Daraja la Kinyerezi labomoka

Daraja la Kinyerezi labomoka

Sio madereva tu, tatizo wajenzi hawaweki mipaka ya UZITO wa magari yanayotakiwa kupita ktk madaraja au barabara zinapokamilika!
if i remember well, pale waliweka limit

na pia temporary darajas zina limits tu... lile lorry ni kubwa sana na zito hata kwa barabara ya kawaida
 
..dreva anatakiwa kupewa adhabu kali...,

cc: John P. Magufuli

sio dereva tu hata mwenye kumiliki hilo gari anapaswa kuchangia gharama za ujenzi upya...
 
Mwenye lori lazima awajibike pamoja na dereva wake. Wote wamevunja sheria za nchi. Shukrani kwa picha nzuri sana.
 
sio dereva tu hata mwenye kumiliki hilo gari anapaswa kuchangia gharama za ujenzi upya...
Hivi hakuna hata tamko lililotolewa na mamlaka yoyote juu ya hili? Hukawii kuambiwa dereva alitoroka!!😡
 
Duhh,
Nimeona Taarifa ITV,
Daraja limetiwa alama ya uzito mwisho wa 7 tones,jamaa akalamba mzigo wa tani 40,kweli dereva killer.
Magufuli alivyo lazima atataifisha hilo gari.
 
Duhh,
Nimeona Taarifa ITV,
Daraja limetiwa alama ya uzito mwisho wa 7 tones,jamaa akalamba mzigo wa tani 40,kweli dereva killer.
Magufuli alivyo lazima atataifisha hilo gari.


Jamaa yangu thamani ya hilo gari haifiki hata robo ya kujenga nguzo za daraja
 
Hii barabara in vibao sehemu nyingi ikionyesha ukomo wa uzito wa gari inayotakiwa kupita. Huyu jamaa naona alikwisha zoea kuchepuka. Magufuli tuone unafuatilia sheria bila upendeleo hapa, sio kwenye kuvunja vibanda tu vya wazee wetu waliojenga miaka hiyo pembeni ya barabara.
 
Kuna kibao kinaonesha maximum tonnage kule mwanzoni kabisa atakuwa alikipuuza

Mashuhuda wanadai tajiri aliyekua amekodisha hilo lori alimlazimisha dereva kupita licha ya kuambiwa kwamba walikua wamebeba mzigo mzito wa matofali. Ingawa huo hauwezi kuwa utetezi wa dereva lakini inadawa huyo mama amekua akipitisha mizigo mikubwa akikihuka amri ya uzito unaotakiwa. Na hilo Kontena kulikua na vibarua ambako inadaiwa watatu wamefariki.
 
Sign board zipo kwanini wote hawaoni wanafaa wAadhibiwe tu

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
..dreva anatakiwa kupewa adhabu kali...,

cc: John P. Magufuli
Huyu tungekuwa na sheria kali kitanzi kilikuwa halali yake!! Hizi sheria hazifuatwi kabisa, utakuta hata huku kwetu vijijini barabara zimeandikwa Max. Weight 10T lakini cha ajabu malori yenye tani zaidi ya hizo yanapita tu!! Sasa hii hasara nani atalipa jamani?
 
Niko Mbezi analogia nataka nikatize ya Kinyerezi daraja limeshatengenezwa ? ova !!!!
 
Hii barabara in vibao sehemu nyingi ikionyesha ukomo wa uzito wa gari inayotakiwa kupita. Huyu jamaa naona alikwisha zoea kuchepuka. Magufuli tuone unafuatilia sheria bila upendeleo hapa, sio kwenye kuvunja vibanda tu vya wazee wetu waliojenga miaka hiyo pembeni ya barabara.

kikawaida Dr Magufuli amekuwa akifuata sheria ktk utekelezaji wa kazi zake,sema tu wanasiasa walio wengi wanatete kura zao na hutumia mianya hiyo kupambana na Dr Magufuli ili asifanikiwe ktk utekelezaji wa majukumu yake,imetokea hii pale kigamboni na wabunge wa DSM walikuja juu kujifanya wanawatetea watu wao wa DSM eti hawawezi kulipa 200tzs na hivyo kuwaambia wapige mbizi ni kuwatusi,lakini Dr ALIKOMAA NAO NA WALILIPA na maisha yanakwenda.
ebu wa mwache Dr apige kazi bila kumwekea vikwazo
 
haya madaraja ya limits lakini madereva wetu shida sana, mwenye lorry anatakiwa afidie hasara kwa kweli
Kosa kubwa na linalotugharimu ni kuaminishwa kuwa elimu ni nyenzo ya kutafutia kazi na kwa wengi haihusiani kabisa na kupambana na changamoto za kuishi. Madereva wengi kama victims wa hili nao wamebakia kuendesha magari bila kufuata sheria alafu ikitokea ajali utasikia "ni mapenzi ya Mungu", "ajali haina kinga", yaani kwa kifupi tunaangamia kwa ukosefu wa maarifa!

 
duu huyu dereva ni zaidi ya JANGA
 
Nakumbuka mwaka jana ili daraja lilivunjwa na lori kwa misingi ya kuzidi uzito, likarekebishwa na kuanza kufanya kazi, lakini juzi mjinga mwingine kapita tena na gari linalozidi tani 7 na kulivunja tena
Hii ni njia muhimu kwa wakati wa mbezi,segerea, Tabata , kinyerezi etc lakini hii hali imehachwa ikijirudia rudia na kubabisha usumbufu kwa raia.
Ni vyema kukawa na approach mpya zidi ya wamiliki na madereva wa malori makubwa yanayopita kwenye madaraja madogo,
 

Attachments

  • IMG_0085.JPG
    IMG_0085.JPG
    361.1 KB · Views: 123
Back
Top Bottom