Dar kupata huduma ya Internet/Wi-Fi bure

Dar kupata huduma ya Internet/Wi-Fi bure

Hii habari kwa wale HACKERS kitaani na Maghetoni itakua ni "Habari njema" maana Kuna WASHAMBA kibao wa DIGITAL especially dada zangu yaan Yeye anachojua ni Apige kapicha kake akatupie Insta basi hapo ndio mwisho wake so watalizwa wengi tuu
🙄🙄🙄🙄 Yetu macho maana SEREKALI YETU KWA KUTURUSHA ROHO ZETU HAWAJAMBO!!!!!!!!!!
 
Hebu wale mnaoishi mitaa ya simu2000 aka mawasiliano mtupe news kuhusu ile free Wi-Fi bado ipo?
 
UTANGULIZI.
Siyo kila sehemu kuna Wi-Fi,sehemu nyingine hazina Wi-Fi.Utajua kama hii sehemu ina Wi-Fi kwa kuona kialama cha Wi-Fi kwenye screen yako,kujua hii sehemu kama ina Wi-Fi au haina lazima uturn Wi-Fi on,ikishakuwa ON hapo ndiyo utajua kama hapa kuna Wi- Fi au hakuna.Sehemu isiyo na Wi-Fi hautaona kialama cha Wi-Fi,na sehemu yenye Wi- Fi utakiona kialama cha Wi-Fi.Sehemu zenye Wi-Fi nyingi ni mijini,yaani stendi za daladala,kwenye maofisi,mahoteli,migahawa n.k,ili mradi iwe mjini.
Baada ya kufika mjini ukiwasha Wi-Fi yako usikae kitako sehemu moja,unaweza kata tamaa kwamba nimeenda mjini nikawasha Wi-Fi halafu sijapata Wi-Fi,kumbe kosa ni la kwako la kukaa kitako sehemu moja,jaribu kutembea barabarani mjini pembezoni mwa maofisi,stendi,mashule,mahoteli.Sasa ukishakuwa unatembea mjini barabarani,hakikisha unaangalia kwenye screen yako iliyo na Wi-Fi on,hapo utaona vialama vya Wi-Fi,kuna Wi-Fi nyingine private,hizi kuzitumia huwezi kwa sababu lazima uwe na password ya hiyo Wi-Fi,utazijuaje private Wi-Fi?,zenyewe zinakuwa zina vikufuli.Wi-Fi nyingine ni public Wi-Fi,hizi ndiyo unaweza kuzitumia,utazijuaje?,zenyewe zinakuwa hazina alama ya vikufuli,maana yake hazina haja ya password.
JINSI YA KU-TURN ON Wi-Fi
Nenda settings,halafu nenda Wi-Fi,ukishakuwa kwenye Wi-Fi chagua options,halafu enable on.
UNAANZAJE KUTUMIA Wi-Fi?
Ukiishaichagua public Wi-Fi unayotaka,kwa simu za touch,long press hiyo Wi-Fi,itakuja options,halafu chagua connect Wi-Fi.Kwa simu za button,chagua options,halafu connect Wi-Fi.
N.B: Wi-Fi nyingine vifurushi vinakuwa vimeisha(nimetumia lugha hiyo ili nieleweke),kwa hiyo kifurushi kikiisha hautoperuzi internet hapo,itaload mpaka itakata yenyewe,ukiona hivyo kwenye hiyo Wi-Fi achana nayo tembea kwenye Wi-Fi nyingine.
Enjoy Wi-Fi
Ok thank dear
 
Hdmi huwezi kuunga kwenye simu, ni cable inatoka kwenye pc kwenye tv baadhi simu zinazo cable za HD Lakini sidhani kama inawezekana kuweka kwenye tv na ukatazama kama kutumia pc
Thanks mkuu nimekuelewa
 
Makamu wa rais nchini Tanzania Samia Suluhu Hassan amezindua mradi wa kuweka huduma ya mtandao wa Wi-Fi katika maeneo ya umma na yale ya burudani mjini Dar es Salaam.

Utekelezaji wa mradi huo wa kampuni ya mawasiliano nchini humo utapanua huduma za mawasiliano ili kuweza kuwafikia watu wengi zaidi na hivyobasi kuimarisha uchumi.

''Tunawapongeza kwa kutekeleza mradi huu na tunatumai upandaji wa miti katika maeneo tofauti mjini ikiwemo maeneo ya burudani, watu wataweza kupata huduma ya mtandao'' ,alisema.

Kwa upande wake Kamishna wa Jimbo la Dar es Salaam Paul Makonda amesema kuwa mradi huo ni mmoja wa awamu tano za juhudi za serikali kuimarisha huduma kadhaa hususan mawasiliano na huduma za mtandao kwa wote.

Utekelezaji wa mradi huo ndio mwanzo wa safari ya kujenga miji na miji mikuu katika kiwango cha 'Smart City' nchini Tanzania.

========

KAMPENI YA MTIWANGU YAJA NA NEEMA HII ILALA
Ikiwa ni Octoba Mosi siku ambayo, imeshuhudiwa maeneo mbalimbali ya Jijini Dar es Salaam na Wilaya zake tano za Temeke, Ilala, Kinondoni, Ubungo na Kigamboni yakitekeleza agizo la Mkuu wa Mkoa huo Paul Makonda katika suala zima la upandaji wa Miti kupitia kampeni yake ya Mtiwangu.
Kampeni hiyo ambayo imezinduliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu, imeambatana na jambo lingine ambalo litawanufaisha wakazi wa Ilala na watanzania kwa ujumla. Akizungumza juu ya suala hilo Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema ameelza kuwa kwa kushirikiana na kampuni ya mtandao wa simu ya TTCL wameweza kuweka ‘Internet’ ya bure kwa wakazi watakao kuwa wanaotembelea maeneo yenye bustani kubwa za mji, jambo litakalo wasaidia kupata taarifa mbalimbali zenye kuelimisha na kuwasiliana kupitia mitandao ya kijamii, ambapo Mkurugenzi wa TTCL Waziri Kindamba ameasema zoezi hilo halitakuwa la kusuasua kwani wamejipanga kufanya mapinduzi ya kimtandao na kuongeza kuwa Tanzania inakuwa nchi ya Tatu Afrika Mashariki kwa kufanya hivyo ikiungana na Kenya, Uganda, huku kwa Afrika ikiwa ya Tano zikiongezeka Nigeria na Afrika Kusini.
DC-MJEMA-MITI-ILALA-13.jpg

Kwa upande wake Makamu wa Rais amepongeza uwepo huo wa ‘Internet’ (WiFi) kwa maeneo yenye bustani ikiwemo NBC, Palm Beach, Mnazi Mmoja na Gymkana ambapo uzinduzi huo ulifanyika, huku akisisitiza suala la kutunza mazingira na upandaji miti liwe endelevu, kwani hali ya hewa ya Dar es Salaam imekuwa ya joto kutokana na athari za Mazingira, hivyo ameziagiza Wizara zinazosimamia Misitu na Mazingira kuzifuatilia bustani zote zilizopandwa miti siku ya leo.
Hayo ni maua sio miti.
 
Back
Top Bottom