana? Pale tu mtakapooana au lini? Hili si jambo dogo na linaweza kuharibu amani kabisa ndani ya nyumba. Ni vyema mkaliweka sawa mapema na wale mnaoishi nao wajue hawaishi tena na kaka au dada bali Mr & Mrs hivyo heshima iwe kwa wote. Pia sishauri kuishi nao mara tu baadavya kuoana, ni bora wakaenda kwa ndugu wengine angalau mwezi mmoja wa kwanza muweze kuwa na wakati wenu wa faragha wa kufahamiana vizuri na kuizoea nyumba yenu mkiwa wenyewe.

3. Mapato na Matumizi

Hili ni eneo nyeti sana. Wasichana wengine wanapoolewa huambiwa kuwa ‘usimwambie mumeo unapata kiasi gani na uwe na akaunti yako ya siri.’ Mmh hapa pana tatizo, maana nijuavyo mimi mwili mmoja ni katika kila idara, hamna siri. Sasa wewe ukificha na mwenzio akaficha, kuna maendeleo kweli hapo? Ni muhimu sana kwa wachumba kukaa na kupanga jinsi ya kuyatumia mapato yenu mtakapooana. Muwe wawazi kila mmoja anachokipata na muainishe matumizi yenu na kuangalia ni kwa jinsi gani mtaweza kuyafanikisha.

Baada ya kuoana, kila kitu kitakuwa ni chenu wote. Kama ulikuwa na nyumba, gari, viwanja, shares, bank accounts n.k vyote vinakuwa mali ya familia, hivyo ni vyema mkaangalia hili mapema ili asije mmoja wenu akajenga nyumba kwa siri bila mwenzie kujua. Pia muangalie ni ndugu gani wanahitaji msaada kifedha na jinsi gani mtaendelea kuwasaidia, mfano ada, matibabu, n.k. Hapa panahitaji hekima kubwa sanabya kiMungu kuamua nani asaidiwe kulingana na kipato chenu kwa wakati huo. Maana ndugu wa kuhitaji msaada wenu watakuwa ni wengi kuliko uwezo wenu. Hapa ndipo mstari wa mithali 14:1 unapoleta maana.
Mithali 14:1 Kila mwanamke aliye na hekima hujenga nyumba yake; Bali aliye mpumbavu huibomoa kwa mikono yake mwenyewe.

4. Mipango ya Mbeleni

Shule, ujenzi, kuanzisha familia, kufungua biashara, kuanzisha huduma n.k yote haya yanahitaji kuzungumziwa mapema na kuwekewa misingi. Mfano wewe unahitaji baada tu ya ndoa utafute scholarship ukasome ulaya wakati mwenzio akifunga macho tu anajiona anaitwa baba, hapo lazima shida itatokea. Lazima mjue vipaumbele vyenu kama familia ni nini. Mkishafahamu hilo ni rahisi kujua muanzie wapi na wakati gani. Mume hawezi tu kuamka asubuhi na kusema anaacha kazi na kuanzisha kanisa, sasa familia itakula wapi? Ni lazima mkae chini mpange mjue mume akiacha kazi familia itaishije, mke je atakuwa tayari kubeba majukumu yote?

Mwisho huu ndio wakati muafaka kumweleza mwenzio kama uliwahi kuchumbiwa hadi kutolewa mahari lakini mambo yakaharibika. Pia kama unamtoto ni lazima narudia LAZIMA umweleze mwenzi wako. Usiingie kwenye ndoa na siri yoyote, itakuwa ni bomu la kuwasambaratisha.

Nakutakia ndoa njema yenye baraka, amani na furaha tele.
 
Ni sawa kabisa kuongea hayo na mengine mengi .

Ila maisha yanabadilika kama upepo .
yaaani ni kama vile umejitayarisha ku takeoff kwenye runway 34
next mnt the wind changes to runway one, one.

anyway my point is
Ni muhimu kuwa na plans lakini
kuwa flexible ili plan ziki change kutokana
na circumstances fulani za maisha uko tayari ku adapt
na hauta kuwa gizani wala kuchanganyikiwa ..

kuwa na plan A, B .....................Z.

at the end of the day
Life goes on....................
 
Asante kwa mada nzuri, very relevant.
Namba moja ni muhimu kuongelea kabla hata ya first date!

Umesahau kuongelea ZERO TOLERANCE zones! Mfano, binafsi kabla hata ya kujizoesha mtu naweka mezani msimamo wangu juu ya mambo 3 ambayo hayakubaliki, hayajadiliki na hayavumiliki. Kuna tigo-utilization, imani za kishirikina (namaanisha je mwenza anadhani waganga wa kienyeji na rituals zinasaidia?) na tatuni physical abuse!

Hiyo ya kuhifadhi hela kwa siri, nakuahidi sio kwa ajili ya nia mbaya. Imeandikwa pia mwaamke atamlinda mwanaume. Labda kiswahili tuseme atamsitiri (manake ulinzi ni nguvu zaidi). Wanaume tukubaliane, mna style yenu ya matumizi. Na mnapenda kupanga matumizi yasiyo ya lazima. Lakini kuna siku utaambiwa kuna msiba kwenu wakati hamna hela na mkeo akaokoa jahazi. Ama mkapata ugeni wa ghafla, mgonjwa amabe hana insurance etc na mama akakuokoa. Dont be negative about it. Paw akiniambia kuna kiwanja kinauza kiasi kadhaa, namuambia nina kiasi kadhaa hebu tafuta cha kuongezea.

Tatizo linapokuja mnapotaka kuweka bifu la kipato nyumbani. Na haiwezekani tukaweka kipato wazi kwa matumizi na bado ukamudu kurudi saa sita usiku na ndyofu kadhaa kichwani. Labda uje na risiti ya tra kama ya samaki samaki nione na st anna hapo na waweke na jina la mnywaji hehehehe.
 
Ni kweli kabisa @Afrodenzi...... mara nyingi watu huwa wanajisahau sana katika mahusiano... inapotokea mabadiliko wanajikuta wanaumia na kushindwa kuhimili mikikimikiki ya mabadiliko katika mipango ya mahusiano yao....... ni vyema kuwa na tayari na hali yoyote
 
Asante kwa mada nzuri, very relevant.
Namba moja ni muhimu kuongelea kabla hata ya first date!

Umesahau kuongelea ZERO TOLERANCE zones! Mfano, binafsi kabla hata ya kujizoesha mtu naweka mezani msimamo wangu juu ya mambo 3 ambayo hayakubaliki, hayajadiliki na hayavumiliki. Kuna tigo-utilization, imani za kishirikina (namaanisha je mwenza anadhani waganga wa kienyeji na rituals zinasaidia?) na tatuni physical abuse!

Hiyo ya kuhifadhi hela kwa siri, nakuahidi sio kwa ajili ya nia mbaya. Imeandikwa pia mwaamke atamlinda mwanaume. Labda kiswahili tuseme atamsitiri (manake ulinzi ni nguvu zaidi). Wanaume tukubaliane, mna style yenu ya matumizi. Na mnapenda kupanga matumizi yasiyo ya lazima. Lakini kuna siku utaambiwa kuna msiba kwenu wakati hamna hela na mkeo akaokoa jahazi. Ama mkapata ugeni wa ghafla, mgonjwa amabe hana insurance etc na mama akakuokoa. Dont be negative about it. Paw akiniambia kuna kiwanja kinauza kiasi kadhaa, namuambia nina kiasi kadhaa hebu tafuta cha kuongezea.

Tatizo linapokuja mnapotaka kuweka bifu la kipato nyumbani. Na haiwezekani tukaweka kipato wazi kwa matumizi na bado ukamudu kurudi saa sita usiku na ndyofu kadhaa kichwani. Labda uje na risiti ya tra kama ya samaki samaki nione na st anna hapo na waweke na jina la mnywaji hehehehe.

kwenye RED Hayo hapo ni mambo ambayo mnapaswa kuyazungumza hata kabla hamjafikia hatua ya kuvishana pete... ni mambo ambayo inawabidi mtambuane katika hatua za mwanzo kabisa za mahusiano yenu.

Kwenye BLUE hapo sasa itawabidi kila mmoja awe na taarifa na mipango ya utunzaji huo wa pesa.. hyo yaweza kuepusha mifarakono katika mahusiano

hapo pa KIJANI umenivunja mbavu.... yaani bila kuja na risiti za TRA hamtapatana? we mwana we
 
kwenye RED Hayo hapo ni mambo ambayo mnapaswa kuyazungumza hata kabla hamjafikia hatua ya kuvishana pete... ni mambo ambayo inawabidi mtambuane katika hatua za mwanzo kabisa za mahusiano yenu.

Kwenye BLUE hapo sasa itawabidi kila mmoja awe na taarifa na mipango ya utunzaji huo wa pesa.. hyo yaweza kuepusha mifarakono katika mahusiano

Hahaha, sasa kuna mwingine akijua tu kuna hiyo hela ya akiba ndo anataka kuipangia matumizi. Unajua kuna watu hawaishi na hela nyumba moja, lol! Im an african woman, mwanaume anaangalia familia. Na mie namsaidia kwenye kuendeleza mali za familia. Kwa sababu siwezi na hatuna ng'ombe wa kuchunga na 'kitonndo' cha kufyagia, na shamba la kulima: basi akitaka kununua shamba, gari, kujenga etc aaah namchukulia hata mkopo. Tatizo lenu wanaume mnasusa na mnakataa kushirikishana maamuzi. Mwishowe mwanamke anaenda lwake na mwanaume lwake!
 
Kaka Nicas Mtei, Naomba nikuulize swali....
Ni vema Ku-Do Before Stage yoyote kuelekea Marriage?

Imani za dini nyingi huwa zinazuia... ila kwa mahusiano ya siku hizi inakuwa ni ngumu sana kwa wachumba kuto DO... ni wachache sana ambao wamefaulu mtihani huo
 
Ni sawa kabisa kuongea hayo na mengine mengi .

Ila maisha yanabadilika kama upepo .
yaaani ni kama vile umejitayarisha ku takeoff kwenye runway 34
next mnt the wind changes to runway one, one.

anyway my point is
Ni muhimu kuwa na plans lakini
kuwa flexible ili plan ziki change kutokana
na circumstances fulani za maisha uko tayari ku adapt
na hauta kuwa gizani wala kuchanganyikiwa ..

kuwa na plan A, B .....................Z.

at the end of the day
Life goes on....................

Afrodenzi = Naomba software ya kunasa maongezi ya simu ya MCHUMBA WANGU kwa njia ya GPS na kusoma txt, bila kugusa simu ya mhusika.
... Asante mkuu' natanguliza shukrani.
 
Hahaha, sasa kuna mwingine akijua tu kuna hiyo hela ya akiba ndo anataka kuipangia matumizi. Unajua kuna watu hawaishi na hela nyumba moja, lol! Im an african woman, mwanaume anaangalia familia. Na mie namsaidia kwenye kuendeleza mali za familia. Kwa sababu siwezi na hatuna ng'ombe wa kuchunga na 'kitonndo' cha kufyagia, na shamba la kulima: basi akitaka kununua shamba, gari, kujenga etc aaah namchukulia hata mkopo. Tatizo lenu wanaume mnasusa na mnakataa kushirikishana maamuzi. Mwishowe mwanamke anaenda lwake na mwanaume lwake!
Suala muhimu hapo ni kutokuwa m binafsi katika hilo suala... Bofya mada hii HAPA ya Dada AshaDii.....itakufafanulia kuhusu suala zima la ubinafsi na mambo mengine mengi....
 
Last edited by a moderator:
KING'AST hiyo ya tigo utilization usiseme kabisa!!acha!!! unaweza usiitumie kumbe jamaa fulani anapelekewa every end of month tena with no cost.gharama zote kalipia King'ast
 
Imani za dini nyingi huwa zinazuia... ila kwa mahusiano ya siku hizi inakuwa ni ngumu sana kwa wachumba kuto DO... ni wachache sana ambao wamefaulu mtihani huo

Sio kwa wanaume wetu hawa wa Kibongo
 
Imani za dini nyingi huwa zinazuia... ila kwa mahusiano ya siku hizi inakuwa ni ngumu sana kwa wachumba kuto DO... ni wachache sana ambao wamefaulu mtihani huo

... Ndiyo maana siku hizi wengi wanafunga ndoa wakiwa na ujauzito, na wengine wakiwa na wajukuu.
 
black-couple-talking.jpg

Baada ya kuvishwa pete ya uchumba, wasichana wengi huona kwamba kilichoko mbele yao ni kupanga harusi tu. Hujishughulisha kwa hali na mali kuhakikisha harusi inakuwa sawa na ile anayoiwaza siku zote, na kusahau kuwa baada ya harusi kuna maisha ambayo ndiyo haswa yanayopaswa kupangiliwa kwa umakini. Baadaye wanajikuta wameingia kwenye ndoa huku mambo mengi yakiwa hewani na hivyo kupelekea migogoro isiyoyalazima mara tu baada ya ndoa.

Kuna mambo muhimu sana ambayo wachumba wanapaswa wayaongelee na kufikia muafaka kabla ya kuunganika na kuwa mwili mmoja. Yanaonekana ya kawaida sana lakini yanaweza kuleta msuguano na kuharibu kabisa furaha ya ndoa. Tuyaangalie kwa uchache:

1. Mahali pa kuabudu.

Binti anaabudu katika kanisa kubwa na ndiye kiongozi wa sifa na muongozaji wa nyimbo karibia zote za kwaya, na kijana anaabudu kwenye kanisa dogo linaloanza na ndiye mwenyekiti wa vijana na mwalimu wa shule ya jumapili. Hapa nani anamfuata nani? Bila kukaa chini na kujadiliana kwa pamoja jambo hili linaweza kuleta mvutano. Ni vyema mkaangalia kwa mapana na marefu option zote kisha kwa pamoja mfikia muafaka kulingana na huduma ya kila mmoja wenu.

2. Jinsi ya Kuishi

Waafrika ni kawaida yetu kuishi pamoja na ndugu zetu na kusaidiana katika mambo mbalimbali ya maisha. Sio jambo geni kumkuta kijana au msichana anaishi na wadogo zake na kuwasomesha. Linapokuja suala la ndoa ni vyema jambo hili likawekwa sawa mapema. Je mtaweza kuishi na ndugu wangapi? Na wa upande upi na kwa kigezo gani? Je wataanza kuishi nanyi muda gani baada ya kuoana? Pale tu mtakapooana au lini? Hili si jambo dogo na linaweza kuharibu amani kabisa ndani ya nyumba. Ni vyema mkaliweka sawa mapema na wale mnaoishi nao wajue hawaishi tena na kaka au dada bali Mr & Mrs hivyo heshima iwe kwa wote. Pia sishauri kuishi nao mara tu baadavya kuoana, ni bora wakaenda kwa ndugu wengine angalau mwezi mmoja wa kwanza muweze kuwa na wakati wenu wa faragha wa kufahamiana vizuri na kuizoea nyumba yenu mkiwa wenyewe.

3. Mapato na Matumizi

Hili ni eneo nyeti sana. Wasichana wengine wanapoolewa huambiwa kuwa ‘usimwambie mumeo unapata kiasi gani na uwe na akaunti yako ya siri.’ Mmh hapa pana tatizo, maana nijuavyo mimi mwili mmoja ni katika kila idara, hamna siri. Sasa wewe ukificha na mwenzio akaficha, kuna maendeleo kweli hapo? Ni muhimu sana kwa wachumba kukaa na kupanga jinsi ya kuyatumia mapato yenu mtakapooana. Muwe wawazi kila mmoja anachokipata na muainishe matumizi yenu na kuangalia ni kwa jinsi gani mtaweza kuyafanikisha.

Baada ya kuoana, kila kitu kitakuwa ni chenu wote. Kama ulikuwa na nyumba, gari, viwanja, shares, bank accounts n.k vyote vinakuwa mali ya familia, hivyo ni vyema mkaangalia hili mapema ili asije mmoja wenu akajenga nyumba kwa siri bila mwenzie kujua. Pia muangalie ni ndugu gani wanahitaji msaada kifedha na jinsi gani mtaendelea kuwasaidia, mfano ada, matibabu, n.k. Hapa panahitaji hekima kubwa sanabya kiMungu kuamua nani asaidiwe kulingana na kipato chenu kwa wakati huo. Maana ndugu wa kuhitaji msaada wenu watakuwa ni wengi kuliko uwezo wenu. Hapa ndipo mstari wa mithali 14:1 unapoleta maana.
Mithali 14:1 Kila mwanamke aliye na hekima hujenga nyumba yake; Bali aliye mpumbavu huibomoa kwa mikono yake mwenyewe.

4. Mipango ya Mbeleni

Shule, ujenzi, kuanzisha familia, kufungua biashara, kuanzisha huduma n.k yote haya yanahitaji kuzungumziwa mapema na kuwekewa misingi. Mfano wewe unahitaji baada tu ya ndoa utafute scholarship ukasome ulaya wakati mwenzio akifunga macho tu anajiona anaitwa baba, hapo lazima shida itatokea. Lazima mjue vipaumbele vyenu kama familia ni nini. Mkishafahamu hilo ni rahisi kujua muanzie wapi na wakati gani. Mume hawezi tu kuamka asubuhi na kusema anaacha kazi na kuanzisha kanisa, sasa familia itakula wapi? Ni lazima mkae chini mpange mjue mume akiacha kazi familia itaishije, mke je atakuwa tayari kubeba majukumu yote?

Mwisho huu ndio wakati muafaka kumweleza mwenzio kama uliwahi kuchumbiwa hadi kutolewa mahari lakini mambo yakaharibika. Pia kama unamtoto ni lazima narudia LAZIMA umweleze mwenzi wako. Usiingie kwenye ndoa na siri yoyote, itakuwa ni bomu la kuwasambaratisha.

Nakutakia ndoa njema yenye baraka, amani na furaha tele.
asomaye na afahamu
 
Back
Top Bottom