Dar kupata huduma ya Internet/Wi-Fi bure

Dar kupata huduma ya Internet/Wi-Fi bure

Mr Hero

JF-Expert Member
Joined
Jun 11, 2015
Posts
5,540
Reaction score
7,464
wifi.jpg


Makamu wa rais nchini Tanzania Samia Suluhu Hassan amezindua mradi wa kuweka huduma ya mtandao wa Wi-Fi katika maeneo ya umma na yale ya burudani mjini Dar es Salaam.

Utekelezaji wa mradi huo wa kampuni ya mawasiliano nchini humo utapanua huduma za mawasiliano ili kuweza kuwafikia watu wengi zaidi na hivyobasi kuimarisha uchumi.

''Tunawapongeza kwa kutekeleza mradi huu na tunatumai upandaji wa miti katika maeneo tofauti mjini ikiwemo maeneo ya burudani,watu wataweza kupata huduma ya mtandao'' ,alisema.

Kwa upande wake Kamishna wa Jimbo la Dar es Salaam Paul Makonda amesema kuwa mradi huo ni mmoja wa awamu tano za juhudi za serikali kuimarisha huduma kadhaa hususan mawasiliano na huduma za mtandao kwa wote.

Utekelezaji wa mradi huo ndio mwanzo wa safari ya kujenga miji na miji mikuu katika kiwango cha 'Smart City'.
======

WADAU, HILI LILISHAWAHI KUHOJIWA HAPA JAMIIFORUMS;
Huwa najiuliza ili kuweza kuwa na free Wi-Fi, mfano kwenye vyuo vyetu au maeneo yetu sehemu mbalimbali, nini kinatakiwa kifanyike? Nchi zingine wamewezaje? Ni lazima serikali ishiriki? Wadau binafsi wakiamua wafanye ni ghali sana?

Humu kuna watu mnauelewa zaidi hebu tuelewesheni..

Soma: Free Wi-Fi: Nchi zingine wamewezaje?
 
Inatakiwa huduma za Internet. Serikali iwekeze sana maana ni sehemu ambayo dunia ndio apo ipo. Na makampuni mengi ya mawasiliano yanapata faida kubwa kutokana na gharama za data kuwa juu sana
 
wanahisi vijana hawataweza kumudu bando nini wanataka wawape bure sasa ili wachochee vizuri
 
Malaika wakija watakuta tayari kuna Wi-Fi sasa hapo sijui itakuaje! [emoji56] [emoji56] [emoji56] [emoji56]
 
Makamu wa rais nchini Tanzania Samia Suluhu Hassan amezindua mradi wa kuweka huduma ya mtandao wa Wi-Fi katika maeneo ya umma na yale ya burudani mjini Dar es Salaam.

Utekelezaji wa mradi huo wa kampuni ya mawasiliano nchini humo utapanua huduma za mawasiliano ili kuweza kuwafikia watu wengi zaidi na hivyobasi kuimarisha uchumi.

''Tunawapongeza kwa kutekeleza mradi huu na tunatumai upandaji wa miti katika maeneo tofauti mjini ikiwemo maeneo ya burudani, watu wataweza kupata huduma ya mtandao'' ,alisema.

Kwa upande wake Kamishna wa Jimbo la Dar es Salaam Paul Makonda amesema kuwa mradi huo ni mmoja wa awamu tano za juhudi za serikali kuimarisha huduma kadhaa hususan mawasiliano na huduma za mtandao kwa wote.

Utekelezaji wa mradi huo ndio mwanzo wa safari ya kujenga miji na miji mikuu katika kiwango cha 'Smart City' nchini Tanzania.

========

KAMPENI YA MTIWANGU YAJA NA NEEMA HII ILALA
Ikiwa ni Octoba Mosi siku ambayo, imeshuhudiwa maeneo mbalimbali ya Jijini Dar es Salaam na Wilaya zake tano za Temeke, Ilala, Kinondoni, Ubungo na Kigamboni yakitekeleza agizo la Mkuu wa Mkoa huo Paul Makonda katika suala zima la upandaji wa Miti kupitia kampeni yake ya Mtiwangu.
Kampeni hiyo ambayo imezinduliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu, imeambatana na jambo lingine ambalo litawanufaisha wakazi wa Ilala na watanzania kwa ujumla. Akizungumza juu ya suala hilo Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema ameelza kuwa kwa kushirikiana na kampuni ya mtandao wa simu ya TTCL wameweza kuweka ‘Internet’ ya bure kwa wakazi watakao kuwa wanaotembelea maeneo yenye bustani kubwa za mji, jambo litakalo wasaidia kupata taarifa mbalimbali zenye kuelimisha na kuwasiliana kupitia mitandao ya kijamii, ambapo Mkurugenzi wa TTCL Waziri Kindamba ameasema zoezi hilo halitakuwa la kusuasua kwani wamejipanga kufanya mapinduzi ya kimtandao na kuongeza kuwa Tanzania inakuwa nchi ya Tatu Afrika Mashariki kwa kufanya hivyo ikiungana na Kenya, Uganda, huku kwa Afrika ikiwa ya Tano zikiongezeka Nigeria na Afrika Kusini.
DC-MJEMA-MITI-ILALA-13.jpg

Kwa upande wake Makamu wa Rais amepongeza uwepo huo wa ‘Internet’ (WiFi) kwa maeneo yenye bustani ikiwemo NBC, Palm Beach, Mnazi Mmoja na Gymkana ambapo uzinduzi huo ulifanyika, huku akisisitiza suala la kutunza mazingira na upandaji miti liwe endelevu, kwani hali ya hewa ya Dar es Salaam imekuwa ya joto kutokana na athari za Mazingira, hivyo ameziagiza Wizara zinazosimamia Misitu na Mazingira kuzifuatilia bustani zote zilizopandwa miti siku ya leo.
 
Gusa unaswe

JPM anatamani mitandao malaika aje aizime mitandao wakati Makonda ye anazindua ya bure......kazi ipo !
 
Back
Top Bottom