Dar: Yaliyojiri Kuagwa kwa Mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Kampuni za IPP, Reginald Mengi

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,814
11,991


Habari,

Mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Kampuni za IPP, Reginald Mengi uliletwa nchini jana Jumatatu Mei 6, 2019 saa 8:00 mchana na ndege na baadae kuhifadhiwa katika Hospitali Kuu ya Jeshi Lugalo, na leo Jumanne Mei 7, 2019 utaagwa viwanja vya Karimjee,

Tuungane hapa kwa kile kitakachojiri kutoka viwanja hivi.

Hii ni ratiba ya kuaga Mwili Karimjee

UPDATES;

UPDATES:11:05
Prof. Palamagamba Kabudi: Katika uhai wake, Dr. Mengi ameshiriki moja kwa moja kukuza uchumi wa nchi yetu na kutoa ajira, hakusita kuwavutia wawekezaji kuja kuwekeza nchini.

Prof. Palamagamba Kabudi: Serikali inatambua pia kwa mchango wake alioutoa katika masuala ya kijamii. Utaratibu wa kukutana na kufurahi na watu wenye ulemavu, ni ishara ya upendo wa makundi hayo, maisha ya Dr. Mengi yana mengi ya kujifunza.

Harrison Mwakyembe: Huwezi kuongelea sanaa inayogusa mamilioni ya watu hapa nchini bila kumtaja Mengi. Dr. Mengi ameondoka na amemgusa kila mmoja.

Balozi Dk. Mwapachu: "Mheshimiwa Rais hudhurio lako ni ashirio la upendo kwa Dk. Mengi, Dk. Riginald Mengi alikataa umaskini, alisumbuliwa sana na kuwepo kwa umaskini ndani ya taifa letu lenye utajiri". "Kwa upande wa elimu, alitambua tatizo la elimu kwa wasichana, aliwafadhili wasichana wengi wa kimasai".


Mkurugenzi Mtendaji Joyce Mhavile (Katikati) na Mkurugenzi wa Masoko wa ITV/Radio One, Mkurugenzi wa masoko Joyce Luhanga (kulia) wamefika kwa ajili ya kumuaga mpendwa wetu Dr. Mengi hapa katika ukumbi wa Karimjee Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli na Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan, wakiwa katika ukumbi wa Karimjee, kumuaga mpendwa wetu, Dr. Mengi.



Wanafamilia ya Marehemu, Dkt. Reginald Mengi wakiwemo watoto na mkewe Jacqueline Ntuyabaliwe tayari wameshawasili katika ukumbi wa Karimjee kwa ajili ya kumuaga Mpedwa wetu Dkt Mengi.

Mwili wa mpendwa wetu, Dr. Reginald Mengi, ukiingizwa katika ukumbi wa Karimjee, kwa ajili ya kuagwa.

Video hapa chini ni Mwili wa Marehemu Dr. Mengi ulivyokuwa ukiingizwa hapa kwenye ukumbi wa Karimjee leo hii. Marafiki zake James Mbatia na Christopher Ole Sendeka wamebeba jeneza lake wakiwa na majonzi na taswira isiyofutika machoni mwao.

Rais Magufuli pamoja na Rais mstaafu wa awamu ya 2 Ali Hassan Mwinyi wakitoa heshima za mwisho mbele ya mwili wa mpendwa wetu Dr Reginald Mengi

Vilevile unaweza kufuatila Mubashara hapa kwenye Video

Your browser is not able to display this video.












UPDATE
Mwili wa mpendwa wetu Dr.Mengi umeshawasili nyumbani kwake Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Ibada ya kuaga mwili wa marehemu Dr, Reginald Mengi imeanza nyumbani kwake, kwa wale ambao hawakupata nafasi ya kuaga katika ukumbi wa Karimjee na hawatokwenda Machame wanaaga nyumbani muda huu

UPDATE
Mwili wa marehemu Dr.Mengi tayari umekwishawasili nyumbani Nkweseko Machame ambapo mwili utalala kabla ya kesho Kwenda ibadani na baadae mazishi





 
Ayubu 14:1-2

1 Mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke Siku zake za kuishi si nyingi, naye hujaa taabu.

2 Yeye huchanua kama vile ua, kisha hukatwa; Hukimbia kama kivuli, wala hakai kamwe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…