Dar: Tundu Lissu ahutubia mkutano mkuu wa CHADEMA, ataka asaidiwe arudi nyumbani, kashapona

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,895
Mbunge wa zamani wa Jimbo la Singida Mashariki (CHADEMA), Tundu Lissu ameuhutubia mkutano mkuu wa chama hicho unaoendelea katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam akisema, mpango wa kukiua chama hicho iliyopangwa imeshindikana na zaidi imekiimarisha zaidi chama hicho.

Lissu amesema Madaktari wake wamemwambia amepona na yuko tayari kurudi Tanzania, kwa ajili ya kuungana na wanachama wenzake wa CHADEMA, na ameomba chama chake kimsaidie haraka iwezekanavyo aweze kurudi. “Madkatari wangu wamesema nimepona, nachechemea kidogo lakini nimepona na niko tayari kurudi nyumbani. “Nipo tayari kurudi nyumbani kuungana na makamanda wengine ili tutengeneze nchi. Naombeni tushirikiane ili niweze kurudi nyumbani haraka na salama.

Mbele ni kuzuri kuliko huko tulikotoka. "Niwatake wanachama wenzangu wa CHADEMA tufanye maandalizi ya kutosha, ili ngwe iliyobaki ambayo siyo ndefu itakuwa ni ngwe ya kurudisha nchi katika utu, demokrasia na haki binadamu. "Baada ya mateso yote tuliyopata, baada ya bonde la uvuli wa mauti, njia iliyobaki ni kuchukua nchi mwakani. Hakuna walichobakiza, wametufunga, wametujeruhi na kila mateso, leo tuna nguvu zaidi kuliko tulivyokuwa.

“Yote yaliyotokea mpaka leo ni utekelezaji wa azma ya kuua mfumo wa vyama vingi. Kwa ushahidi huu wa mkutano na mfumo wa uchaguzi katika chama mpaka siku ya leo, hicho walichokidhamiria hakijafanikiwa mpaka leo,” amesema Tundu Lissu kwa njia ya Video Call.
 
Sisi tutapaki karandinga Airport, akikanyaga tu ardhi yetu, tunapiga pingu.

1576686689019.jpeg
 
Malipo ni hapa hapa duniani. Na hata maandiko matakatifu yatuambia; "Aliyeua kwa upanga naye atauwawa kwa upanga". Naam! Unaweza kuita karma ama vinginenevyo vyovyote vile. Angalia pande zote za dunia na historia yake uone ukweli na mantiki ya usemi huu. Suala ni muda tu, bali ncha ya upanga inasubiri shingo za watu dhalimu. Tubuni ili msamehewe mbele ya mbingu na hata mbele za macho ya wanadamu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Akikanyaga Airport tu, moja kwa moja gerezani Segerea
Umeshindwa kumkamata Mkapa aliyekiri kua utamkamata Lisu?
Umeshindwa hata kumuuliza jpm anayeita watngeneza ndege na kuagiza akiwa chumbani pake bila hata kudurusu sheria ya manunuzi utamkamata Lisu?

Umshindwa kumkamata aliyeuza nyumba za umma Kwa hawara zake utamkamata Lisu?
Umeshindwa kumkamata aliyepiga t 1.5 utamkamata lisu?
Wewe endelea kuitegemea dolla ikufanyie siasa tu huna lolote si ushawishi wala mbinu umekwama mzee
 
Hizo Risasi zilipiga hadi ubongo, "Arudi watengeneze nchi" Nchi gani labda?? ya ahadi? Wameshindwa kutengeneza tu ofisi na kumbi za mikutano ije kuwa nchi.
Wao waendelee na kikao chao cha Mwisho wa Mwaka cha SACCOSS kugawana faida

Sent using Jamii Forums mobile app

Una maanisha au umea ndika kwa sababu umeandika tu
Kwa nini tusiwe SERIOUS katika mijadala kama hii,maisha yetu yanaguswa na hii mijadala,therefore tuchangie vitu vya maana
Nb...ninaheshimu ulichoandika lakini sikubaliani nacho katu katu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Heshima ndogo ambayo nchi hii ilikuwanayo ilitoweka kabisa kufuatia matukio ya kidhalimu kama ya kushambulia na kujeruhi watu wenye mawazo tofauti na utawala wa kiimla.

Lkn dunia ya wastaarabu haiwezi kamwe kuvumilia upumbavu kama huu kwa hali yoyote ile.
 
Back
Top Bottom