Darasa la kupigilia pamba kijanja

Habari wakuu,

Nimeona na mimi nitoe darasa kidogo kuhusu mavazi sababu na mimi ni kipaumbele changu katika maisha.

1.Epuka kuvaa marangirangi
Wakati unamatch mavazi jitahidi kupunguza idadi ya rangi,rangi 3 tu zinatosha kukutoa bomba.
7af7aaaf7345a87c091b24ea071e6ea2.jpg


2. Vaa kulingana na mazingira/sehemu
Mtu mjanja anajua kubadilika kulingana na mazingira,sio kuvaa jezi la Man utd lenye jina la Wazza kwenye sherehe.
682feac35e6012400de3ccc95fe6451a.jpg
b51129054b1bc8db689b2aa5aa68d038.jpg


3. Masharti ya kuchomekea;
* Marufuku kuvaa oversize/undersize
* Usivae mlegezo
* Hakikisha singlet haionekani
* Usivae mkanda mrefu
* Usivae makubanzi/sandals
* Hakikisha umemach rangi
a858110041666998af8e8cf6741da5d0.jpg


4. Kama umevaa pensi /kaptula...
* Hakikisha unavaa soksi fupi zisizoonekana
* Piga raba au makubanzi/sandals bila soksi
* Haipendezi kuchemekea
* Hakikisha miguu ni soft
e186f5adbb83472ec3e02b254619f541.jpg
b03d0102663f3a9f0cdd5a06bf43f22c.jpg
92abf51a5d9cbebe31d55155ba5f8647.jpg


5. Usivae shati jeupe kama la mwanafunzi
Shati nyeupe ni nzuri kama unaijulia wakati unanunua hakikisha ina urembo wa aina yoyote ile au ni ya kimtindo sio kuvaa shati la shule.
0544b7f62d281aa4861bbd867323483a.jpg


6. Hakikisha una suruali nyeusi
Mwanaume yoyote yule wa kijanja anajua umuhimu wa suruali nyeusi sababu inamatch mashati ya rangi nyingi.
6c38a77ca2b76b59cd3c995e2413f2c2.jpg


7. Saa
*Kama umevaa jeans/kadet unaruhusiwa kuvaa saa ya aina yoyote
*km umevaa suti/suruali ya kitambaa epuka kuvaa saa ya mkanda wa plastic.
a55e604b73469ebba13f064da8aadedc.jpg
f6b82927b1639a280c0e9bf80ee2cc96.jpg
bb562ebc465e502d31275ee189deb85a.jpg
3ad27555edd1291d60ab6b44df9986fa.jpg


8. Miwani
Duh hapa pagumu kidogo lakini cha msingi zingatia muundo wa kichwa chako pamoja na aina ya macho uliyonayo na aina ya pamba ulizovaa pia.Sio umepiga jeans kali,kichwa kama madenge na macho kama bundi kisha unapiga miwani ndogo ya njano,ni kituko.
c00b5f6af53bb5adbb80236b9640ad8c.jpg
0f2b06f16e0e5258c47c145a7bb31931.jpg
b0f81d79519fa57e12ae0bd30b68c561.jpg


9/.Vaa kofia za kijanja
Kofia pia huongeza mvuto,chagua kofia kulingana na aina ya kichwa na mavazi uliyovaa,haipendezi kuvaa suti na kapelo.Kanzu sharti ivaliwe na barakashia ndo utaeleweka la sivyo ni sawa na kuvaa dera tu
ac6d7b2e0efc8f8d736bb50b43192bc3.jpg


10/Mkanda
*Usivae mkanda mrefu km vile umefunga nyoka kiunoni
*Mikanda ya vitambaa au madoidoi inafaa kuvaliwa na jeans/kadeti/kaptula
*Zingatia upana wamkanda na rux za nguo yako

11/Vaa viatu kijanja
Hapa pia Kuna changamoto
*Usivaa suruali ya kitambaa na Rana
*Usivae suruali ya kuchomekea na makubanzi
*Ukipiga jeans unaweza kumatch t.shirt/shirt na rangi ya viatu
*Ukivaa suti yakupasa upige kiatu kikali ....ulikosea itakuwa sawa na Toyota Mark X yenye matairi ya Fuso !!!
1226b48d9dfc7ec250baad4f0d88ab13.jpg
560db2f0ece8249c51f54099a525b596.jpg



***Usipojua kuvaa utadharaurika***

The Bitoz
[/IMG]


!
!
Nimejifunza kitu humu. Fresh sana
 
Back
Top Bottom