Dar: Mkutano wa Baraza Kuu la CHADEMA, uamuzi wa rufaa ya kina Mdee, Bobi Wine yupo

View attachment 2220462
Halima Mdee na wenzake 18 wakiwa chumba maalum kilichoandaliwa wakisubiri kusikilizwa kwa rufaa zao kupinga kufukuzwa unachama. Rufaa hizo zinasiiilizwa na wajumbe wa Baraza Kuu la CHADEMA, Ukumbi wa Mlimani City Dar es Salaam. Wamesema wako tayari kwa lolote.

View attachment 2220248

Kuwa wa kwanza kufahamu kwamba kile kikao kikubwa kabisa cha maamuzi Kikatiba cha CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA), leo 11/5/2022 kinafanyika ndani ya Ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam.

Kikao hiki ni cha kawaida cha chama hicho na ambacho hufanyika angalau mara moja kwa mwaka, ndani ya kikao cha leo ajenda kadhaa zitajadiliwa ikiwemo Dira ya Chama hicho kuelekea 2025, pamoja na suala Muhimu la KATIBA MPYA na TUME HURU YA UCHAGUZI, limo pia suala dogo la Rufaa za waliokuwa wanachama wa chama hicho WALIOFUTWA UANACHAMA NA KAMATI KUU KUTOKANA NA USALITI

Tayari Wajumbe wamekwishaingia ndani ya Ukumbi huku wengine wakiendelea kumiminika , Ulinzi wa VIP PROTECTION ni wa Uhakika .

Maajabu ni kwamba baadhi ya vyombo vya habari vya Tanzania vimeanza kurusha matukio hayo moja kwa moja , ikiwemo Clouds TV , jambo ambalo ni jipya mno kwa siasa za Tanzania.

Wabunge 19 Wakuja kusikiliza hatma yao

Endelea kufuatilia Taarifa za Baraza hili Muhimu hapa hapa JF

Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, James Mbatia, Viongozi wa dini wakiongozwa na Askofu Emmaus B Mwamakula, Mwenyekiti wa ACTwazalendo, Juma Duni, wachambuzi wa siasa, Jenerali Ulimwengu na mwanasiasa Hashim Rungwe wameshawasili ukumbini.

Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe ameongozana na mgeni wake ambaye ni kiongozi wa upinzani nchini Uganda, Robert Kyagulanyi (Bobi Wine) wameshawasili.

Jenerali Ulimwengu anazungumza:
“Chadema ni mojawapo ya nguzo muhimu ya demokrasia katika nchi hii, imejipambanua na vyama vingine kwa kufanya siasa ya kweli, siasa ya kweli ni kuzungumzia masuala yanayowahusu wananchi.

“Wakati mwingine wanakosoa watawala, wafanyabiashara au hata wahuni tu wa mtaani, pamoja na kuonyesha njia.
Juma Duni, Mwenyekiti wa ACT Wazalendo:
"Safari ya vyama vya siasa nchini ni moja na lengo ni kupata mabadiliko chini ya katiba mpya na tume huru.”

"Sote vyama vya upinzani kwa pamoja tuna nguvu ya pamoja inayotusukuma kudai katiba mpya na tume huru, hatuna haja kutengana katika hili.

"Tunaposema People's power hiyo power sio yetu sisi viongozi, bali ni power inayotoka nyuma ya watu wetu na hao ndio wanaotaka katiba mpya.”

"Vyama vya siasa tukiwa wamoja dola itatusikiliza, tukitengana dola itatucheka, nina miaka 30 katika siasa, nikipigania katiba mpya na tume huru. Tuwe wamoja.

Bobi Wine anaungumza
"Nisisahu kujitambulisha kwenu kuwa, mimi ndiye Rais wa Uganda ambaye nilichaguliwa na watu wa Uganda.

"Pamoja na kuwa katika maeneo tofauti ya kijiografia lakini mambo tunayoyapitia katika siasa yanafanana.

"Kwa mara ya kwanza ilibidi mgombea urais nchini Uganda katika uchaguzi mkuu nchini humo kuvaa kifaa cha kuzuia risasi, na ni uchaguzi uliomwaga damu nyingi za raia wema.

"Timu yangu ya kampeni iliyokuwa na watu takribani 130 walizingirwa na kukamatwa na kukaa jela kwa miezi 7. Pamoja na mazingira hayo yote ulikuwa ni uchaguzi ambao watu wa Uganda walishinda.

"Nawapa salamu kutoka kwa watu wa Uganda, ambao hawajakata tamaa na hawataacha kupaza sauti kwa mambo ambayo hayaendi sawa. Nadhani hilo halina tofauti sana na hapa Tanzania.

"Kama hauwezi kujifunza kwa yaliyotokea huko nyuma, huwezi kutengeneza njia nzuri huko mbele unapokwenda."

"Wakati Rais Yoweri Museveni anachukua madaraka kwa mara ya kwanza, mimi (Bob Wine) nilikuwa nina miaka minne, na sasa nina miaka 40 huku Rais Museveni akiwa hana mpango wa kustaafu.

"Pamoja na yote yanayoendelea Uganda lakini tuna katiba nzuri ambayo naweza kusema kuwa ni moja ya katiba bora Afrika lakini haiheshimiwi.

"Hata inapotokea Museven amekuwa akibadilisha mara kwa mawa katiba lakini bado ipo vizuri, sheria za Uganda ni nzuri zikiwa kwenye makaratasi tu.
Je wewe hutaki kujua ukweli mbona uku hiyo
20220210_042641.jpg

Sent from my SM-A307FN using JamiiForums mobile app
 
Wakuu nafuatilia live kupitia clous tv na naona matangazo yanakatakata sana kila saa mziki. Kaka kuna chanel ingine inarusha tafadhali nisaidieni
 
Leo ndio mwisho wa hicho ki saccos chenu.
Muulize mzee wassira aliyesema kuwa saccos haifiki 2020 kuwa yeye na saccos nani hakufika 2020 kisiasa? Kuna mwingine alisema atafuta upinzani kabla ya 2020, ajabu akafutika yeye na kuacha upinzani unataradadi
 
Kikao kisicho na dira Wala mwelekeo leo ndiyo chadema wanaenda kujivua nguo Bora wawahoji kwenye vyumba hao kina mdee wakiwahoji hadharani ni aibu kwa mbowe na wenzake maana wanaenda kusema ukweli wa wakiowapeleka
ni ukweli kuwa mbowe ndio alitoa amri mbunge atoke lockup usiku aende dodoma kuapishwa????
 
Kama wakitubu madhambi yao naona wasamehewe, kwani mkuu wa aliyewalaghai hayupo nasi leo na wao wenyewe wamejifunza kitu kwamba CDM haiwezi kufa kwa propaganda za kitoto kama hizo.

With a condition wavuliwe nyazifa zao zote ndani ya chama, na wawe tayari kukitumikia chama kwa moyo wote pia wakae katika kipindi cha uangalizi wa miaka 2 hadi 2024.

Hakuna kosa lisilosamehewa, cha msingi ni wao KUTUBU kama Yesu kristo alivyotuangiza sisi KUSAMEHE hawa wengi wao ni mabinti hawajajua maisha hasa ya kisiasa katika ukomavu wake.
 
Hawawezi kuwasamehe.
 
Mmeanaza kulegea.
 
Back
Top Bottom