Dar Lux kapotezwa?

Nahisi inachosha akili, wengine wanaamua kupumzika baada ya kuhakikisha pesa yake imerudi, lakini kuna wengine wanapata hasara, ni kama biashara ya aviation, kuna kampuni zinafunga miezi ni hasara tupu, aisee..
 
That explains it. Haiwezekani wengine wote wafe ukasema hawajui wanachokifanya there's more to it. Hii ni biashara kichaa kuliko zote.
Hii biashara sio poa niliwahi kuwa na mazungumzo na bosi wa zilizokuwa basi za Hekima zilitamba sana miaka ya 2000 mwanzoni route ya Dar-Mbeya-Tunduma.

Akaniambia msione vyuma tu vinapita barabarani ila mjue wakurugenzi wa mabasi wote tuna sonona

Mara ya mwisho niliona kawekeza zaidi kwenye usafirishaji wa malori, mabasi alipiga chini
 

Nazikumbuka Hekima. Mabasi huwa yana timeframe ya miaka miwili kabla ya kupotea kwenye ramani.
 
Hati za yule mjane...na machoziye....hilo ndo jibu
 
Hakika BANK haipo kwa ajili ya kusaidia mtu
 
Niliwahi kufanya interview na mmiliki wa hizi chuma. Full confidence. Nn kimetokea? Uchawi? Alilewa sifa? Customer care? Nchi nyingine hawa wafanyabiashara husaidiwa maana hutengeneza ajira Ila hapa, mpaka utoke damu masikion ndo TRA wakuachie

Hii biashara hakuna anayeweza kufanikiwa nayo tatizo kubwa likiwa Serikali na wafanyakazi.

1. Serikali - polisi, tra, latra, tanroads, TBS nk. Humu kuna usumbufu pasua kichwa kodi, tozo, rushwa na kila aina ya uhuni ikiwamo bidhaa fake.

2. Wafanyakazi wakiwamo madereva, Makonda, wasimamizi, mafundi fake. Wizi wizi na kutowajibika.

Mawili haya kwa Tanzania hii hata kama ungekuwa malaika sahau kufanikiwa.

Sana sana upumue pumue kwa muda ukiwa mbunge, waziri au kwa kuwa na mamlaka au access na connections za kutosha serikalini.

Ndiyo maana kila siku inaendeshwa na wawekezaji wapya ambao nao huwa hawadumu.
 
Utafika mbali wanaoendelea ni wasio na mikopo unakuwa na real capital
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…