Dar Ndio Imekuwa hatari hivi?

Dar Ndio Imekuwa hatari hivi?

pole sana kaka.
Hilo eneo lina shida,nilisikia kuna gari ilipigwa pini na Noah kwa mbele na bodaboda kulia na kushoto,wakashuka jamaa na kushambulia kwa mapang. kama hivyo.
Huo mtandao uvunjwe haraka sana.
 
Kuna siku nilikuwa natoka kumpokea mtu airport ndege ilifika saa tatu hadi kuondoka pale ilikuwa saa nne hivi. Tulivyoondoka kuna taxi nayo ilibeba wazungu wameshuka na ndege hio hio tukawa tunaongozana. Wao walikuwa wameacha vioo wazi.
Kufika hapo Kamata tumesimama kwenye traffic lights wakatokea vijana kama nane hivi wakawavamia na kuwapora vitu, process ilichukua kama dakika mbili tu wale vijana wakatokomea upande ambao sasa ipo Mkuki Mall.
Kosa la hawa watu ni kuacha vioo wazi na kuto-lock milango baaasi.
 
Get well soon ... u should take care ...due to policcm they don't care anyone but wanawaza tareh 26 ..to kill innocent people.
Mbona unaleta vitu vya kipuuzi? How sure you are that police do not care?
In which country on this earth do such things never happen, are there no police men in those countries??
 
Sijajua kama ulikuwa na gari ama la, lakini iko hivi, hakikisha kama unaendesha gari uwe umefunga vioo vyote na umeweka lock za milango, wapo wanaojisahau kuweka lock za milango, epuka kushika simu gari inapokuwa imesimama, hii unajenga mazingira ya vishawishi kwa muhalifu kukushambulia, iwapo hauna gari epuka kutembea sehemu ya giza ama kuongozana na watu usiowafahamu na ukawa uko karibu yao, weka mazoea ya kumtumia dreva unayemfahamu akufate eneo lako la kazi kama usiku umeenda sana, hii ni kuanzia saa moja usiku na kuendelea. Maeneo hatarishi ni mengi sana kwa Dsm, usiamini kokote kwa kipindi hiki cha uchumi kuwapindia watu, hapo mbeleni uhalifu utazidi sana maana wahusika ambao ni polisi ni kama wameliweka pembeni swala la kuwadhibiti waporaji na zaidi nguvu zao wamezielekeza kudhibiti raia asiye hata na silaha.
Pole sana mkuu.
 
Mbona unaleta vitu vya kipuuzi? How sure you are that police do not care?
In which country on this earth do such things never happen, are there no police men in those countries??
My be was Green guard
 
Back
Top Bottom