LESSON THREE~sehemu ya kwanza
KUJIAMINI (self confidence).
Amani iwe nawe mwanadarasa popote ulipo, mwalimu anaamini u mzima wa Afya ya mwili na unaendelea
kuwepo ama
kuishi chini ya jua hili. Kabla hatujafunga masomo yetu ya utangulizi na kuanza kuzichambua nyanja mbalimbali twende tukajifunze kitu muhimu kabisa kukijua ambacho ni
kujiamini ama
ujasiri binafsi. Hili suala linagusa kila nyanja iwe ni Elimu, biashara, kilimo ama uchumi na nyanja mbalimbali, hapa tutaenda kuangalia kwa ujumla
(in general). Tutakuja kuongelea tena kwenye kila nyanja tutakayoichambua.
Mwalimu anakwambia bado haujachelewa kutuma namba yako ili akuongeze kwenye list kwa ajili ya masomo yanayokwenda kuchambua nyanja mbalimbali yatakayokuwa yanaendelea huko whatsapp.
Twende tulianze somo letu, moja ya sababu kubwa ya watu kuwa hivyo walivyo ni kukosa/kushindwa kujiamini, tungelikuwa bado tupo kwenye kipindi kama cha karne zilizopita lisingeonekana umuhimu sana, lakini kwa karne tuliyopo sasa iliyojaa
USHINDANI ni muhimu sana tena sana kulifahamu hili. Tunapozungumzia kujiamini tunamaanisha nini, tumaanisha hivi
uthaminishaji chanya juu yako mwenyewe katika kuweza kufanya jambo fulani (
your positive self-assessment in performing a task). Kwa lugha rahisi ni kuamini katika uwezo wako binafsi
(to believe in your own abilities).
Sote tunajua kuwa vitu vyovyote vipya vinagunduliwa na binadamu na si paka wala mjusi bali binadamu, na huo ugunduzi huanza na binadamu mmoja
(a single person). Kabla ya kutekeleza ugunduzi huo aliwaza kwanza kama tulivyosema kwenye masomo yaliyopita kuwa kila kitu huanzia ndani (
kama wazo) ndipo huja kujidhihirisha kwa nje (
kama kitendo). Baada ya kupata wazo kilichofwata kwa mtu huyo ni kujiuliza je
nitaweza/staweza kufanya? Na nitafanikisha? Hapa hakuwa na jibu alijiambia kuwa nitapata jibu baada ya kufanya, kitendo cha kuchukua hatua ya kufanya hujificha chini ya neno
kujiamini.
Kuchukua hatua ya kufanya ndiko tunakoita kujiamini, unaamini katika uwezo wako kwamba unaweza kufanya bila kujalisha matokeo yatakuwaje, uwe makini hapa,
hamna njia yoyote ya kujua/kuhakikisha kama unaweza au hauwezi jambo fulani pasipo KUFANYA. Kuna msemo wa kawaida kabisa wenzetu wanasema “
when you start the journey of your professional life, have confidence in your abilities. Because you have not proven your abilities yet.” < unapoianza safari ya utashi katika maisha yako, jiamini au kuwa jasiri katika uwezo wako kwasababu haujauhakikisha (
not proven) uwezo wako bado.
Mwalimu anakwambia tuliza akili uweze kupaelewa hapa, moja ya kosa kubwa ambalo wanadarasa wanalifanya ni kushindwa kutofautisha au kushindwa kufuata
hatua za msingi kuanzia ndani (
kwenye kufikiri) mpaka nje (
kwenye vitendo). Kushindwa ama kukosa kujiamini kunakuja baada ya kukosa mpangilio kuanzia
kifikra mpaka nje (
vitendo). Twende tukaangalie tunapokosea, ni hivi;
Unapowaza kufanya jambo lolote hata liwe kubwa kiasi gani, hakikisha hauvuki hatua ya kwanza ni hatua gani hiyo hii hapa, hatua ya kwanza inakuwa kati ya mawazo (
idea) na kutenda, mawazo hubeba maarifa (
knowledge) juu ya hicho unachowaza kukifanya, huwezi kuwaza kufanya kitu chochote bila kuwa na maarifa (
haijalishi maarifa ya kutosha au laah) juu ya kitu hicho. Mwalimu aliwahi kusema kuwa kila kitu kipya tunachokiona huanza kama jaribio lakini nyuma ya jaribio kuna kitu kinaitwa nadharia (
hypothesis), hivyo katika hatua ya kwanza ambapo ni mawazo na kutenda humaanisha nadharia na jaribio (
hypothesis and experiment). Hivyo hupaswi kuvuka hapo kwenye mawazo na vitendo. Hupaswi kuvuka kwenda wapi? Twende tukaiangalie hatua ya pili;
Hatua ya pili,
uchunguzi na
matokeo (
observation and results) baada ya kuwaza na kufanya (to take an action) kinachofwata ni uchunguzi wa nini kinachoendelea katika kitendo hicho, Je kinachoendelea kinakupa mwanga wa kuyafikia matokeo uliyoyawaza? Na bila kujalisha ulichokutana nacho wakati wa uchunguzi ulipokuwa unafanya jambo hilo je mwisho umepata matokeo gani?. Kuvuka ama kuruka hatua kunakuwaje ambako ndiko mwalimu anakwambia ni kosa kubwa na kunapelekea ushindwe kujiamini na kisha unashindwa kufanya kabisa jambo hilo ni hivi;
Mwanadarasa anapokuwa katika hatua ya kwanza ya mawazo
huruka hatua zingine zote zinazofwata na kwenda moja kwa moja kwenye hatua ya
matokeo, yaani yeye hujipa hatua mbili tu (
mawazo na matokeo) “
hahaha, hatari sana! Wala Mwanadarasa hataki kusumbua akili yake anajirahisishia na kujipa hatua mbili tu anaamua kupita
short cut” kinachofanyika hapo ni Mwanadarasa kujipa matokeo mwenyewe kwenye kichwa chake bila kitendo kufanyika, ana heri yule anaejipa matokeo chanya kabla ya kitendo maana huyo ndiye aliyejaa kujiamini (
Over confidence) lakini huyu tunaemzungumzia hapa yeye matokeo ambayo hujipa ni hasi. Hivyo hushindwa kabisa kukifanya hicho kitu kwasababu ya kujipa matokeo mwenyewe.
Anauona uwezo wake hauwezi kufanya jambo hilo pasipo hata kuujaribu, matokeo yake jamii inakosa ugunduzi wa vitu mbalimbali, jamii inakosa uanzishwaji wa vitu vipya tunarudi kulekule tunaishia kuiga tu. Hivyo mwalimu wako anakwambia mwanadarasa
HAUNA UHAKIKA JUU YA UWEZO WAKO KWAMBA UNAWEZA AU LAAH NI MPAKA UMEFANYA. Kiuhalisia ni ngumu kuanza kuyatekeleza mawazo yako kwa kuanza na 100% za kujiamini (
confidence), kujiamini huimarishwa na kuanza kuchukua hatua ya kufanya. Unaweza ukawa shuhuda hapa ukamsikia mtu anasema
nilikuwa nakihofia tu bure kukifanya hiki kumbe kirahisi tu.
Kuna mwanafilosofia mmoja anaitwa
Plato anasema “
The beginning is the most important part of the work” kumbe kitu cha kwanza kabisa katika kufanya jambo lolote ni
KUANZA (beginning). Au kwa lugha nyingine tunaweza kusema uthubutu na ni hatua moja muhimu sana ya kujenga kujiamini (
self-confidence). Aina ya pili ya kutokujiamini ambayo pia ina wanadarasa wengi ambao wengi wameiweza ile ya uthubutu wa kuanza kufanya jambo ni hii hapa twende tukaiangalie;
Aina hii ya pili huja baada ya mtu kuanza kufanya, anapoianza hatua ya pili ya uchunguzi juu ya mwelekeo wa kile alichokikusudia, uchunguzi wake ukibeba hasi nyingi basi kujiamini kote kunatoweka, anaishia hapo na hiyo hujijenga na kuwa
TABIA huyu jamaa
Michael Jordan anasema
“if you quit once it becomes a habit. Never quit” ndio maana utamsikia mtu anasema
nimejaribu kufanya vitu vingi kwenye haya maisha lakini ukimwangalia hana hata kimoja mkononi. Watu wanashindwa kusimamia kile wanachokiamini. Watu wanashindwa kuwa wavumilivu
jean Jaques anasema “
patience is bitter but its fruits is sweet”. Mtu anatamani aanze kufanya jambo leo kesho aone mafanikio.
Mwalimu anakwambia safari ya mafanikio katika maisha ni kama kilimo cha miti tena ya mbao huwezi kupanda na ukatarajia kuvuna ndani ya miezi miwili au mitatu ijayo. Lakini kuna sababu kadhaa zinazopelekea watu kushindwa kujiamini au kupoteza kujiamini, tutaenda kuziangalia chache ambazo ni muhimu sana. Tukianza na ya kwanza misingi uliyojengwa nayo mwanadarasa hapa mwalimu aliongelea sana katika masomo yaliyopita, watu wamejengwa kwenye msingi
kawaida ama mazoea, mwanadarasa haamini kama anaweza kufanya jambo ambalo halijazoeleka katika jamii, mwanajamii amejengwa katika msingi wa kutokuwa na
uthubutu hivyo haamini kama anaweza kuthubutu na kufanya kitu tofauti na wengi walivyozoea.
Wanadarasa walio wengi wanaishi maisha ya kuwapendeza watu
(to please people), kabla ya kufanya chochote mwanadarasa anakuwa na maswali ya
kijinga kabisa kichwani, mwalimu lazima awe mkali kidogo hapa, maswali yenyewe ni kama haya
moja wengine watasemaje (
what will others say?) Mbili je Watu watanicheka (will people laugh at me)? Tatu nitawatazamaje watu endapo hili jambo litafeli (how can I face others if fail?) Na maswali mengine mengi mwalimu anayaita ya
kijinga. Kuna msemo mujarabu kabisa unasema “
Dont be afraid to stand for what you believe in, even if that means standing alone” <usiogope kukisimamia kile unachokiamini hatakama unaona umesimama peke yako hamna anaejali> hivyo ndivyo mwanadarasa inatakiwa uwe na mwalimu anakwambia tena kama alivyokwambia kwenye masomo yaliyopita toka kabisa kwenye msingi kawaida unaokuongoza ujiwaze katika kufeli kuna huyu jamaa anaitwa
Bill Cosby anasema “
In order to succeed, your desire for success should be greater than your fear of failure” <ili kuweza kufanikiwa, matamanio ya kufanikiwa yanapaswa yawe makubwa zaidi kushinda hofu ya kushindwa>.
Kwanini mwalimu anazungumzia zaidi wanadarasa kushindwa kujiamini katika kufanya mambo mageni/mapya, kwasababu wengi wa wanadarasa hawapati taabu sana kujiamini kufanya mambo yaliyozoeleka katika jamii. Kwanini watu hujiamini kufanya mambo ambayo tayari yamezoeleka kwasababu wanajiona kupata
ulinzi wa jamii kwamba kwa sehemu yoyote mwanadarasa atakayokwama basi hatakosa wa
KUMUULIZA, lakini kwenye kufanya jambo jipya anajiona ataonekana kichaa mbele ya jamii na ni kweli mwanafilosofia mmoja anaeitwa
Aristotle anasema “
no great genius has ever existed without some touch of madness”. Hivyo usiogope watu watakuonaje ni wajibu wako kuwashangaza watu (
to prove them wrong).
Sababu ya pili ya watu kushindwa kujiamini, kukosa maarifa na ufahamu wa kutosha juu ya kitu wanachopanga kukifanya, (
lack of enough knowledge and good understanding). Mwalimu anakwambia kwamba watu wengi hushindwa au hukosa kujiamini kwasababu hawana uelewa wa kutosha juu ya kufanya kitu fulani, kwasababu wapo kwenye msingi wa kuiga, basi kila atakachotaka kukifanya hawezi kuwa na uelewa wa kutosha juu ya hicho kitu, wengi wao husita kufanya kabisa lakini wale ambao hulazimisha kufanya basi hufeli vibaya kiasi kwamba wanashindwa kuinuka tena kisha mtaani watu huwapachika majina kuwa
mkurupukaji. Hata iwe biashara tutakuja kuangalia vizuri tukifika kwenye nyanja ya biashara, kabla ya kuanza biashara yoyote hakikisha unataarifa zote muhimu (
details) za kuihusu biashara hiyo. Moja ya kitu wanadarasa walio wengi wanashindwa kukizingatia na ni kitu muhimu basi ni
kutenga muda wa kutosha wa kutafuta kukijua (
doing research) juu ya hicho anachotaka kufanya na kuruhusu hisia za kukuona ukifanya hicho kitu zikikuongoza.
Sababu ya tatu kushindwa kuuishi wakati uliopo, watu wengi miili yao inaishi wakati uliopo huku mawazo na fikra zao zinaishi wakati uliopita (
past). Wengi wao kipindi fulani kilichopita walijaribu kufanya vitu viwili vitatu na viliwaletea matokeo mabaya sana, ile hali ikawaharibu kisaikolojia na wakakubali kuishi nayo. Bado mwanadarasa anajiona ni yuleyule aliyeshindwa kipindi kile, bila kujalisha sababu zilizofanya ashindwe kipindi kilichopita, bila kujalisha kuwa kwasasa ufahamu umeongezeka kiasi gani. Mwalimu anakwambia mwanadarasa
uishi usasa achana na ukale. Maarifa uliyonayo kwasasa ni tofauti na yale yaliyopita kale haina cha kufanya nawewe, historia haibadilishi chochote juu yako (
past has nothing to do with you).
Karl marx anasema
“it is not history which uses men as a means of archiving-as if it were an individual person- its own ends. History is nothing but activity of men in pursuits of their ends”.
Kataa kabisa kuishi kutokana na historia mwanadarasa “
Stop being a prisoner of your past. Become the architect of your future”. By Robin.
Mwalimu anasema tumaangalia kwa uchache tu kuhusu kujiamini (
self-confidence) tutakuja kuangalia tena kwa kila nyanja tutakayoigusa.
<H.FARADAY> (0625934471).