Dar yaongoza ukatili wa wanawake

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
1614235620427.png

Waziri wa Afya nchini Tanzania, Dk Dorothy Gwajima ameutaja Mkoa wa Dar es Salaam nchini Tanzania kuongoza kwa kuripotiwa matukio 2618 ya ukatili wa wanawake mwaka 2019/20.

Dk Gwajima amesema hayo leo Jumatano Februari 24, 2021 wakati akifungua kongamano la chama cha maofisa maendeleo wa jamii nchini lililofanyika jijini Dodoma.

Amesema Serikali inatekeleza mpango wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto lakini pamoja na jitihada hizo bado kuna changamoto ya ukatili wanayofanyiwa watoto.

Ameutaja ukatili huo ni kubakwa, kuajiriwa katika kazi za hatari, kutosikilizwa pamoja na mila na desturi zinazoendeleza ukatili kwa wanawake na watoto.

Amesema mwaka 2019/20, matukio 14,891 wakiwemo wanaume 2,679 na wanawake 12,212 yaliripotiwa nchini.

“Hii maana yake wanawake wanafanyiwa ukatili mkubwa sana kwa takwimu hizi..., hili halikubaliki,” amesema.

Amesema pia katika mwaka huo wa 2019/20 matukio 14,222 ya ukatili wa wanawake yaliripotiwa nchini.

“Eti ushangae wewe, kule ambako tunasema maendeleo ni makubwa yanaendelezwa na matendo ya ukatili. Dar es Salaam matukio 2618, Arusha 1393, Tanga 1352, Lindi 1161 na Manyara 968,”amesema.

Amehoji tatizo ni nini kwenye miji hiyo mikubwa ambayo kila nyumba kuna Televisheni, kuna wasomi na barabara, “takwimu si nzuri haipendezi, inatakiwa kuimarisha nguvu nyingi kwa kuzungumza na jamii ili trend katika miaka inayokuja ishuke.”

Amewataka maofisa maendeleo hao kuhakikisha kuwa kamati hizo kwa ajili ya kushughulika na changamoto hiyo zinapewa mafunzo na kusimamia ulinzi na usalama wa wanawake na watoto katika maeneo yao.

Amesema kwa kufanya hivyo watakuwa wamewaokoa watoto dhidi ya mimba za utotoni.

Chanzo: Mwananchi
 
Kusema kwamba inaongoza sidhani kama yupo sahihi. Tatizo kaangalia namba directly.

Dar inaweza kua na matukio 2,618 kama alivyodai ila ukicompare na total population ya watu Mil 7 iyo ni ndogo sana.
 
Very sad,,,pia enyi wanawake/wakina dada ombeni sana mupate wakaka wema wakuwaowa,,,wengi wa wanamme hawakutulia na wengine ni walevi na watumia drugs.
 
Kule Kanda maalum Ni mengi zaidi ya mno Ila hayaripotiwi kwani kwa ujinga walionao wanawake wa kule wanaona ni ujiko kufanyiwa ukatili.
Mkoa wenye idadi ndogo sana Ni TANGA. Na mkoa unaongoza kwa ukatili dhidi ya wanaume Ni Mbeya.
 
Back
Top Bottom