Darasa: Chakula cha akili (Mental food)

Darasa: Chakula cha akili (Mental food)

Pamoja sana mwl

brain is like parachute it work when u open
 
Sehemu ya tatu.

Kengele imeshagongwa tayari kwa kipindi kuanza ni imani ya mwalimu kuwa mwanadarasa yu buheri wa afya. Katika sehemu ya tatu ya hili somo letu la kwanza tutaenda kuangalia kitu kinachoitwa;

NINI MAANA YA NENO MAISHA? (what does the word life mean?).

Lakini kabla ya kulianza somo hili tujikumbushe kidogo kuhusu ni nini mwalimu alitufundisha kipindi kilichopita, mwalimu alitupa utangulizi wa somo letu (introduction),pia mwalimu katika sehemu ya kwanza akatuuliza kuwa sisi ni akina nani tukapata kutambua kuwa msingi mkubwa unaotufanya tujione sisi ni viumbe hai vinavyoitwa binadamu ni kuwa na uwezo wa kumudu kitendo kinachoitwa (Reasoning).

Mwalimu hakuishia hapo kwenye sehemu ya pili akatuuliza tena kuwa kwanini tuko hivi? Ndipo alipotupeleka kwenye vitu vinavyoitwa mifumo ya maisha (systems of life), na mapinduzi ya kimfumo (system revolution). Kwa kujikumbusha hapo tutakuwa tunaenda na mtiririko mzuri kama kusudio la mwalimu linavyotaka, kama haukuelewa kitu usisite kusoma upya kwenye post ya kwanza maana hatutakuwa na tunzo ya mtu aliyewahi kumaliza kusoma bali utatunukiwa tunzo na moyo+akili yako kwa kuelewa Somo.

Cha kujikumbusha cha mwisho ni mwalimu aliweka baadhi ya vipande vya masomo kama kiporo (pending) ambayo

moja (1) litaongelewa katika somo la leo na la pili (2) litaongelewa katika masomo ya mbeleni, vipande hivyo ni

1. Tofauti ya kuwepo na kuishi (Existing and Living).
2. Mifumo na misingi, jinsi ya kutoka au jinsi ya kuikabili kwa kuirekebisha (systems modification).

Baada ya kujikumbusha hayo mwalimu anatutaka tulianze hili somo letu ambalo ni sehemu ya tatu katika somo la kwanza. Somo hili lenye kichwa;

nini maana ya neno maisha?. Mwanadarasa atajibu tu maisha ni kitendo cha kuwepo hai hapa duniani kabla mtu hajafukiwa na udongo, MWALIMU anafurahi kuona mwanadarasa hayuko mbali sana na maana halisi ya maisha, Mwalimu anamtaka mwanadarasa awe makini kusikiliza maana ya neno maisha na maneno yanayolizunguka neno maisha ambayo yanaonekana kuwa sawa LAKINI si sawa kuna utofauti ndani yake, ni maneno yapi hayo na utofauti wake nini twende tukayaangalie.
Maisha (life), tukianza na muhusika mkuu ambae ni neno maisha mwalimu anatuambia maisha ni hali inayowatofautisha wanyama (ambapo hapa binadamu yupo ndani yake) na mimea kutoka kwenye viumbe visivyo hai (organic matters) hali hii ikihusisha kitendo cha kuweza kukua (growth), kujizalisha au kuzaliana (reproduction), uwezo wa kufanya kazi au vitendo mbalimbali (functional activity) na kuweza kupata mabadiliko ndani au nje ya mwili kukielekea kifo (continual change preceding death).

Mwalimu anatuambia kuwa pamoja na kuwepo kwa maana nyingi lakini hii ni sahihi zaidi. LAKINI mwalimu kwa kujua wanadarasa ni wavivu wa kutaka kuishika na kuijua maana ya maisha yenye maelezo mengi anaamua kuwarahisishia kuwa mtu akikuuliza nini maana ya maisha mwambie ni hali ya uwepo wa binadamu au mnyama (existance of an individual human being or animal) hawa ndo wahusika wakuu katika somo letu hivyo weka mbali kidogo mimea.

Baada ya kupata tafsiri ya neno maisha twende tukaangalie maneno yanayolizunguka neno maisha pamoja na utofauti wake, Tukianza na maneno haya KUWEPO na KUISHI (Existing and Living) ambayo ni kiporo chetu cha kwanza yana maana au uhusiano gani mwalimu anasema Existing (kuwepo) ni pale mlengwa wetu (mnyama-binadamu) ambapo anakumbana na vitendo mahususi au muhimu vinavyofanywa au kufanyika ili kumuwezesha kuwa hai au mzima (doing necessary to stay alive). Vitendo hivyo mahususi au muhimu ni kama

kula (Eating), kupumua (breathing), kulala (sleeping), usafi au usalama wa afya (hygiene). Hapa sasa wengi wa wanadarasa ndipo walipo kuhakikisha wanaendelea kuliona jua, Reasoning inafanyika ili aweze kuwa hai tu au kuwa mzima ubongo utasukuma akili yake ilete maarifa ya kuweza kula, kuweza kuwa na pakulala.

Mwalimu anawaangalia wanadarasa anaamua kuwashangaza kidogo, unajua ubongo wako unasukuma akili ya asilimia 2.6% katika kuwaza kula, asilimia 3.4% kuwaza kuwa na pakulala na asilimia 15% zikikamilishwa na vitendo vingine vinavyokamilisha Existing, asilimia 80% badala ya kuzipeleka zinakotakiwa ziende zinaendelea kupunga upepo kichwani, mwalimu anaona kweli vichwa vya wanadarasa wengine ni sehemu ya kuhifadhia ubongo, mwalimu anatoa mfano kidogo mtu akisema piga push-up 10, ukifika ya 8 mpaka ya 9 utakuwa umechoka, vivyo hivyo akisema piga push-up 20 ukifika ya 18-19 mikono itakuwa inatetemeka KWANINI? Kuna kitu kinaitwa "set of mind".

Mwalimu anatutaka tuandike pembeni ya daftari kiporo hiki kuwa tutakuja kuangalia kitu kinachoitwa set of mind pia tutaangalia kitu kinachoitwa asilimia 80% za ubongo za nini? Zina kazi gani na zitumikeje.Living (ishi) hapa ndipo watoto wa kisasa wanaita kujiongeza, ambapo inamaanisha kwamba ni ubora (savour) wa kila dakika unayokuwepo (exist), "to savour every moment of your existence" vitendo vinavyofanyika hapa ni kuweza kuona (taking in the sights), kuweza kunusa (taking in the smells) na kuyaweza mazingira yanayokuzunguka (taking in the environment around you).

Mwalimu anaona hapa panahitaji maelezo zaidi anaamua kuelezea kwa kina kidogo kuwa kwanza ni lazima ujue kuwa living ipo ndani ya existing ila ni kujiongeza au kujiboresha zaidi kutoka kuishia kwenye existing tu kisha kufika kwenye hatua nyingine ambayo ni living hivyo wanadarasa 100% wana exist wakati asilimia chache wako kwenye living, huku kujiongeza au kujiboresha (savour= quality by taste or/and smell) tunakoongelea hapa kwa kila dakika unayokuwepo (exist) unatokana na uwezo unaofanywa na ubongo wako kwa akili yako huo uwezo uliofichika ndani ya vitendo vinavyofanywa na milango ya fahamu.

Tunaposema uwezo wa kuona (Taking in the sights) kuweza kuona vitu ambavyo haviwezi kuonwa na mtu mwingine kwahiyo si kwa macho haya nje bali kwa macho ya ubongo. Hivyo kwa kuwa kila binadamu ameumbwa tofauti ina maana kwamba kila binadamu anacho cha kwake cha kukiona tofauti na mwingine kwasababu hata ubongo wa mapacha haufanani, mwalimu anaamua kuuliza wanadarasa nani ambae ameshakiona cha kwake? Na je huyo aliyekiona cha kwake anakifanyia kazi? Au unafanya cha mwenzako?

Hivyo hii ni homework yako ya kwanza leo kukiona cha kwako na kama ulishakiona je unakifanyia kazi na kama unakifanyia kazi ni unakifanyia kwa asilimia ngapi?.

Mwalimu anamuona mwanadarasa yule umri umekwenda kidogo anajiona hata akikiona saizi hawezi kukifanyia kazi muda umeenda anasikitika sana LAKINI anasahau kuwa ana watoto ana nduguze ambao umri uko mahala pake kukiona hicho kilichoumbwa kwa ajili yake, hivyo mwalimu anakumbusha tena hili darasa ni kwa manufaa ya kizazi hiki na kijacho, mwalimu anacheka kidogo kuona kwamba hiki alichokiona cha kukuambia mwanadarasa haya kitatumika vizazi na vizazi hata akifukiwa leo chini ya udongo moyo wake una amani kwa kutua mzigo mzito kwa faida ya wewe mwanadarasa na yeyote atakae yasikia haya ni wajibu wako kuwafahamisha wanaokuzunguka waweze kuona vilivyopo ndani ya ubongo wao maana wana macho lakini hawaoni wanasubiri neno la kwamba ONA.

Sio hivyo tu pia Tunaposema uwezo wa kunusa (smell) hapa mwalimu anamaanisha kuweza kunusa harufu ambayo iko mbali ambayo mpaka wengine wanakuja kuinusa wewe ulishainusa mile tano kabla yao. Hapa kwenye kuyaweza mazingira mazingira yanayokuzunguka mwalimu anamaanisha nini, mwalimu anaamini kila mwanadarasa ana mazingira tofauti toka anavyoamka kutembea mpaka anapofika darasani mwalimu anauliza je mazingira uliyonayo yanakutumia au wewe unayatumia? Je unaona nini kwenye mazingira ambacho wengine hawakioni au unanusa nini katika mazingira uliyopo ambacho wengine wameshndwa kunusa? AU WEWE NI SEHEMU AU UNATUMIKA KAMA MAZINGIRA YA MWENZAKO? Hiyo ni homework ya pili kwako wewe mwana darasa katika somo letu la leo.

Mwalimu anaendelea kusema tunapozungumzia ubora kwa njia ya ladha (taste) mwalimu anamaanisha ni ile ladha ya maisha unayoipata wewe kama wewe katika maisha yako je inapaswa kuendelea nayo na je ni chachu, chungu au tamu? Jibu analo mwanadarasa maana akifungua tu kitabu chake kinachoitwa experience anaikuta.

Lakini siyo maneno hayo tu yanayolizunguka neno maisha kuna neno lingine linaloitwa hai au uzima (being alive) lina tofauti sana na neno ishi (living) tunapozungumzia neno hai (alive) ni pale mtu anapokuwa zaidi ya kuishi, mtu ambae amejifunza jinsi ya kuishi (those who have actually learned how to truly live), watu ambao wanafanya zaidi ya kupumua (those who do more than just breath in and out) huyu mtu tunamuita yuko alive ana uhai wa akili, amekiona alichokuja nacho duniani na ana kifanyia kazi kwahiyo alive inakamilisha kitendo cha living "uhai unakamilisha ishi".

Mwalimu anasema wale ambao walikiona kitu chao na kukifanyia kazi ndio walio na ufaulu wa angalau wa maisha na kwa macho haya ya nje hicho atakachokiona mtu na kukifanya na kisha kikajulikana ndipo hapo washuhudiaji watakitamka kuwa kile ni kipaji, ufaulu wa asilimia kadhaa wa maisha uko ndani ya hiki kinachoonekana kipaji, mwalimu anawakazia macho wanadarasa kisha anauliza kama wanawajua watu waliotumia kitu cha pekee walichoumbwa nacho na kama kweli wanamafanikio, wale walioitumia sauti kwa kuiona ni kitu cha pekee na hamna mwingine aliye nacho kama cha kwake na akatumia sauti yake na kama je imempa mafanikio, yule aliyoona miguu yake si kwa ajili ya kutembelea tu kama wengine watjmiavyo yeye akaenda mbali zaidi na kama je amepata mafanikio!!??

Mwalimu anasikitika kwa kuona pamoja na yeye kuhangaika na chemistry yake katika level ya chini mpaka ya juu ya elimu akiupa ubongo ushike kile kilichoonwa na mwenzie, mwalimu anakuwa mnyonge kabisa kwa kuona hajafanikiwa hata robo kuyafaulu maisha yake. Mwalimu anakutaka upaweke akilini hapa maana tutapaongelea kwa kina katika masomo yajayo yatakayohusu ELIMU katika maisha ambapo mwalimu atatujulisha mengi.

Lakini pia mwalimu aligusia katika somo lilopita kuwa tutajua kwanini mzungu ana jukumu moja na huku wewe mwanadarasa una majukumu matatu katika maisha ni yapi hayo kwa kugusia tu ni kwamba mzungu mfumo alionao tayari ni mfumo unaokiwezesha kila kizazi kinachokuja "huyu aliyepo ni kwa ajili ya yule ajae" hivo huyu aliyepo jukumu lake ni kuandaa kwa ajili ya kizazi kingine kwahiyo nguvu yote itaelekezwa kwa ajili ya kizazi kijacho kwasababu yeye alikwisha andaliwa na kizazi kilichopita lakini huyu mwenye jukumu moja ndiye anaetumia zile 80% za ubongo.

Huku upande wa pili mwanadarasa majukumu yake yakiwa matatu yaani wewe mwanadarasa hapo ulipo jukumu lako la kwanza ni kusaidia kizazi kilichopita hahaha na (na ole wako usisaidie uachiwe laana) jukumu la pili ni kuhakikisha wewe unajimudu au umudu familia yako au kwa lugha nyingine ndo ujiandalie maana haukuandaliwa hahaha (ole wako ushindwe kujimudu ukimbiwe na mke, uchukiwe na ndugu na uwe kero kwa ajili ya shida zako) jukumu la mwisho ukiandalie kizazi chako kijacho watoto wako hahaha (ole wako ushindwe watoto wako waje wauane na kukuombea ufe haraka ili warithi kakibanda kako. Cha ajabu huyu mwanadarasa ndo anatumia 20% ya ubongo wake.

Hivyo tutakuja kupaangalia kwa upana hapa katika mfululizo wa masomo yetu.

H.FARADAY (0625934471).
 
Kwa sisi ambao tupo kwenye economic struggle bado tuna safari ndefu

great thinker
 
Neno la leo katika kuianza week yetu.

"Pale unapoona pana msaada basi pang'ang'anie mpaka uupate ule msaada maana pakiondoka hapatarudi tena kwasababu palikuja kwa ajili ya msaada, lakini katika karne zote zilizopita na zijazo hakutakuwa na msaada mkubwa utakaopata kutoka kwa binadamu mwenzio zaidi ya yule anaekupa msaada wa ONA".

BY H.FARADAY

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Neno la leo katika kuianza week yetu.

"Pale unapoona pana msaada basi pang'ang'anie mpaka uupate ule msaada maana pakiondoka hapatarudi tena kwasababu palikuja kwa ajili ya msaada, lakini katika karne zote zilizopita na zijazo hakutakuwa na msaada mkubwa utakaopata kutoka kwa binadamu mwenzio zaidi ya yule anaekupa msaada wa ONA".

BY H.FARADAY

Sent using Jamii Forums mobile app

Asante kwa ukumbusho, lakini ni vyema kutafakari kwa kina kuhusu huo msaada, maana ipo misaada ambayo mbele ya safari ikakughalimu...
 
LESSON;USOMAJI VITABU/NUKUU ZA WATU AU WAJASIRIAMALI WALIOFANIKIWA BADO HAIJAWA SULUHISHO LA HALI YA MTANZANIA.

Karibu darasani kwa mara nyingine tena upate kula chakula cha akili, chakula cha leo huenda kikakuacha mdomo wazi lakini hamna namna ndo ukombozi wa kifikra unavyowadia. Mwalimu ana imani kuwa akiweka maelezo yote ya somo hili kwenye makala moja basi huenda mwanadarasa akafika mwisho kisha akasahau alikotoka, hivyo somo litaendelea na part B yake.

Kitu cha kwanza ambacho mwalimu anataka mwanadarasa ukijue ni kwamba masomo ya mwalimu hayafundishi kuhusu ujasiriamali japo ndani ya masomo ya mwalimu unaweza ukajifunza kuhusu ujasiriamali kwasababu nayo ni moja ya nyanja katika maisha.

Mwalimu anagusa mfumo mzima wa maisha ambao ndio chanzo cha hali ya mtanzania ama mwafrika. Unaweza ukasikia wanasiasa wakisema chama fulani kina mfumo mbaya wa uongozaji, naam maisha nayo yana mfumo wake jinsi ya kuyaongoza. Mifumo ya maisha ipo mingi lakini asilimia 99 ya mifumo yote unayohubiriwa ni vipande vya mfumo mmoja mkuu, ambao ni mfumo wa maisha wa nje, kama ujasiriamali, kanuni mbalimbali za ufanyaji biashara n.k. Lakini mfumo wa pili ambao ndio kiini ni mfumo wa ndani ambao ndio haswa mwalimu anafundisha, ni mfumo unaoudhibiti ule wa nje.

Kosa kubwa ni kwamba kila leo unahubiriwa mfumo wa nje kutokana na upofu tulionao kwa kushindwa kuuona huo wa ndani matokeo yake tunajikuta bado tuna hali ngumu. Kung’ang’ana na mfumo wa nje na kuuacha ule wa ndani ni sawa na kumpigia mbuzi gitaa, ndio maana kufundishwa kuhusu ujasiriamali watu wamehudhuria semina za kila aina, kuhusu kuzijua kanuni za kufanya biashara watu wamesoma kila aina ya vitabu mpaka wanachanganyikiwa wenyewe, sio hivyo tu bali pia watu wamesoma elimu yetu ya hapa Tanzania tokea awali mpaka wamepata Uprofesa lakini bado inaonekana haina msaada, watu wamesoma vitabu vingi vinavyohusu uongozi (how to be a good leader) wamesoma mstari kwa mstari lakini bado hali ya uongozi wa watu mbalimbali bado ni tatizo kwasababu gani, ni kwasababu tunang’ang’ana na mfumo matokeo na si mfumo chanzo.

Kabla ya kwenda kukiangalia kichwa cha somo letu, twende tukaangalie kidogo au japo kwa ufupi mambo au elimu inayohusu ama kugusa mfumo wa ndani. Hapa duniani kuna vitu hivi viwili Dini na Imani pamoja na kuwa ni vitu viwili tofauti lakini ni vitu vinavyoshirikiana, kwa lugha rahisi hakuna Dini bila imani japo kuna Imani pasipo dini.

Hatutaenda kujikita zaidi huko kwasababu kuna somo linalohusu “uhusiano kati ya imani, dini na maisha yetu” hilo ndilo ambalo limezungumzia kwa kina kuyahusu hayo. Lakini leo mwalimu anaenda kutufunza nini kwa kuyaongelea hayo maneno mawili dini na imani na uhusiano wake na mfumo wa ndani? iko hivi; Wengi wa wanadarasa wanachojua ni kwamba wana dini ya aina moja au hawana kabisa, utamsikia huyu akisema mimi ni mkristo mwingine atasema mimi ni muislamu na dini zingine unazozijua, lakini kuna mwingine atasema mimi si mkristo wala muislamu huyu atajiona hana dini.

Hapo tumeangalia kuhusu dini lakini twende tukaangalie imani, wanadarasa wote wana imani moja haijalishi aina ya dini uliyonayo au hata hauna dini lakini wana imani ambayo ni kuamini katika uumbaji. Hapa kila mtu ataamini vile anavyoona yeye japo asilimia kubwa wanaamini kwamba Mungu ndiye muumbaji, japo wapo pia ambao wanaamini katika uumbaji lakini wana amini kuwa siyo Mungu ambae ndo muumbaji, wanamjua wenyewe muumbaji wao. Sasa basi baada ya imani hii ya kuumbwa kwako kuna imani inayofwata hapo, hapa ndo penye upofu, mwalimu anakwambia imani hii inaitwa imani ya upili.

Kabla ya kujua ni imani gani mwalimu anakuambatanishia na dini yake, dini ya imani hii inaitwa awali. Kwanini iitwe imani ya upili halafu iwe na dini ya awali? Mwalimu anakuomba uchukue break fupi kama kichwa kimeanza kupoteza mwelekeo lakini yote kwa yote huu ndio ukweli whether you understand or not.

Kabla ya kuelezea hiyo dini ya awali na imani ya upili na kwamba kwanini viitwe upili na awali, twende tukapate jinsi inavyounda mfumo wa ndani, hapa kuna vitu viwili ambavyo ni muhimu kuvielewa imani ya upili ndiyo inayounda mfumo wa ndani, mfumo ukisha kuundwa hujidhihirisha kwa nje na moja kwa moja unaenda kuunda mfumo wa nje. Kisha mfumo huu wa nje unatengeneza dini yake ambayo mwalimu ameiita awali, kwanini inaitwa imani ya upili ni kwasababu ile ya kwanza ipo kwa muumbaji na kwanini tunaita dini ya awali kwamba ukristo, uislamu na zingine zinafwata baada ya hiyo? Mwalimu anakwambia tuliza akili utaweza kumwelewa tu.

Kama imani ya awali ilivyo ambayo tunaamini katika uumbaji huwa tunaijenga kwa kujifunza ambapo masomo yake yanakuwa yanatolewa na dini ya upili kwa mfano ukristo ama uislamu, vivyo hivyo imani hii ya upili inajengwa kwa kujifunza, tofauti na imani ya awali kujengwa na masomo yanayotolewa na dini ya upili yenyewe inajengwa na masomo yanayotolewa na nguvu ya ubongo kwa kutumia akili na badala ya dini ya awali kutoa masomo kwa ajili ya imani ya upili dini hii huenda kuunda mfumo wa nje.

Masomo yanayotolewa na nguvu ya ubongo kwa kutumia akili ili kujenga imani ya upili, kama ambavyo dini ya ukristo inavyotoa elimu kupitia biblia, nguvu ya ubongo kwa kutumia akili inatoa elimu ya kujenga imani ya upili kwa kwa kutumia misingi miwili, msingi wa saikolojia an msingi wa pili ni msingi wa filosofia. Misingi hii haiwi kwa kila mtu bali kwa watu wachache ambao wana kitu cha ziada ndani mwao, kama ambavyo unaweza kusikia katika msahafu ama biblia kwamba kulikuwepo na flani akasema hivi, basi kariba ya hao wa kwenye misahafu ama biblia ndivyo ambavyo iko hivyo kwenye misingi ya saikolojia na filosofia.

Hawa watu walipata kutokea katika karne nyingi zilizopita na maneno yao (sio matendo yao kwasababu kinachojenga imani ni maneno, imani huja kwa kusikia) na hayo maneno yao bado yanaishi mpaka leo.

Maneno yao ndiyo yanayotumika katika kuijenga imani hii ya upili kwa wewe mwanadarasa, hivyo utamsikia mwalimu FARADAY akisema, mwanafilosofia mmoja alisema hivi, ama mwanasaikolojia mmoja alisema hivi, yote hayo mwalimu FARADAY anachojaribu kukifanya hapo ni kuijenga imani ya upili ndani ya mwanadarasa ambayo wengi hawaijui. Wanaheri wale walioishi kipindi cha hawa waliokuwa na kitu cha ziada ambao ndio wanafilosofia na wanasaikolojia kama ARISTOTLE, SOCRATE, KARL MARX NA PLATO, maana waliweza kujengwa imani moja kwa moja kutoka kwa wahusika. Mwanadarasa anajiuliza ina maana siku hizi hamna wanafilosofia au wanasaikolojia?.

Jibu ni wapo lakini hatuitambui michango yao kwasababu hatuna imani nao, michango yao itakuja kuonekana na kizazi kijacho. Lakini kutowatambua pia kuna madaraja, kutowatambua kwako mtanzania ni tofauti na kutowatambua kwao superiors. Ngoja mwalimu akazie hapa hapa moja kwa moja superiors asilimia kubwa wanawatambua kwasababu wana imani ya upili, sisi hatuwatambui kabisa kwasababu ya kutokujua kabisa kama kuna imani ya upili. Kwanini superior hataki uwatambue hawa kwasababu wana mawazo (ideas) zilizoimara na zenye kuyafiti mazingira kuliko wale waliopita karl marx kwa kuliona hili lingetokea akatuandikia “The ruling ideas of each age have ever been the ideas of its ruling class” cha kushangaza tumeweza kuliona hili mara nyingi sana lakini hatukujua nguvu kubwa iliyokuwa nyuma yake.

Baada ya superior kuhisi ungekuja kushtuka siku moja akaja kukudumaza hapa, kwamba unauwezo wa kuikuza hiyo imani lakini haitaweza kwenda mbali sana kwasababu umeshindwa kuthamini uwezo wa wanafilosofia na wanasaikolojia waliopo. Lakini kibaya zaidi alichokifanya ni kukuletea uongo uliyopakwa mafuta akijua huwezi kuung’amua kwa kukuaminisha watu ambao siyo wanafilosofia wala wanasaikolojia lakini kakuacha uamini kuwa hao ndio. Na wewe bila kufanya reasoning unakubali na kusema naam ndio hao. Watu wenyewe ni hawa, mtu aliyesomea sana mambo ya filosofi mpaka ngazi za juu za elimu kama uprofesa, ama aliyesomea saikolojia mpaka ngazi ya juu ya elimu. Watu hawa si wanafilosofia wala wanasaikolojia bali ni watu waliojaa imani ya filosofia na saikolojia kwa kuwasoma sana wale watu waliokuwa na kitu cha ziada. Hivyo hawa wanakuwa wameielewa filosofia ama saikoloji lakini siyo kuijua.

Ni wachache sana wanaoweza kuijua na kuielewa vyote wakawa navyo hawa tunawaita (exceptional) lakini kwa sisi wengi wanaielewa kwasababu muda unaotakiwa kuijua huyu anautumia kuielewa nini kinatokea wanaoielewa ndio waalimu ama wakufunzi ama wafundishaji wa filosofia ama saikolojia Aristotle aliliona hili akasema “"Those that know, do. Those that understand, teach." Kwahiyo kumbe mwalimu Faraday pamoja na kwamba unatumia maneno ya kifilosofia kila mara lakini wewe si mwanafilosofi? jibu ni ndiyo mimi siyo mwanafilosofi bali ninaeneza imani ya upili kwa kutumia misingi ambayo ni filosofia na saikolojia hivyo ninaielewa ndio maana nafundisha.

Kwahiyo mtu ambae ni mwanafilosofi ndo yupi kama yule anaemjua Socrate au Aristotle siyo, basi atakuwa ni nani? Blaise pascal aliliona hili akajibu hivi “"To have no time for philosophy is to be a true philosopher." Hivyo Tanzania yetu ina walimu wengi sana wa filosofia lakini wanafilosofia ni wachache.

Baada ya maelezo hayo ambapo Mwalimu alikuwa anajaribu kuelezea kwa uchache kuhusu misingi miwili filosofia na saikolojia ambayo ndiyo hutoa masomo kwa ajili ya kujenga imani ya upili. Kutokana na ukubwa wake na umuhimu wake ilipaswa kujengwa kwenye misingi hiyo na kujengwa ina maana uiishi, lakini hali ni tofauti kidogo kwasababu kwanza hatuijui kabisa hivyo kivipi tutaweza kuiishi?, tunakuja kuuishi mfumo wa nje kabisa ambao unatokana na dini ya awali na ndio maana tunakuwa kama kitu kinachoelea angani bila kushikiliwa na mizizi, ( Mwalimu akifika kwenye nyanja ya elimu atayaanika mengi sana).

Tuliza akili hapa, dini ya awali ni lazima uwe nayo madam umezaliwa chini ya jua hili, hapa ndo kizungumkuti kinapoanzia, haijalishi imani ya upili unayo au laah lakini dini ya awali lazima uwe nayo, sasa nini kinatokea hapo ni kwamba unaenda kutumia imani ya tatu ambayo inaundwa na dini ya upili kutokana na kuundwa kwa mfumo wa nje wazungu wanasema vitu vinaenda anticlockwise yaan badala ya dini ya awali kutumia imani ya upili kwasababu imani ya upili ndiyo inayo-control dini ya awali, inaenda kinyume kwa dini ya awali inayo-control mfumo wa nje matokeo yake imani inayozaliwa kutoka mfumo wa nje hutumika tena kama imani ya kui-contol dini ya awali yani baba anadhibitiwa na mtoto.

Mwalimu ngoja aelezee kidogo imani ya upili ni nini maana akili za wanadarasa zimeanza kuchanganya mafaili, ni hivi imani ya upili ni imani inayofwata baada ya imani ya kwanza ama ya awali imani hii ya awali Mwalimu amesema ni imani juu ya uumbaji, ambapo wengine wanaamini kuumbwa na Mungu na n.k, imani ya upili ndiyo hufuata na ni imani juu ya uumbwaji, hapa ni juu yako mwenyewe, yaan imani juu ya Faraday mwenyewe ambae ameumbwa kutoka kwa muumbaji hii imani ndiyo daraja la kuunganisha vitu vyote vinavyofanyika katika mfumo wa nje na yule muumbaji, pasipo imani hii kuiishi, mambo yote ya mfumo wa nje ni kupaka rangi upepo.

Tukiangalia kwanini dini ya awali hii ni dini juu yako mwenyewe ambayo ni maisha yako unayokuwa nayo kabla ya kutokwa na roho, kwanini awali na ukristo ama uislamu uwe dini upili ni kwasababu yanaanza maisha ama ananza mtu kuzaliwa na kuishi ndipo kinafwata kuwa muislamu au mkristo na ndio maana hata kabla ya wewe mtanzania kujua kitu kinachoitwa ukristo ama uislamu ulikuwa na maisha yenye imani ya yule aliyekuumba imani ya awali na ndio maana wengine hawana dini ya upili lakini wana imani ya awali.

Mwalimu anaomba kwa leo aishie hapa, jitahidi usome kwa utulivu ili uweze kuyaelewa haya, umesoma masomo kadhaa ya mwalimu amejaribu ku-balance kidogo, kwa kuyatoa masomo yanayogusa kutambua kwamba unauwezo gani ama unaweza kufanya nini na nini na pia ameyatoa masomo ya kujitambua kama hili. Kuyaelewa masomo ya kujitambua yanahitaji utulivu la sivyo hutaweza kuyafikia mapinduzi ya kifikra kwasababu hayo ndio nguzo haswa.

Mwalimu ataendelea kuelezea mambo mengi moja kuuelewa mfumo wa ndani, jinsi ya kuutumia na jinsi ya kuuishi kama superiors wengi wafanyavyo, mbili mwalimu ataelezea kuhusu mfumo wa nje, hapa atagusia mambo mengi ikiwa ni pamoja na kwanini watu wamehubiriwa sana kuhusu ujasiriamali ama kanuni za biashara ama wamesoma sana jinsi ya kuongoza lakini bado ni tatizo kaama mwalimu alivyosema mwanzoni mwa somo lakini bado hali iko vilevile na cha mwisho mwalimu ataenda kutueleza pia juu ya kichwa cha somo letu kwamba watu wamesoma vitabu vingi vya watu waliofanikiwa ama wajasiriamali waliofanikiwa vitabu vya kila aina kama vya Napoleon Hill ama Kiyosaki na wengine wengi na hata watu wamefafanua kabisa kwa lugha ya kiswahili ili watu waweze kuelewa lakini bado msaada hauonekani.

Na mwalimu anakwambia hakuna kitabu ambacho kimeelezea mambo ya kipuuzi ama mambo ya uongo vyote/vingi viko sahihi na vimeongelea ukweli LAKINI KWANINI SASA HATUENDI?? Fuatilia part B ya somo hili.


By H.FARADAY (0625934471).
 
NYONGEZA.​

Ngoja mwalimu akuweke sawa mwanadarasa, ni wajibu wa mwalimu kutumia ukali pale unapohitajika ili akili ipate stimulus. Usichanganye, masomo anayoyatoa mwalimu si kama mihadhara au mahubiri ya dini, hii ni shule ama elimu kama elimu zingine unzazozijua. Ni sawa na mtu anavyoanza elimu ya awali mpaka chuo, hata elimu hii iko hivyo utofauti wake ni kwamba wewe mtanzania haijarasmishwa kwako, kutokana na wengi kutoijua na wanaoijua wameamua kubaki nayo bila kuwafikishia watu.

Kwanini watu wanaoijua wanashindwa kuwapa wanajamii? Sababu ya kwanza Nature ya watanzania, watanzania wamejengwa katika msingi wa kutokutaka kuyajua maarifa, baadhi ya misingi waliyokaririshwa ndiyo wanayoiona thabiti na hivyo kushindwa kuiruhusu akili kupokea maarifa mapya.

Changamoto ya pili kazi kubwa iliyonyuma ya kuifanya elimu hii mwingine aweze kuielewa, kuna kazi kubwa ya kuileta katika lugha ambayo mtanzania wa kawaida ataielewa kwa maana ya lugha ya kiswahili, wengi wameipata kutoka lugha za kigiriki, kilatini na kiingereza. Hivyo ni gharama kubwa kuiandaa inahitaji nguvu akili na muda mwingi sana.

Elimu hii ina vitu vingi sana kuliko unavyofikiri, mwalimu vitu alivyovigusia ni vidogo sana asilimia 5 ya 100 lakini nguvu ya hiyo asilimia 5 ya mia kwa mwenye akili ameweza kupata kitu cha ziada kwa masomo yote mwalimu aliyoyatoa.

Ukombozi wa kifikra ni mkubwa sana, kuliko unavyofikiri wanaobahatika kuifahamu elimu hii wanatamani siku zirudi nyuma ili wabadilishe mfumo mzima wa maisha. Na mengine mengi ambayo mwalimu hataweza kuyamaliza yote kuyaongea hapa.

Tuhamie upande wa pili uwe makini hapa, katika suala zima la kuelimika, si suala la wewe kulazimishwa hii ni kwa yule ambae ataona umuhimu wa kuelimika, hivyo elimu yoyote inayotolewa siyo ya watu wote ni ya watu wachache wenye utayari wa kuijua. Mwalimu anatoa mwendelezo wa masomo haya, kwa kuendelea kufundisha kwenye group aliloliunda, hakuombi, wala kukubembeleza wala kukulazimisha kuja kujiunga yule mwenye kuhitaji kujifunza haya atamtafuta mwalimu.

Masomo haya sio simulizi au hadithi bali ni science ya maisha, mwalimu msaada wake ni kujitolea kukufikishia elimu hii ambapo wengi pamoja na kuijua kwao wamesita kuitoa, gharama ya muda akili na nguvu ya mwalimu acha iwe juu yake basi jiandalie mwenyewe hata nakala bado ushindwe unahitaji mwalimu akuandalie aje akuletee hadi nyumbani kwako!!, so much amaizing Tanzania ina baadhi yawatu wa ajabu sana kuwahi kutokea juu ya uso wa dunia hii.

Mwenye nia ya kupata mapinduzi ya kifikra mtafute mwalimu, mwalimu anahitaji watu serious wa kuhakikisha mind za watanzania zinabadilika haijalishi wewe peke yako unajimudu basi saidia elimu hii iende na wengine wajimudu, kuna raha gani ya wewe kula kushiba wakati jirani yako anakufaa njaa. 21-37% za watanzania ni maskini wa kutupwa, kujinasua na hili hakutawezekana bila kubadili attitude of mind. Ada ya elimu hii kwa huyu mtanzania tunayetaka aelimike hataiweza, lakini kushindwa kutoa mia mbili kwa ajili ya kuyaweka haya kwa ajili ya vizazi vyako ni ujinga, amka mtanzania.

Naomba WhatsApp nifwatwe na watu wenye ubongo wenye akili na si vichwa vyenye ubongo.

H. Faraday.
 
Asee hili somo linahitaji utulivu wa hali ya juu ukisoma kwa kukurupuka hutaelewa hata kimoja

Its hard to deep understand but easy to get partial understand according to what you have read

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwalimu mke wangu ana gubu,mda mwingine ananifokea mbele ya mfanyakazi au mdogo wake ,
Anathamini anachokifanya yeye au kukianzisha ila hathamini nilichokianzisha mimi mfano naweza nikawa nimenunua mifugo yeye haijali kwa kila kitu piahapendi wakwe nimemvumilia naomba mbinu ya kumshambulia kisaikology niharibu akili yake
 
Mwalimu nilikua na swali

Kwa hyo imani ya upili inapata mafunzo kutoka kwenye dini zote mbili yaan dini ya awali na dini ya upili?

Lakini kwa kusoma hapo nimebaini mfumo wa ndani ambao unajikita kwenye dini na imani (kwa maana ya imani zote mbili ya awali na ya upili)una kusudi la kuandaa mfumo wa nje mi niuite mfumo wa mazoea kujiandaa kwa chochote kitakachotokea iwe ni kibaya hama kizuri

Kwa nini kwa sababu mfumo wa mazoea hauwezi kubadilika kwa haraka kwa kuwa ulishazoeleka hivyo utachukua muda mrefu kufanyia assessment mfumo wa ndani kuzoeleka kwa sababu ya jambo moja kutokuipa kipaumbele japo sijafahamu kiundani nini hasa kilichomo ndani zaidi ukiachilia mbali vitu vilivyoweza kuunda mfumo wa ndani ambao ni dini na imani ya upili

Swali langu mwalimu hapa mwalimu ni kwamba mifumo hii yote ya ndani na nje inamjengaje mwanadarasa kutambua nafasi aliyonayo na kutengeneza strategies za kujikomboa yeye na kizazi chake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwalimu mke wangu ana gubu,mda mwingine ananifokea mbele ya mfanyakazi au mdogo wake ,
Anathamini anachokifanya yeye au kukianzisha ila hathamini nilichokianzisha mimi mfano naweza nikawa nimenunua mifugo yeye haijali kwa kila kitu piahapendi wakwe nimemvumilia naomba mbinu ya kumshambulia kisaikology niharibu akili yake
Mwalimu atakuwa na maswali kadhaa ya kukuhusu ambayo ni binafsi kidogo hivyo mfuate p.m au tumia namba yake.

Lakini kwa faida ya wote "upo katika vita ya akili na hisia kumshambulia ni kuzidi kurusha mabomu zaidi, binadamu tumeumbiwa kukubali kushindwa kwa muumbaji pekee lakini si kwa binadamu mwenzio, hivyo hakutakuwa na mwisho wa vita yenu mpaka pale mmoja wenu atakapovuja damu ya ndani (spiritual blood)" hivyo hupaswi kumshambulia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom