DAR LUX yadhalilisha abiria wake

DAR LUX yadhalilisha abiria wake

Hii ndio Tanzania kila mtu akili zake!
 
Hili swala la gari kutokupumzika kwa hapa Tz ni kawaida. Haswa kwa wamiliki wenye magari machache.....Gari inatoka Dar inafika Mwanza usiku. Kesho yake gari hiyo hiyo inageuza Dar ikiwa na madereva wale wale.
 
Wakuu hii mada yenu nimeifikisha kwenye group letu la wana dar lux(blue) whatsapp kwa kuwa wahusika wako kule nahakika watatupa majibu mazuri na ni watu wasio ficha na pia madereva wao pia wako kule watatoa majibu juu ya hii tuhuma
Mkuu hebu fikisha na hili.

Kuna Dar Lux inayokwenda Tunduma (Mimi nilipanda Jumatatu ya tarehe 10/10/2016 namba ya gari ni T568 DCW sina uhakika sana na hizi namba za mwisho CW sababu zimekorogwa sana kwenye tiketi hapa) gari ilifika Mbeya mida ya 2+ usiku lakini tulipofika nane nane mhudumu akatangaza kwamba hatosimama kituo kingine chochote mpaka Mbeya stand. Cha ajabu hawakuingia stand na sisi tulikuwa wageni Mbeya tukajikuta tunashushiwa Mbalizi baada ya abiria wazoefu kutuambia tulishapita Mbeya. Kumuuliza muhudumu akatuambia siku hizi gari za Tunduma hazingii Mbeya stand, tukamuuliza kwa nini aliatangaza wataingia stand na wakafanya kinyume chake? tukamuuliza tena kwa nini asingetangaza kwamba watu wanaoshukia Mbeya watawashusha angalau hata Simike? Matokeo yake akatujibu utumbo mtupu.

Mbali na changamoto hiyo huduma zao za ndani ya basi zilikuwa nzuri sana na hata kurudi tulirudi pia na basi ilo ilo. Warekebishe ilo tu.
 
Cyo kwenda nakugeuza kwa maana ya mchana mmoja, nikwamba mfano gari linatoka Mza asbh j'mosi linafika dar saa saba usiku afu kesho yake asbh gari hilo hilo lirudi Mza huko ndiko namaanisha, lkn pia muda wa mabasi kuondoka stendi ni saa 12 kamili na abiria wanakuwa hapo saa moja kabla ya muda, hivyo kukaa mpaka saa moja kasoro unaweza kuiona taharuki niliyosema
Sasa abiria wanadhalilika vipi??...

Umesema Dar Lux wanadhalilisha abiria wao...Sijakuelewa
 
Mtoa mada eleza vizur abiria wamedhalilishwaje? Kwan wanazunguka na gari au wao wakifika gari inageuza na wengine!
 
Mabasi ya DAR LUX yafanyayo safari zake ktk baadhi ya mikoa hapa nchini imejikuta ikidharirisha abiria wake baada yakuonekana inapendwa na abiria wengi. Uongozi wa compuni hiyo umejikuta unaingiwa tamaa nakujikuta inalazimisha madereva wake kufika nakugeuza siku hiyo hiyo bila kujali umbali wa safari anayoenda ( yaani go and return) bila kupumzika kwakuwa wapo wawili ktk kila gari. Hali hiyo leo imesababisha Dereva kusinzia mpaka saa moja kasorobo nakuibua taharuki kubwa kwa abiria wa gari Na.2 la Dar-Mza.Hizo ni taarifa nilizozipata kwa mmoja wa wafanyakazi wakampuni hiyo ambae chonde ameomba kuhifadhi jina lake. Kwa mujibu wa bwana huyo ameongeza kusema hata ujira wa madereva wake hauendani na umbali wa safari za Mza tena kwa kwenda nakugeuza.Tuwaombe mamlaka zinazohusika na safari za mabasi kuchunguza hilo swala kwakuwa ni la hatari kwa usalama wa abiria na madereva wake

Siku zinavyozidi kwenda janga la kushindwa kujieleza linaendelea hapa bongo
 
Cyo kwenda nakugeuza kwa maana ya mchana mmoja, nikwamba mfano gari linatoka Mza asbh j'mosi linafika dar saa saba usiku afu kesho yake asbh gari hilo hilo lirudi Mza huko ndiko namaanisha, lkn pia muda wa mabasi kuondoka stendi ni saa 12 kamili na abiria wanakuwa hapo saa moja kabla ya muda, hivyo kukaa mpaka saa moja kasoro unaweza kuiona taharuki niliyosema

Jambo ambalo umeshindwa kulieleza hapo mwanzo
 
Basi au gari haliangushwi, narudia haliangushwi, bali LINAANGUKA.
Ili uliangushe umepaswa kuwa nje ya basi husika u apply force against the said object.
Unaonekana shuleni ulikuwa unakaba waalimu wewe.
Biniadamu anapaswa kulala masaa mangapi, wanaanza safari saa ngapi na wanatakiwa kulala ikifika saa ngapi.
Usitake kutuambukiza ujinga!!!
Umaanishe eti uingie kazini leo kesho upumzike kwa kuwa unafanya kazi kwenye kiwanda cha nondo!!! Hiyo ndiyo kazi yake, tena wako wawili, wanapokezana, hawapaswi kuendesha kupita 80kph.
Udundulizaji wa abiria ndio kigezo cha kulaza bus!! Kinyume chake linatakiwa lizunguke lilipe mkopo.

kwa hiyo gari linaweza kuanguka au kupata ajali kama halijaendeshwa. yaani gari liwe limepaki halafu lianguke lenyewe au ligongane na kuua watu
 
Hii ndio Tanzania!
Mtoa mada anataka Gari lipumzike! Kwa hiyo toka saa saba usiku mpaka saa kumi na mbili lalipoondoka lilikuwa linazurura Mwanza nzima?
 
Kuna kaugonjwa fulani watu wanaumwa humu,si kila mtu mwandishi wa habari.Yeye anamahanisha madereva wapumzike sio wakifika saa saba uck saa kumi na moja waanze tena safari na gari ile ile na madereva wale wale.Kesho wakiangusha magar mnajazana humu kuwatukana madereva.Hii nchi ina mapunguani wengi.
 
kwa hiyo gari linaweza kuanguka au kupata ajali kama halijaendeshwa. yaani gari liwe limepaki halafu lianguke lenyewe au ligongane na kuua watu
Usiwe mgumu kuelewa!
Dereva anachofanya ni kukamilisha mfumo wa gari kutembea, akiipa umeme starter itazungusha ingine, mfumo wa vilainishi ukiwa sawa ingine itazunguka (dereva hazungushi crankshaft kwa mikono yake) pump itawaka sambamba na sterter, itasukuma mafuta kwenda kwenye combustion chamber ambako piston zitafanya ule mkandamizo kwenye block ingine na nguvu itatengenezwa pale, (hii nguvu hatengenezi dereva)
Likiwaka dereva ataunganisha (mfumo) ingine na gearbox, hapo hapo gari litaanza kujongea.

LINAJONGE KUELEKEA MFUMO UNAVYO SUPPORT.

Anachofanya dereva ni kulielekeza kimfumo lijongee kwa mwelekeo anaoutaka.

Wakati linajongea mfumo umepaswa kuwa supportive kuufanya mjongeo kuwa sustainable.

Kwa mfano wakati wa kujongea tairi likachomoka ina maana mfumo wa gari unashindwa ku surport acceleration na gari litaanguka!! (dereva) hawi ameliangusha.

Au dereva akilielekeza gari korongoni halikadhalika hawi ameliangusha yeye, bali korongo litakuwa ni gape kwenye mfumo ku surport acceleration hivyo litaanguka lenyewe.

NAAMINI NIMEELEWEKA
 
Hujaeleweka
Dereva kusinzia mpaka saa moja kasoro robo, ina maana akiwa katika usukani au ofisini kwao?
aliyekuletea habari hdizo muambie awasiliane na namba za SUMATRA zipo katika kila Basi la abiria kioo cha pili toka kiti cha ereva,
Au awasiliane na Chama cha abiria CHAKUA wapo Stand ya Ubungo, Msamvu, Stabd ya Mkoa Dodoma, hata huko Mwanza hawa CHAKUA simu zao zinawasiliana na Traffic Makao Makuu, Traffi wa barabarani wote mikoani, na SUMATRA pia wana Whatsapp/
Kama Basi linageuza na Madereva wanabadilishana, sioni tatizo ila kama Basi ni bovu au kujaza abiria na kuwasimamisha waripoti

Hata wewe hueleweki! ungetoa namba za hao unaotaka awapigie, sio kumwambia eti azisome ktk kioo cha gari, unadhani yupo humo kwenye gari tu anangoja nini?
 
Kama mtoa mada unawasemea madereva na wafanyakazi wa kwenye gari kuwa wazi na urekebishe kichwa cha habari ila ukisema abiria wanadhalilishwa unakosea na ni upotoshaji
 
Basi alitakiwa aseme hivyo mana alikuwa anakitu cha muhimu ila uwasilishaji ndo kachemka...ila Dar Lux wapo vizuri lakini kuna mikokoteni kama Najimunisa,Green Star(sijui bado lipo)..haya si ya kujiroga kupanda safari ya Mwanza
Mkuu mara ya mwisho umesafiri lini?
 
Usiwe mgumu kuelewa!
Dereva anachofanya ni kukamilisha mfumo wa gari kutembea, akiipa umeme starter itazungusha ingine, mfumo wa vilainishi ukiwa sawa ingine itazunguka (dereva hazungushi crankshaft kwa mikono yake) pump itawaka sambamba na sterter, itasukuma mafuta kwenda kwenye combustion chamber ambako piston zitafanya ule mkandamizo kwenye block ingine na nguvu itatengenezwa pale, (hii nguvu hatengenezi dereva)
Likiwaka dereva ataunganisha (mfumo) ingine na gearbox, hapo hapo gari litaanza kujongea.

LINAJONGE KUELEKEA MFUMO UNAVYO SUPPORT.

Anachofanya dereva ni kulielekeza kimfumo lijongee kwa mwelekeo anaoutaka.

Wakati linajongea mfumo umepaswa kuwa supportive kuufanya mjongeo kuwa sustainable.

Kwa mfano wakati wa kujongea tairi likachomoka ina maana mfumo wa gari unashindwa ku surport acceleration na gari litaanguka!! (dereva) hawi ameliangusha.

Au dereva akilielekeza gari korongoni halikadhalika hawi ameliangusha yeye, bali korongo litakuwa ni gape kwenye mfumo ku surport acceleration hivyo litaanguka lenyewe.

NAAMINI NIMEELEWEKA
bado wewe ni mbumbumbu kama dereva ataendesha pasipo uangalifu ajali itatokea vipi? gari halijiongozi ila linaongozwa na dereva huyo ambaye anafika mwanza akiwa amechoka na kuamka na usingizi
 
Mabasi ya DAR LUX yafanyayo safari zake ktk baadhi ya mikoa hapa nchini imejikuta ikidhalilisha abiria wake baada yakuonekana inapendwa na abiria wengi. Uongozi wa kampuni hiyo umejikuta unaingiwa tamaa na kujikuta inalazimisha madereva wake kufika na kugeuza siku hiyo hiyo bila kujali umbali wa safari anayoenda ( yaani go and return) bila kupumzika kwa kuwa wapo wawili ktk kila gari.

Hali hiyo leo imesababisha Dereva kusinzia mpaka saa moja kasorobo na kuibua taharuki kubwa kwa abiria wa gari Na.2 la Dar-Mza.Hizo ni taarifa nilizozipata kwa mmoja wa wafanyakazi wa kampuni hiyo ambaye chonde ameomba kuhifadhi jina lake. Kwa mujibu wa bwana huyo ameongeza kusema hata ujira wa madereva wake hauendani na umbali wa safari za Mza tena kwa kwenda nakugeuza.

Tuwaombe mamlaka zinazohusika na safari za mabasi kuchunguza hilo swala kwa kuwa ni la hatari kwa usalama wa abiria na madereva wake

Mie nimesafiri na Dar Lux Ni mazuri sana km yanayoelekea nairobi ,
Acheni kuchafua kampuni nzuri, usb cable kila kiti zinazofanya kazi sio magumashi km mabasi mengine,
 
Back
Top Bottom