Alikuwa hajasikia tangazo la Polisi la mwisho kutoka nje saa 12 jioni, akaenda kununua mkate...
Majirani wanasema mtoto alilia juice akaenda kumnunulia, akapigwa risasi kifuani.
Marehemu alikuwa nyumbani kwake, Mbezi Luis.
Hadi jana jioni, bado mwili ulikuwa uko chumba cha kuhifadhia maiti.
====================
Mwanahabari Maneno Selanyika ambaye aliwahi kuwa Mwandishi wa Habari katika Media tofauti ikiwemo New Habari amefariki Dunia kwa kupigwa shaba wakati wa mbilinge la maandamano lililodumu kwa siku kadhaa hapa TZ kuanzia siku ya Uchaguzi Mkuu Oktoba 29, 2025.
Taarifa kutoka katika magroup ya WhatsApp zinaeleza Maneno Selanyika alikuwa hajasikia tangazo lililotolewa na Jeshi la Polisi kuwa hakuna raia anayetakiwa kutoka nje kuanzia Saa 12 Jioni wakati wa maandamano hayo.
Inaelezwa kuwa alitoka kwenda kununua mahitaji dukani kwa ajili ya mtoto wake maeneo ya Mbezi Luis Jijini Dar, akakutana na shaba ya kifua na kwamba mwili wake bado haujazikwa hadi leo tarehe nne Novemba 2025.