Mwanamageuko
JF-Expert Member
- Oct 31, 2010
- 8,602
- 5,570
Kazi nzuri pongezi kwa polisi lakini je kama huyo Shafi ni lini alitoroka gerezani? Kwanini raia hatukutahadharishwa?View attachment 591778
Jeshi la Polisi kanda maalumu ya Dar es salaam limefanikiwa kuwaua Majambazi watatu na kuwakamata wengine wawili huko Vingunguti-Becco katika Mkoa wa kiporisi Ilala.
Taarifa hiyo imetolewa leo na Kamishina wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, SACP L.B Mambosasa alipokuwa akiongea na vyombo vya habari ofisini kwake makao makuu ya jeshi hilo.
Kamishina Mambosasa amesema kuwa Jeshi la Polisi limefanikiwa kuwaua na kuwakamata majambazi hao kutokana na taarifa zilizotolewa na wasamalia wema juu ya uhalifu uliopangwa kufanyika kwenyw moja ya maghara eneo la Tazara.
Katika taarifa yake, Kamishina Mambosasa amesema kuwa mnamo saa kumi na moja na dakika ishirini jioni Polisi walifanikiwa kuweka mtego na kulisimamisha gari aina ya Toyota Mark II lenye rangi ya bluu (namba zake hazikufahamika). Baada ya Majambazi kugundua kuwa waliosimamisha gari walikua Askari, majambazi hao walianza kuwashambulia askari kwa risasi hivyo askari kujibu mapigo na kuwajeruhi majambazi watatu.
Aidha, taarifa inasema kuwa majambazi hao wamegundulika kuwa ni wahalifu Sugu waliokwisha fanya matukio mbalimbali ya kihalifu katika jiji la Dar es salaam. Mmoja amejulika kwa jina moja la SHAFI, huyu alikua akitumikia kifungo cha miaka 30 jela kwa unyang’anyi wa kutumia silaha, wa pili ni Babu Jaffari ambae pia ameshiriki matukio mbalimbali kwa kutumia silaha na wa tatu ni Mbegu Maloni ambae ndie mtafutaji wa kazi za kwenda kupora (MasterPlan) likiwemo tukio hilo la Tazara.
Katika eneo hilo la tukio kumekutwa Bastora moja aina ya Browning, Risasi tatu ambapo moja ilikuwa chemba tayari kwa kufyatuka, maganda matatu ya Risasi zilizofyatuliwa kutoka katika Bastora ya Majambazi. Majambazi hao walifariki wakati wakipelekwa Hospital ya Muhimbili kwa matibabu baada ya kuvuja damu nyingi. Hata hivyo msako mkali unaendelea kumsaka jambazi alietoroka na gari hilo lililotumiwa na majambazi hao.
Wakati huohuo Jeshi la Polisi Kanda maalum ya DSM katika tarehe ya 16.09.2017, majira ya saa kumi na moja na dk hamsini jioni huko Makaburi ya Wangazija, Upanga limewakamata Rahma Almas@Baby miaka 37, mkazi wa Temeke Mkuranga B, Mohamed Maganga miaka 61, mkazi wa Pugu ambae pia ni Mlinzi na mfanya usafi katika makaburi hayo. Watuhumiwa hawa wamekamatwa wakiwa na Bunduki mbili aina ya UZIGUN na RIFFLE, Bomu la kurusha kwa mkono, risasi 162 za silaha aina ya Uzigun na risasi tano za Riffle.
Baada ya mahojiano mtuhumiwa Rahma Almas@Baby alikiri kuhifadhi silaha hizo zilizotumika ktk matukio mbalimbali a kihalifu ikiwemo mauaji ya WAYNE DERRICK LOTTER Mkurugenzi wa Palm Conservation Foundation, miaka 52 raia wa Afrika kusini alieuawa mwezi uliopita Masaki akitokea airport ya JNIA.
Katika tukio jingine Polisi Kanda maalum ya DSM wamewakamata watuhumiwa watano wa uvunjaji wa Ofisi ya Mawakili ya Prime attorneys iliyovunjwa tarehe 12.09.2017 na kuibiwa kasiki iliyokuwa na pesa Tsh.3,700,000/=, Laptop mbili na nyaraka mbalimbali za ofisi na za wateja. Prime attorneys ndio waliokuwa watetezi wa Yussuph Manji wakati wa kesi iliyokuwa ikimkabiro ya uhujumu Uchumi ambayo pia imefutwa tayari.
Watuhumiwa hao waliokamatwa sehem mbalimbali za Jiji la DSM baada ya msako mkali ni:-
1. Said Idrisa Salehe (47), mkazi wa Mbezi Luis.
2. Mustapha Ibrahim Said (35) mkazi wa Magomeni Mwembechai.
3. Somfi Uliza Somfi (52) mkazi wa Mahomeni Mapipa.
4. Iman Mbago Mhina (36) mkazi wa Kimara Mwisho.
5. Hussein Haji Suleiman (45) Mkazi wa Kigogo Mbuyuni.
Baada ya mahojiano watuhumiwa hao walikiri kuhusika na tukio hilo na kuonesha kasiki la fedha pamoja na mitungi mitatu ya gesi iliyotumika kukatia kasiki hilo. Upelelezi unaendelea ili kuwabaini watuhumiwa wengine walioshiriki tukio hilo.
Kamishina Mambosasa katika taarifa yake amesema kuwa Polisi Kanda maalum ya DSM kupitia kikosi chake cha usalama barabarani wameendelea na oparesheni ya ukamataji wa makosa ya usalama barabarani kwa kipindi cha kuanzia tarehe 15.09.2017 hadi tarehe 18.09.2017 kama ifuatavyo:-
Jumla ya Magari yaliyokamatwa 13,784
1. Pikipiki zilizokamatwa 392
2. Daladala zilizokamatwa 5,387
3. Magari mwngine binafsi na malori 8,397
4. Bodaboda waliofikishwa mahakamani kwa kutovaa Helmet na kupakia abiria mishikaki 22.
Jumla ya makosa yote yaliyokamatwa ni 14,176.
Pesa za tozo zilizopatikana ni Tsh. 424,620,000/=