VIKWAZO
JF-Expert Member
- Apr 9, 2011
- 1,899
- 580
Kuna lori lililokuwa limebeba kontena limejaribu kupita daraja linalounganisha UKONGA {BANANA)- SEGEREA- KINYEREZI NA MBEZI limeharibika kabisa kwa kutumbukia na lori , kwa sasa foleni ni kubwa magari yote yanarudi, kwa wanaotoka mjini ni vyema kutumia njia ya VINGUNGUTI kwenda KINYEREZI, SEGEREA NA MBEZI,
Daraja limearibika sana.
NI VYEMA SHERIA IKACHUKUA MKONDO WAKE, haiingi akili mjinga mmoja kukata mawasilino wa watu wote kwenye njia muhimu kama hii.
Mfumo wa kudhibiti malori ya mizigo ni dhaifu sana nchini, madereva wangepewa route za kupita pale wanapotoa mizigo bandari na wanapoingiza mizigo hapa mjini kutoka mikoani,
Bila shaka jamaa wametumia mwanya wa polisi/trafic kutofanya kazi usiku kufanya huu utumbo, hivi kwa nini usiku kwa mji mkubwa kama Dar jeshi la polisi linalala mapema HIVYO?
UPDATE
Monday 09/03/2015
Limevunjwa tena na lori lilizidi uzito

Nakumbuka mwaka jana ili daraja lilivunjwa na lori kwa misingi ya kuzidi uzito, likarekebishwa na kuanza kufanya kazi, lakini juzi mjinga mwingine kapita tena na gari linalozidi tani 7 na kulivunja tena
Hii ni njia muhimu kwa wakati wa mbezi,segerea, Tabata , kinyerezi etc lakini hii hali imehachwa ikijirudia rudia na kubabisha usumbufu kwa raia.
Ni vyema kukawa na approach mpya zidi ya wamiliki na madereva wa malori makubwa yanayopita kwenye madaraja madogo,