Haber Faraday
Member
- Jul 3, 2017
- 97
- 182
- Thread starter
- #141
LABDA LEO NIANDIKIE HAPA JUU CHONDECHONDE UZI NI MREFU SOMA UKIWA NA ENERGY YA KUTOSHA LAKINI KIKUBWA USI-QUOTE.
SOMO LA PILI SEHEMU YA TANO [C] LESSON TWO PART FIVE [C] (Mwendelezo wa hitimisho).
Baada ya mapumziko marefu karibu tena darasani, uzidi kujifunza. Leo tutaendelea na njia yetu ya tatu yenye kichwa WASAMEHE WANAOKUZUNGUKA, somo lililopita tuliishia sehemu iliyosema baada ya hatua ya kwanza ya kukabiliana na watu wanaokuzunguka wanaokuletea matokeo HASI hatua hiyo tuliyosema ni kuandika FUNZO ulilolipata baada ya kutokea kwa tukio hilo” mwalimu aliahidi kuja kutufundsha hatua inayofuata ambapo alisema, ni kufanya kitu cha kisaikolojia ambacho mtenda kitamsumbua sana na huku hamna kisasi. Twendelee.....
Mwalimu anakunywa glass ya maji kisha anacheka kidogo na kusema “hakuna kazi ambayo ingekuwa inachosha na kuboa kama kula na kunywa kama Mungu asingeumba kitendo hicho kuwa cha starehe” mwalimu anaona kwanii Mungu hakukiumbia starehe kitendo cha kusoma watu wengi wangebadilika na jamii kiujumla maana hamna mabadiliko ya kweli kama mabadiliko ya kichwani kwenye ubongo tutakuwa tunapiga kelele tu kutaka kubadili tabia za watu pasipokuanza na kichwani. “human can alter their lives only by altering their attitudes of minds” by William James.
Turudi kwenye somo bado tupo kwenye uhusika wa kiumbo, kama umepasahau hapo rejea somo lililopita ambapo tunaenda kupambana na mtenda kwa kutumia njia ya kisaikoloji kama hatua ya pili, lakini kabla ya kuzama hapo kwa kina kabisa mwalimu anataka kukuweka sawa juu ya hawa wahusika wanaokuzunguka, ni hivi tunaongelea wahusika wanaokuzunguka unaoshirikiana nao ambao mlikuwa mnaishi kwa amani kabla ya kukuletea matokeo HASI hivyo usichanganye na AJALI, mfano wa ajali ni kama jambazi huyo si mshirika wako labda mwizi wa mtaani tofauti na vile atakavyokuibia mwanao ndani ambae huwezi mfunga jela.
Hao watu wanaoleta matukio hasi tunaowaita ajali hawahusiki katika njia hii ya kupambana kwa kutumia saikolojia hawa wanahitaji NGUVU lakini si ilimradi nguvu kuna somo tutakuja jifunza linaitwa “uses of smartness power against evil” hivyo watu tunaopambana nao walengwa haswa ni wale tunaoshirikiana nao katika shughuli za kutuingizia kipato, au shughuli yoyote inayotupatia mahitaji muhimu yanayofanya tuzidi kuamka tena na tena kama kilimo, biashara na kadhalika.
Mwalimu ataenda kutupa story mbili, moja ilimtokea mwenyewe miaka hiyo angali kijana na nyingine ilitokea kwa jirani yake. Umri wa Mwalimu umemfanya ayashuhudie mengi. Story ya kwanza inayomuhusu mwalimu mwenyewe kipindi angali kijana inaanza hivi.
Kipindi mwalimu FARADAY nipo kidato cha tano shule ya bweni miaka hiyo, nilitoroka na kwenda mjini kusafisha macho kidogo, kutokana na shule yenyewe ilikuwa mbali na mji kidogo, basi huyu FARADAY akiendelea kupuyanga na mtaa huku na huku, huku na huku mara secondmaster wa shule huyu tukagongana ana kwa ana, ikawa hamna namna tena ikabidi kusarenda na kizuri zaidi tulikuwa na mwenzangu basi ilibidi tusubiri kiama chetu. Alichokifanya yule second master ni kutubeba kwenye pikipiki yake akaturudisha shule na tulipofika shule akaturuhusu tuende mabwenini bila kuongea chochote.
Kiichofwata “kuwa makini hapa mwanadarasa” akili yangu mimi Faraday na mwenzangu tulijua kesho mstarini lazima makalio yetu yachezee bakora kama ilivyokuwa desturi ya mwalimu huyo, kamwili ka mwalimu Faraday kwa wakati huo hata avae suruali nne kwa wakati mmoja huwezi kuona tofauti basi mimi na mwenzangu tukatupia suruali aina ya jinsi ndani tukawa tumenenepa miguuni tu basi kama ilivoada siku ikafika mwalimuakaja mstarini alichokifanya ni alitangaza tu matangazo mengine akaenda zake. Basi tukatoka wanyonge tukisubiri kesho tena tukajua leo pengine anawahi vikao siku ya pili ikawadia alikuwa amesafiri kwa siku mbili, tukapumua kidogo huku tukijua akirudi anaanza na sisi lakini alivyorudi akatoa matangazo machache akaenda zake tukajua labda ni kwasababu ya uchovu wa safari siku iliyofwata tukajitupia suruali za kutosha lakini hakuja kabisa basi ikawa hivyo tuliteseka kwa wiki mbili mwisho tukakata tamaa kwamba basi tusubiri pale siku akiamua tutaadhibiwa.
Yule mwalimu hakutupiga wala kutuuliza mpaka tunahitimu shule lakini tuliishi kwa muda mrefu tukimkwepa kwa kuhofia akituona tu atakumbuka, kwamba labda alikuwa amesahau, ilifikia mahali tukataka twende tukajipeleke wenyewe tumuombe atuadhibu ili yaishe lakini tukasita.
Tunarudi kwenye somo letu, kumbe mwalimu alikuwa ametusamehe lakini akawa ametupa Adhabu iliyotutesa kwa muda mrefu, alijua akili ndiyo iliyotutuma tutoroke hivyo akaamua kukuiadhibu akili yenyewe. Hatukurudia kutoroka tena na hatukuthubutu kumuudhi tena yule mwalimu kwa kuhofia angekumbushia na siku ile. Hivyo yeye alisamehe akafuta kinyongo ndani mwake akatuadhibu kisaikolojia tukapata adhabu ya muda mrefu na hatukuwa kujenga kisasi chochote juu ya mwalimu na pia wakati anatupakia kwenye pikpiki alituuliza tumefwata kununua nini tukamuonesha kuwa tuliishiwa nguo za ndani baada ya siku kadhaa duka letu la shule wakawa wanauza makufuli ya kiume, hivyo mwalimu alipata funzo kwanza lililotokana na kutoroka kwetu. Naamini kupitia story hiyo mwanadarasa umeanza kupata mwanga.
Hivyo tukio lolote linapotokea lina kitu cha kujifunza. Mwalimu angependa kutoa story ya pili ya jirani yake aliyechepukwa na mkewe lakini makala itakuwa ndefu sana na inatakiwa leo ikamilike sehemu ya tano na uwe mwsho wa somo la pili. Tutatumia story hiyo moja kama mfano.
Chanzo cha matukio mengi kutoka kwa watu wanaotuzunguka ni tabia lakini chanzo cha tabia huwa ni ndani tabia inazilishwa na vitu vitatu, matamanio, hisia na maarifa kuna huyu jamaa plato anasema “human behaviour flows from three sources, desire, emotions and knowledge” hivyo kuhangaika kuzuia tabia ya mtu ni kutwanga maji kwenye kinu, inabidi kuzuia chanzo cha tabia, leo hii ndio maana makosa yanajirudia kwasababu watu wanazuia tabia na si chanzo cha tabia. Hamna mtoto unaemzaa akawa mwizi toka tumboni, hamna mfanyakazi aliyesomea kitu fulani alisomea aje afanye uzembe hapana.
Leo hii inawezekana umeajiri mpaka sasa idadi inafika wafanyakazi wanne kwenye kitengo kimoja wale watatu wote wa mwanzo umewafukuza kwa kukuletea matokeo hasi bado haujafanya suluhisho hata huyu aliyepo atafanya nae utamfukuza, watu wamekuwa wakiwafumania wenza wao na kutoa talaka lakini wanakuta mwanamke mpya nae kafanya yaleyale utafukuza mpaka uzeeni hahaha somo la leo linampa raha sana mwalimu.
Jinsi ya kutumia hii njia isiyoonekana katika kupambana na wahusika, mwalimu anakwambia usipambane na wahusika kwa njia zilizozoeleka kwasababu si sahihi na kama zingekuwa sahihi basi makosa yasingejirudia. Kupambana unakoenda kukufanya hapa ni kupambana na ubongo wa mtenda ambapo utaenda kumpa mshtuko mkubwa ndani yake. Mwalimu anakwambia kwa kosa lolote ambalo umefanyiwa na mtu anaekuzunguka kitu cha kwanza usifanye kile ambacho yeye mtenda anategemea utamfanyia kwa mfano Leo mfanyakazi wako kasababisha hasara yeye tayari anakuwa amekwisha jihukumu kuwa hapa nafukuzwa kazi hivyo hata ukimfukuza kazi hakitakuwa kitu kigeni nafsini mwake.
Leo hii mifugo ya mtu ikila shambani kwako ukaipeleka mifugo hiyo ofisi ya kijiji na mwenye mifugo akalipishwa faini halitakuwa jambo la kumshtua, Leo hii ukimfumania mwenza wako kisha ukamtimua au ukampa talaka ni kitu ambacho alijua kitatokea endapo utagundua. Hivyo unapopambana na muhusika huyo kwa njia zilizozoeleka unakuwa unatekeleza kitu ambacho sauti yake ilimkataza lakini kwasababu aliipuuza hivyo hataweza kubadili tabia kwasababu baada ya kuipuuza sauti yake ya ndani alivyofikiria matokeo hasi ya kile alichoenda kukifanya alikiundia njia za kukabiliana na hilo.
Hivyo pale muhusika anapokosea fanya maamuzi ambayo hakuyategemea utaenda kuathiri mfumo wake wa ndani na kumpa adhabu ya muda mrefu. Kwa mfano mfanyakazi anapokosea na huku moyoni akiwa anajua kazi hamna tena lakini akakuta haujamfukuza huku moyoni mwako ukiwa umesamehe na hauna kinyongo, ukachukua sababu ya uzembe wake kama funzo na ukawa unaziandaa njia za kuziba mwanya wa uzembe huo bila kuongea chochote kwa huyo aliyesababisha uzembe ukamuacha aendelee na kazi kila siku akija asubuhi anategemea akute barua ya kumfukazi kazi kwa sekretari lakini anakuta sivyo. Hakuna mfanyakazi atakaekuwa makini kama huyo katika kufanya kazi.
Kwasababu hata ikimfukuza kazi haitafanya ile hasara ilipwe, Leo hii huyu aliyelisha mifugo yako ukaichukua na kuipeleka kwa mwenyewe na sio ofisi ya kijiji bila kuongea chochote, mwenye mifugo anaweza akakesha usiku akiwaza nini utakachoenda kukifanya akisikia mfugo unaguna tayari anahisi labda mifugo Itakufa hivyo hiyo hali itamsumbua sana tofauti na unavyofikiri. Na hauwezi kufa njaa utakachotakiwa kukifanya ni njia za kufanya uweze kupata mazao kwa njia nyingine kama yalikuwa ya chakula na hautakufa njaa nature itafanya kazi yake. Kwasababu hata ukilipwa faini mazao hayataota na wala haiwezi kuwa sawa na jasho ulilolimwaga.
Hahaha pagumu hapo lakini ndio ukweli wenyewe unakuwa tofauti kabisa na uhalisia. Lakini njia hii inafanya kazi kwa mtu mwenye akili timamu sasa sijui kama unaweza kuajiri mtu ambae hana utimamu kichwani.
Kwanini huyu unaemuona kama adui Kwasababu amekusababishia matokeo hasi utumie hii njia isiyoonekana ambayo inakutaka uendelee na huyo unaemuona ndo adui wako kwasasa Kwasababu; ngoja upate msaada wa sheria hapa moja kati ya sheria za nguvu/uwezo sheria namba mbili (laws of power) inasema “be wary of friends they will betray you more quickly, for they are easily aroused to eny. They also become spoiled and aroused to eny, they also become spoiled and tyrannical. But hire a former enemy and he will be more loyal than a friend because he has more to prove. In fact you have more to fear from friends than enemy. And if you have no enemies find a way to make them”.
Tukimalizia uhusika wa pili wa kihisia hapa ni pale mtu anakuchukia kutokana na mafanikio yako, yawe ni ya kikazi au yakielimu furahi kwasababu yeye ndiye chachu ya wewe kufanya vizuri na hata akikukosoa amini kuwa ni kweli kwa kuwa hatakuwa mnafiki. Hivyo huna budi kusamehe na kufurahia uwepo wake mwanafilosofia huyu anaitwa Voltaire anasema “The best is the enemy of good”.
Jitahidi uweze kusoma na kuelewa huo ndo mwisho wa som la pili.
Tuonane katika sehemu zingine kwa ajili ya kumalizia utangulizi bado haujachelewa kutuma namba yako.

<H.FARADAY>(0625934471).