Dar: Polisi waua watu wawili wakamatwa, wamekamata risasi zaidi ya 162

View attachment 591778

Jeshi la Polisi kanda maalumu ya Dar es salaam limefanikiwa kuwaua Majambazi watatu na kuwakamata wengine wawili huko Vingunguti-Becco katika Mkoa wa kiporisi Ilala.

Taarifa hiyo imetolewa leo na Kamishina wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, SACP L.B Mambosasa alipokuwa akiongea na vyombo vya habari ofisini kwake makao makuu ya jeshi hilo.

Kamishina Mambosasa amesema kuwa Jeshi la Polisi limefanikiwa kuwaua na kuwakamata majambazi hao kutokana na taarifa zilizotolewa na wasamalia wema juu ya uhalifu uliopangwa kufanyika kwenyw moja ya maghara eneo la Tazara.

Katika taarifa yake, Kamishina Mambosasa amesema kuwa mnamo saa kumi na moja na dakika ishirini jioni Polisi walifanikiwa kuweka mtego na kulisimamisha gari aina ya Toyota Mark II lenye rangi ya bluu (namba zake hazikufahamika). Baada ya Majambazi kugundua kuwa waliosimamisha gari walikua Askari, majambazi hao walianza kuwashambulia askari kwa risasi hivyo askari kujibu mapigo na kuwajeruhi majambazi watatu.

Aidha, taarifa inasema kuwa majambazi hao wamegundulika kuwa ni wahalifu Sugu waliokwisha fanya matukio mbalimbali ya kihalifu katika jiji la Dar es salaam. Mmoja amejulika kwa jina moja la SHAFI, huyu alikua akitumikia kifungo cha miaka 30 jela kwa unyang’anyi wa kutumia silaha, wa pili ni Babu Jaffari ambae pia ameshiriki matukio mbalimbali kwa kutumia silaha na wa tatu ni Mbegu Maloni ambae ndie mtafutaji wa kazi za kwenda kupora (MasterPlan) likiwemo tukio hilo la Tazara.

Katika eneo hilo la tukio kumekutwa Bastora moja aina ya Browning, Risasi tatu ambapo moja ilikuwa chemba tayari kwa kufyatuka, maganda matatu ya Risasi zilizofyatuliwa kutoka katika Bastora ya Majambazi. Majambazi hao walifariki wakati wakipelekwa Hospital ya Muhimbili kwa matibabu baada ya kuvuja damu nyingi. Hata hivyo msako mkali unaendelea kumsaka jambazi alietoroka na gari hilo lililotumiwa na majambazi hao.

Wakati huohuo Jeshi la Polisi Kanda maalum ya DSM katika tarehe ya 16.09.2017, majira ya saa kumi na moja na dk hamsini jioni huko Makaburi ya Wangazija, Upanga limewakamata Rahma Almas@Baby miaka 37, mkazi wa Temeke Mkuranga B, Mohamed Maganga miaka 61, mkazi wa Pugu ambae pia ni Mlinzi na mfanya usafi katika makaburi hayo. Watuhumiwa hawa wamekamatwa wakiwa na Bunduki mbili aina ya UZIGUN na RIFFLE, Bomu la kurusha kwa mkono, risasi 162 za silaha aina ya Uzigun na risasi tano za Riffle.

Baada ya mahojiano mtuhumiwa Rahma Almas@Baby alikiri kuhifadhi silaha hizo zilizotumika ktk matukio mbalimbali a kihalifu ikiwemo mauaji ya WAYNE DERRICK LOTTER Mkurugenzi wa Palm Conservation Foundation, miaka 52 raia wa Afrika kusini alieuawa mwezi uliopita Masaki akitokea airport ya JNIA.

Katika tukio jingine Polisi Kanda maalum ya DSM wamewakamata watuhumiwa watano wa uvunjaji wa Ofisi ya Mawakili ya Prime attorneys iliyovunjwa tarehe 12.09.2017 na kuibiwa kasiki iliyokuwa na pesa Tsh.3,700,000/=, Laptop mbili na nyaraka mbalimbali za ofisi na za wateja. Prime attorneys ndio waliokuwa watetezi wa Yussuph Manji wakati wa kesi iliyokuwa ikimkabiro ya uhujumu Uchumi ambayo pia imefutwa tayari.

Watuhumiwa hao waliokamatwa sehem mbalimbali za Jiji la DSM baada ya msako mkali ni:-
1. Said Idrisa Salehe (47), mkazi wa Mbezi Luis.
2. Mustapha Ibrahim Said (35) mkazi wa Magomeni Mwembechai.
3. Somfi Uliza Somfi (52) mkazi wa Mahomeni Mapipa.
4. Iman Mbago Mhina (36) mkazi wa Kimara Mwisho.
5. Hussein Haji Suleiman (45) Mkazi wa Kigogo Mbuyuni.
Baada ya mahojiano watuhumiwa hao walikiri kuhusika na tukio hilo na kuonesha kasiki la fedha pamoja na mitungi mitatu ya gesi iliyotumika kukatia kasiki hilo. Upelelezi unaendelea ili kuwabaini watuhumiwa wengine walioshiriki tukio hilo.

Kamishina Mambosasa katika taarifa yake amesema kuwa Polisi Kanda maalum ya DSM kupitia kikosi chake cha usalama barabarani wameendelea na oparesheni ya ukamataji wa makosa ya usalama barabarani kwa kipindi cha kuanzia tarehe 15.09.2017 hadi tarehe 18.09.2017 kama ifuatavyo:-
Jumla ya Magari yaliyokamatwa 13,784
1. Pikipiki zilizokamatwa 392
2. Daladala zilizokamatwa 5,387
3. Magari mwngine binafsi na malori 8,397
4. Bodaboda waliofikishwa mahakamani kwa kutovaa Helmet na kupakia abiria mishikaki 22.
Jumla ya makosa yote yaliyokamatwa ni 14,176.
Pesa za tozo zilizopatikana ni Tsh. 424,620,000/=
Kazi nzuri pongezi kwa polisi lakini je kama huyo Shafi ni lini alitoroka gerezani? Kwanini raia hatukutahadharishwa?
 
1. Hivi inakuwaje kila majambazi wakikamatwa wanafariki wakiwa njiani kuelekea hospitali?
Mkuu kama kuna msela unamjua mtu wa matukio mshauri aache,siku hizi hawaruhusu jambazi apelekwe hospitalini au mahakamani,tangu walipouwawa polisi wenzao wakishakuchukua maelezo wanakumalizia njiani wakiwa wanakupeleka hospitalini,huko nyuma jambazi alikuwa anafungwa baadae anakata rufaa anatoka halafu anaanza kusumbua mtaani tena,mambo ya upelelezi bado haujakamilika kwa majambazi hakuna tena.Na wanapukutika kweli,itafika wakati ujambazi utabaki 1% kama sio kuisha kabisa.
 
Hiiiv....siku zoote hawa majambaz wao hufa wakati wakiwa wanakimbizwa hospital?? Hakuna hata siku moja kwamba polisi walipiga risasi akafa hapo hapo???
 
View attachment 591778

Jeshi la Polisi kanda maalumu ya Dar es salaam limefanikiwa kuwaua Majambazi watatu na kuwakamata wengine wawili huko Vingunguti-Becco katika Mkoa wa kiporisi Ilala.

Taarifa hiyo imetolewa leo na Kamishina wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, SACP L.B Mambosasa alipokuwa akizungumza

Aidha, taarifa inasema kuwa majambazi hao wamegundulika kuwa ni wahalifu Sugu waliokwisha fanya matukio mbalimbali ya kihalifu katika jiji la Dar es salaam. Mmoja amejulika kwa jina moja la SHAFI, huyu alikua akitumikia kifungo cha miaka 30 jela kwa unyang’anyi wa kutumia silaha, wa

MLETA TAARIFA SIJAELEWA INA MAANA HUYU ANAETUMIKIA KIFUNGO CHA MIAKA 30 AKAKAMATWA NA UJAMBAZI .

HEBU WEKA TAARIFA YAKO VIZULI ISIJE UKAWA UMEJITUNGIA TUU
 
~~~>>>Kwa siku 3 tu Pesa za tozo zilizopatikana ni Tsh. 424,620,000/=......


Na hii ni kwa Daslam tu.....
 
Nilichokiamini kwenye hizi porojo za Mambo Kesho ni Tozo tu mengine yote ni soga za kujisifia ili kupoteza lengo.

Hatutaondoka kwenye sakata la Lissu mpaka wahusika watakapokamatwa.
Bado mnataka FBI? Kwa hiyo Tundulissu ni damu zaidi kuliko wanaCCM walioawa Kibiti au polisi waliouawa Sitakishari?
 
Kazi ya upelelezi ngumu sana au maelezo yamepungua? Wahalifu walikua kwenye gari, wakasimamishwa wakaanza kurushiana risasi, baadhi wakajeruhiwa na wamefariki wakiwa njiani kupelekwa kwenye matibabu.

Mnalifuatilia gari lenye wahalifu baada ya kutonywa na wasamaria wema, mnalizingira na kuanza kufyatuliana risasi. Baadae mmoja anatoroka na hilo gari

Namba za gari hazijajulikana....
porojo tu hakuna kingine, yaani majambazi mmewasimamisha wakagundua ni polisi katika kufyatuliana risasi(asa sijui walishuka kwenye gari) maana kama hawakushuka wangetoroka na aliye toroka na gari.

hawa wameingia studia kutengeneza movie, wiki majambazi waliovunja ofisi ya mawakili hawajagawana pesa japo wamefanikiwa kulikata sanduku la mkwanja

hollywood
 
Namna hiyo kazi nzuri. Ila nauliz majambazi wa siku hizi mbona wote hufia njiani wakipelekwa hospitali?
 
Kazi ya upelelezi ngumu sana au maelezo yamepungua? Wahalifu walikua kwenye gari, wakasimamishwa wakaanza kurushiana risasi, baadhi wakajeruhiwa na wamefariki wakiwa njiani kupelekwa kwenye matibabu.

Mnalifuatilia gari lenye wahalifu baada ya kutonywa na wasamaria wema, mnalizingira na kuanza kufyatuliana risasi. Baadae mmoja anatoroka na hilo gari

Namba za gari hazijajulikana....

Sasa mkuu kama wanaoenda kufanya kazi jeshi la polisi ni form four wenye division four, unatarajia wakitunga script zao zinakuwa na tofauti na bongo movie? Story ina maswali mengi sana
 
Kuna mijitu kazi yao ni kuponda tu, sijui ilipewa semina kwamba chochote mtakachoona pondeni tu,
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom