Ni jumatatu nyingine tena hii, amani kwenu wanadarasa popote mlipo, wengine mkiendelea kuwepo na wengine kuishi na wale wengine ambao mko hai.
Leo mwalimu amekuja na suala jipya kidogo. Umsikilize kwa makini, tayari mpaka sasa ameweka masomo mawili yenye jumla ya sehemu 12 (twelve sub-lessons). Kwa yule anaesoma kwa kuzingatia na si kutaka kuwahi kumaliza amejifunza mengi na anaendelea kujifunza tena na tena kwa kuyarudia kusoma. Kama mwalimu alivyosema huo ni utangulizi tu na bado somo moja la tatu lenye sehemu nne (four sub-lessons) ili kukamilisha sehemu ya utangulizi na sehemu hizo tayari mwalimu ameshamaliza kuziandaa. Alikuwa anafwatilia utaratibu wa kutoa nakala (hardcopy) utakaokuwa na huo utangulizi ukiwa umekamilika ukiwa na masomo yote na baadhi ya sehemu (sub-lessons) za somo la kwanza na la pili zikiwa zimehaririwa (edit).
Mwalimu alisema hataendelea kutoa mtiririko wa masomo unaofwatana hapa kama alivyotoa baadhi ya sehemu kadhaa za masomo yaliyopita. Ni pamoja na huo mwendelezo wa masomo ya utangulizi yaliyobaki hautaonekana hapa, lakini kuanzia kesho mwalimu ataanza kuutoa huo mwendelezo kwenye group na bado una nafasi ya kujiunga. Hapa darasani atakuja kurudi akikamilisha somo lolote litakalogusa nyanja yoyote atakayoanza nayo lakini Mwalimu yupo hapa kujibu maswali yoyote kuhusu masomo aliyoyatoa na kutoa ufafanuzi wowote atakapohitajika.
Tukiacha yote hayo kubwa ni hili Mwalimu anahitaji wanadarasa baadhi watakaokuwa wawakilishi katika sehemu mbalimbali hapa nchini kwa ajili ya kusambaza nakala za Mwalimu. Mwalimu anahitaji kila mkoa watu watatu na ni vzuri wawe wilaya tofauti.
Sifa za hao mabalozi (hapa ndo kasheshe mwalimu sijui aweke ada kabisa ya kumsajili huyo balozi maana huyu binadamu).
1. Uwe mwaminifu.
Mwalimu anaposema mwaminifu anamaanisha, balozi usiye na tamaa ya pesa ambae utakuwa mwaminifu kuisambaza hiyo nakala bila kuzidisha kiasi atakachopanga Mwalimu.
•Iko hivi kutaka kuibadilisha jamii tuliyonayo, tufanyike msaada kwa ajili ya matunda ya vizazi vijavyo yatupasa kujitolea na ndio maana Mwalimu ameamua kutoa masomo haya BURE (free of charge) hamna hela itakayofikia thamani ya maarifa (knowledge) ambayo Mwalimu anaitoa hivyo hata nakala zake zitauzwa gharama iliyotumika kuiandaa nakala hiyo.
•usije ukaniambia Mwalimu kitu nilichokiona kwenye ubongo wangu ni kusambaza nakala zako hahaha mwalimu hataki kusikia kitu hicho.
•mwalimu umri umeenda hawezi kuzunguka Tanzania yote hivyo anataka uwe balozi hapo ulipo kikubwa maarifa haya yawafikie wengi hata wale walio ndani vijijini.
Hiyo ni sifa kubwa ya balozi zingine mwalimu atazipata atakapomfanyia usahili.
Hivyo tumia namba ya mwalimu ili kupata utaratibu wote.
Kesho tutaendelea na mwendelezo lakini upande wa pili lakini nitakuwepo hapa kutoa ufafanuzi juu ya masomo yote yaliyopita na maswali mengine.
<H.Faraday> 《0625934471》.
Sent using
Jamii Forums mobile app