Darasa la kupigilia pamba kijanja

Bitoz

JF-Expert Member
Aug 27, 2015
30,823
126,549
Habari wakuu,

Nimeona na mimi nitoe darasa kidogo kuhusu mavazi sababu na mimi ni kipaumbele changu katika maisha.

1.Epuka kuvaa marangirangi
Wakati unamatch mavazi jitahidi kupunguza idadi ya rangi,rangi 3 tu zinatosha kukutoa bomba.
7af7aaaf7345a87c091b24ea071e6ea2.jpg


2. Vaa kulingana na mazingira/sehemu
Mtu mjanja anajua kubadilika kulingana na mazingira,sio kuvaa jezi la Man utd lenye jina la Wazza kwenye sherehe
b51129054b1bc8db689b2aa5aa68d038.jpg


3. Masharti ya kuchomekea;
* Marufuku kuvaa oversize/undersize
* Usivae mlegezo
* Hakikisha singlet haionekani
* Usivae mkanda mrefu
* Usivae makubanzi/sandals
* Hakikisha umemach rangi
a858110041666998af8e8cf6741da5d0.jpg


4. Kama umevaa pensi /kaptula...
* Hakikisha unavaa soksi fupi zisizoonekana
* Piga raba au makubanzi/sandals bila soksi
* Haipendezi kuchemekea
* Hakikisha miguu ni soft
b03d0102663f3a9f0cdd5a06bf43f22c.jpg


5. Usivae shati jeupe kama la mwanafunzi
Shati nyeupe ni nzuri kama unaijulia wakati unanunua hakikisha ina urembo wa aina yoyote ile au ni ya kimtindo sio kuvaa shati la shule.
0544b7f62d281aa4861bbd867323483a.jpg


6. Hakikisha una suruali nyeusi
Mwanaume yoyote yule wa kijanja anajua umuhimu wa suruali nyeusi sababu inamatch mashati ya rangi nyingi.
6c38a77ca2b76b59cd3c995e2413f2c2.jpg


7. Saa
*Kama umevaa jeans/kadet unaruhusiwa kuvaa saa ya aina yoyote
*km umevaa suti/suruali ya kitambaa epuka kuvaa saa ya mkanda wa plastic.
3ad27555edd1291d60ab6b44df9986fa.jpg


8. Miwani
Duh hapa pagumu kidogo lakini cha msingi zingatia muundo wa kichwa chako pamoja na aina ya macho uliyonayo na aina ya pamba ulizovaa pia.Sio umepiga jeans kali,kichwa kama madenge na macho kama bundi kisha unapiga miwani ndogo ya njano,ni kituko
0f2b06f16e0e5258c47c145a7bb31931.jpg
b0f81d79519fa57e12ae0bd30b68c561.jpg


9/.Vaa kofia za kijanja
Kofia pia huongeza mvuto,chagua kofia kulingana na aina ya kichwa na mavazi uliyovaa,haipendezi kuvaa suti na kapelo.Kanzu sharti ivaliwe na barakashia ndo utaeleweka la sivyo ni sawa na kuvaa dera tu
b175ffb99c2f4802d88bcf9d73e4c686.jpg


10/Mkanda
*Usivae mkanda mrefu km vile umefunga nyoka kiunoni
*Mikanda ya vitambaa au madoidoi inafaa kuvaliwa na jeans/kadeti/kaptula
*Jitahidi mkumatch rangi ya mkanda na viatu kama umevaa nguo za kuchomekea
*Zingatia upana wamkanda na rux za nguo yako
4e1f51f4448a15f1438520e6552fbc12.jpg


11/ Tupia cheni za ukweli
Mikufu ya kiume pia huongeza mvuto
* Kama umevaa nguo za kuchomekea au suti itapendeza ukivaa cheni ndogo ambayo haitokezi nje ya shati
*Kama umepiga pamba za kishua mfano T.shirt na jeans hapa tupia cheni kubwa lakini hata cheni ndogo zinakubali
760ba534702fff8e83b6705156230e0e.jpg


12/Uvaaji wa Tie
*Vaa kulingana na urefu wako
*Km wewe mwembamba inapendeza kuvaa tie nyembamba
*Jitahidi kumatch tie na rangi ya shirt/suruali
*Hakikisha tie yako imefungwa vizuri shingoni
1a615cffd7ab7b7411f7cb78e7451bac.jpg


13/T.shirt na Jeans
Wanaume wajanja wa mjini hupenda kupiga t shirt na jeans na chini kutupia raba Kali.....Vazi hili lina mvuto wa aina yake hasa limivaliwa kitaani na sehemu za mitoko km vile kwenye Club za starehe
30d2f4f404cbe492a0e5de9bc240926f.jpg


14/Vaa viatu kijanja
Hapa pia Kuna changamoto
*Usivaa suruali ya kitambaa na Raba
*Usivae suruali ya kuchomekea na makubanzi
*Ukipiga jeans unaweza kumatch t.shirt/shirt na rangi ya viatu
*Ukivaa suti yakupasa upige kiatu kikali ....ulikosea itakuwa sawa na Toyota Mark X yenye matairi ya Fuso !!!
1226b48d9dfc7ec250baad4f0d88ab13.jpg
560db2f0ece8249c51f54099a525b596.jpg



***Usipojua kuvaa utadharaurika***

The Bitoz
 
Habari wakuu
Nimeona na mimi nitoe darasa kidogo kuhusu mavazi sababu na mimi inikipaumbele changu katika maisha.... ...

1/Epuka kuvaa marangirangi
Wakati unamatch mavazi jitahidi kupunguza idadi ya rangi ,rangi 3 tu zinatosha kukutoa bomba !!!

2/Vaa kulingana na mazingira/sehemu
Mtu mjanja anajua kubadilika kulingana na mazingira....sio kuvaa jezi la Man utd lenye jina la Wazza kwenye sherehe....

3Masharti ya kuchomekea:
*marufuku kuvaa oversize
*usivae mlegezo
*hakikisha singlend haionekani
*usivae mkanda mrefu
*usivae makubanzi/sandals
*hakikisha umemach rangi

4/Km umevaa pensi /kaptula...
* hakikisha unavaa soksi fupi zisizoonekana
*Piga raba au makubanzi/sandals bila soksi
*Haipendezi kuchemekea
*Hakikisha miguu ni soft

5/Usivae shati nyeupe km la mwanafunzi
Shati nyeupe ni nzuri km unaijulia...wakati unanunua hakikisha ina urembo wa aina yoyote ile au ni ya kimtindo...sio kuvaa shati la shule !!!

6/Hakikisha una suruali nyeusi
Mwanaume yoyote yule wa kijanja anajua umuhimu wa suruali nyeusi sababu inamatch mashati ya rangi nyingi

7/Saa
Km umevaa jeans/kadet unaruhusiwa kuvaa saa ya aina yoyote...km umevaa suti/suruali ya kitambaa epuka kuvaa saa ya mkanda wa plastic

Mwanamitindo wa Uswaz
The Bitoz
Utakuta mtu kapiga suti yake na mkononi ana Casio G-Shock.
 
Back
Top Bottom