Jinsi ya kupambika ukiwa na urefu chini ya futi 5.7' [ 170cm +]

Saint_Mwakyoma

JF-Expert Member
Jun 8, 2019
865
1,204
Changamoto ya utafutaji wa mavazi kwa upande wa wanaume ni kubwa kwasababu wafanya biashara wengi wanalenga soko la watu wenye urefu wa juu wastani kwasababu hata sisi tulio na urefu wa chini wastani tunaweza zipunguza izo nguo na kuzivaa kwaio wanaepekana na hasara za mara kwa mara
Aina za mikato kwa watu wa urefu tajwa tu;

1. Mashati ya mikono mirefu
Hapa kwenye mashati ya mikono mirefu ili likupendeze ni lazima liwe la kukubana kidogo [slim fit] lisiwe kubwa la kujiachia litakufanya uonekane umejaa jaa na utachukiza

2. Mashati ya mikono mifupi
Hapa ndio penyewe ukiwa na urefu tajwa mashati ya mikono mifupi yatakupendeza muda wote na likiwa slim fit yani lakukubana ila lisibane sana utachukiza

3. Vest [ nguo laini za kifuani]
Epuka kuvaa vest za rangi nyingi kwa wakati mmoja ili upendeze pendelea kuvaa vest za rangi moja plain colou ila rangi nyeupe ni the best

4. Suruali za vitambaa
Hapa kwenye suruali za vitambaa ni lazima uhakikishe hauvai suruali za kubana kamwe usivae suruali za kubana tena zikiwa za vitambaa hakikisha suruali haikubani kuhusu swala la mikunjo ya luks ni mapendeleo yako ila upigaji wa pasi uzingatiwe kamwe usivae suruali kinjiwa [ don't touch my shoes]

5. Cardet na suruali za jeans
Hapo ndipo wengi wetu tuna haribu ni kweli ukiwa na urefu tajwa kupata suruali ya dukani kwa size yako inakuwa ni kazi sometimes maana wengi wetu tunavaa namba 28, 30 ikizidi hapo inakuwaga kiuno kikubwa sasa inabaki kazi ya kupunguza izo suruali sasa hapo ndipo wengi wetu tujikuta tunapunguza vibaya na kushindwa kupata muonekano mzuri kwaio kujua vipimo vyako vya kiuno , paja na mguu inasaidia sana kwenye muktadha huu.

6. Boxer au bukta laini
Ni vyema kuvaa boxer zinazoachia ili kuupa mshipi uwezo wa misuli kurelax na kupata hewa na kupunguza msuguano wa kende hii inakufanya uwe huru na mwepesi haswa ukiwa katika shughuli zako

7. Soksi
Hapa kwenye soksi wengi wetu tunapa puuzia lakini ukiwa na urefu tajwa hapo juu soksi si kitu cha kuacha kuvaa maana kinaongeza mvuto wa muonekano wako lakini soksi zenye rangi nyingi nyingi si mzuri sio tu kwetu bali kwa mwanaume yeyote huwa hazimpendezi na pana vike visoksi vidogo vyemba mba ambavyo vinaishia kwenye visigino havifai haswa kwa kada yetu

8. T shirts na golf T shirts [ form 6]
Hapa ndio maala pakuchukulia points zote 3 kwa maana kwa urefu wetu izi nguo ndio mahala pake haswa kama vile mashati ya mikono mirefu yalivyo kwa warefu kikubwa ni kutulia na kuacha pressure za kwenda na fashion kwa kipato chako hakikisha unajua rangi yako na rangi unazoendana nazo kimuonekano sio kisa nguo kavaa flani basi ununue na uvaaji wa nguo ni jambo moja ila wapi unaenda nayo ilo pia ni swala jingine ambalo linaujazo wake

9. Vizibao na makoti ya suti
Ukishakua na urefu tajwa hapo juu automatically vizibao vitakupendeza zaidi kuliko makoti ya suti na kama utapenda zaidi makoti ya suti hakikisha sio single batani maana yatakufanya uonekane umevimba

10. Vizibao na makoti ya jeans

Hapo unaweza enda vyovyote tu lakini usivae crazy jeans coats utachekesha ila lazer jackets na hood jackets izo azichagui hazibagui

11. Upande wa kofia snap cap, golf cap, cow boy cap, round caps

Hapa ni wewe na pendeleo lako tu na jinsi unavyojiamini na wapi unaenda

12. VIATU , sandrozi
A. Viatu vya ofisini

Hapa kwenye viatu wengi wetu tunakimbilia viatu vyenye visigino virefu [ travolter] hapa ndipo tunapo haribu kabisa , ukishavaa viatu virefu automatically kiuno kitakua juu juu icho kitu kinapelekea kukupa mwendo mbaya ambao hauvutiii wewe binafsi unaweza hisi unavutia ila hauvutii kabisa kifupi vaa viatu vinavyoendana na nini umevaa juu ukiamua kuvaa nguo za ofisini na raba basi hakikisha ni kicks simple ambayo haina multiple colours yani rangi nyingi nyingi.

B. Raba na viatu vya mazoezi

Hapa ni mahala petu ukizingatia miguu yetu ni miguu ya raba kwaio tuna uwanja mpana sana ila ni wewe na pendeleo lako la kampuni yako pendea. Vans kwa upande wangu ndio my best , all star converse, addidas, reebook, nike air Jordan, supra , nk ni wewe tu

C. American boots, safari boots na Timberland varieties boots

Hapa napo pana tatizo sana wengi wenu tunapenda sana kuvaa hizi boots lakini zinatukataa ukiona haufeel nice ukivaa hizo boots ni bora uache tu maana sio lazima uvae

13. Manukato
Kwa taarifa yako manukato pia ni nguo na haswa kwa urefu wetu manukato ni kitu cha muhimu maana kinatu tambulisha kabla hatuja jitambulisha ila kikubwa epuka manukato makali sana yawe classic yanayokupa amani

14. Attitudes

Utakua umefanya kazi ya bure kama au kubali ukweli kwamba wewe si mrefu , heshimu uwepo wako popote pale unapopita au unapokaa amini hautakiwi kutretiwa kama takataka na usiwafanyie wengine hivyo shortly jikubali maana unatosha

Ili kuwezesha uzi kuendelea mbele karibu utuonyeshe muonekano wako na idea zako pia kwa watu wa urefu tajwa ili tuache kuvaa miundo inayochukiza kabisa kama unapicha au video itapendeza sana karibuni wakuu
 
Black round cap , plain white t shirt na sports kicks simple look
IMG_20220513_032929.jpg
 
Shati la mikono mirefu ka kubana [slim fit ] na plai cardet uamuzi ni wako kuchomekea au kutochomekea
c5041c4aab19c07d8ca977484ed2901b.jpg
 
Hapo ndio umependeza mkuu?
Mpaka unashauri na watu
Hakuna mtu kashauriwa hii ni mada izo ni idea za watu wengi binafsi zimenibadilisha na wewe karibu utupe idea zako na kama utapenda muonekano wako pia kua huru karibu utotoe ushamba mkuu
 
Back
Top Bottom