Kama hujui kitu ama ukae kimya au google katiba ya jamhuri wa muongano Tanzania hala nenda kwenyekipengele husika ndiyo uje na ujinga wako....mhe. kanyunyu una hakika na ulichokiandika? bw. maneno alikuwa mbunge wa jimbo la chalinze katika bunge lililopita na minimum qualification ya ubunge ni elimu ya kidato cha nne, ni vipi angeukwaa ubunge bila kuwa na elimu hiyo. kumbuka huyu aligombea na omary madega kwenye kura za maoni ndani ya ccm mwaka 2005 ambaye kwa vyovyote asingenyamaza angemlipua tu maneno kama kweli ni darasa la saba. bunge lililopita mbunge pekee aliyefahamika kutokuwa na elimu ya kidato cha nne ni samwel chitalilo aliyekuwa mbunge wa buchosa. wapiga kura walimfungulia kesi ya kudanganya kuhusu elimu yake lakini kwasababu ambazo hazijulikani kesi hiyo haikufanikiwa.
Hukuona kazi ya Mkuu wa wilaya kule Igunga, wanamchango mkubwa sana kwa serikali ya CCM...nafikiri hakuna ajuaye kazi ya mkuu wa wilaya yenye kupimika na kwa ajili hiyo kisomo siyo tatizo kwa CCM.
Kikubwa ni uwezo wa kusaidiana na Msimamizi wa Uchaguzi KUIBA kura na kuchakachua matokeo kiasi kwamba hata Mbunge wa upinzani ile kura aliyojipigia inapotea pia
umekosea anaitwa dr dr dr dr Vasco da gama msonga....Jaman tukumbuke kua tuna maprof na ma dr.wametufikisha tulipo.imagine dr.vasco da gama.may be huyo la saba ana za kuzaliwa.
Ndo maana amepelekwa KIGOMA,,,,,NO CHALLENGES OVA THERE
mhhh. kazi kwelikweli, kama ni darasa la 7 kwelikweli atakuwa hata ung'eng'e haupandi! na ikitokea wakija wageni kutembelea wilaya yake kutoka ng'ambo atakuwa anawakimbia kama mshikaji wangu fulani ambaye ni mwenyekiti wa halmashauri na ni standard 7 lever anapatashida sana wakija wageni lazima atakula kona na kumwachia kazi makamu mwenyekiti wa halmashauri ambaye ni form 4 amsaidie kazi
Mkuu thats true,na nipo ofisi na jamaa angu mmoja hapa anasema huyu bwana anamjua tokea kitambo hapo Bagamoyo kuwa hana lolote na hana ujenzi wa hoja zaidi ya ubabe,ngoja tumcheki atakuja na kasi gani hapa Kigoma ila mwenzie Mongella ndio alikua anapga siasa sana hapa namna ya kuilinda hii ccm,nashukuru alikoenda Arusha watamtia adabu na ubabe wake huo.
Unatafuta ugomvi wewe, wangempeleka A town
Hivi hawa wasomi wetu tunaojitapa nao wamelisaidiaje Taifa letu?
inawezekana ikawa kweli fanya utafiti ..hebu fikiria mtu yupo form one lakini hawezi kusoma na kuandika kwa ufasaha...hata wenye digree hawawezi kujieleza kwa mambo ya kawaida tu kwa kiingereza hii nimeiona mwenyewe kwenye michujo ya baadhi ya enteview kwa mfano mtu anulizwa umetoka wapi? kuja hapa anasema nimetoka mwanza swali lingine lina kuja hivi ............explain your journey from mwanza to dar
unatamani umpige
Mkuu unashaanga Darasa la Saba kuteuliwa kuwa DC?Mbona ushangai Profesa kuchakuliwa kuwa Waziri asiyekuwa na wizara maalumu!
Ukishaa staajabu ya Mussa utayaona ya Firauni!