Dar kupata huduma ya Internet/Wi-Fi bure

Dodoma itaendelea kuwa Makao makuu ya nchi,Dsm itaendelea kuwa mji mkuu wa vipau mbele vya nchi.
 
hii habari nmeiona BBC sijaona vyombo vya ndani hats vile vya Lumumba vikiripoti .. .. pengine waandishi wa BBC hawakuielewa..
 
Makamu wa rais nchini Tanzania Samia Suluhu Hassan amezindua mradi wa kuweka huduma ya mtandao wa Wi-Fi katika maeneo ya umma na yale ya burudani mjini Dar es Salaam.

Utekelezaji wa mradi huo wa kampuni ya mawasiliano nchini humo utapanua huduma za mawasiliano ili kuweza kuwafikia watu wengi zaidi na hivyobasi kuimarisha uchumi.

''Tunawapongeza kwa kutekeleza mradi huu na tunatumai upandaji wa miti katika maeneo tofauti mjini ikiwemo maeneo ya burudani, watu wataweza kupata huduma ya mtandao'' ,alisema.

Kwa upande wake Kamishna wa Jimbo la Dar es Salaam Paul Makonda amesema kuwa mradi huo ni mmoja wa awamu tano za juhudi za serikali kuimarisha huduma kadhaa hususan mawasiliano na huduma za mtandao kwa wote.

Utekelezaji wa mradi huo ndio mwanzo wa safari ya kujenga miji na miji mikuu katika kiwango cha 'Smart City' nchini Tanzania.

========

KAMPENI YA MTIWANGU YAJA NA NEEMA HII ILALA
Ikiwa ni Octoba Mosi siku ambayo, imeshuhudiwa maeneo mbalimbali ya Jijini Dar es Salaam na Wilaya zake tano za Temeke, Ilala, Kinondoni, Ubungo na Kigamboni yakitekeleza agizo la Mkuu wa Mkoa huo Paul Makonda katika suala zima la upandaji wa Miti kupitia kampeni yake ya Mtiwangu.
Kampeni hiyo ambayo imezinduliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu, imeambatana na jambo lingine ambalo litawanufaisha wakazi wa Ilala na watanzania kwa ujumla. Akizungumza juu ya suala hilo Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema ameelza kuwa kwa kushirikiana na kampuni ya mtandao wa simu ya TTCL wameweza kuweka ‘Internet’ ya bure kwa wakazi watakao kuwa wanaotembelea maeneo yenye bustani kubwa za mji, jambo litakalo wasaidia kupata taarifa mbalimbali zenye kuelimisha na kuwasiliana kupitia mitandao ya kijamii, ambapo Mkurugenzi wa TTCL Waziri Kindamba ameasema zoezi hilo halitakuwa la kusuasua kwani wamejipanga kufanya mapinduzi ya kimtandao na kuongeza kuwa Tanzania inakuwa nchi ya Tatu Afrika Mashariki kwa kufanya hivyo ikiungana na Kenya, Uganda, huku kwa Afrika ikiwa ya Tano zikiongezeka Nigeria na Afrika Kusini.
DC-MJEMA-MITI-ILALA-13.jpg

Kwa upande wake Makamu wa Rais amepongeza uwepo huo wa ‘Internet’ (WiFi) kwa maeneo yenye bustani ikiwemo NBC, Palm Beach, Mnazi Mmoja na Gymkana ambapo uzinduzi huo ulifanyika, huku akisisitiza suala la kutunza mazingira na upandaji miti liwe endelevu, kwani hali ya hewa ya Dar es Salaam imekuwa ya joto kutokana na athari za Mazingira, hivyo ameziagiza Wizara zinazosimamia Misitu na Mazingira kuzifuatilia bustani zote zilizopandwa miti siku ya leo.
At the same time wengine wanawaza malaika washuke ili kuzuia mitandao ya kijamii!
 
Aisee wewe mtoa mada hebu acha kuandika unachofikiria kichwani mwako, toka lini kumetangazwa Dar ni Jimbo na lina kamishina? au ni cheo kingine alichonacho

Ttcl iko hoi halafu inatoa vya bure?

Waweke WiFi sehemu zote muhimu lakini iwe ya kulipia have hata kwa gharama ndogo.
 
Wakiweka wifi mimi namtuma malaika akafunge mitandao yote, wifi watabak kuangalia tu[emoji81][emoji81][emoji81][emoji81]
 
Kweli walionacho wanazidi kuongezewa,yaani hiyo huduma ya free Internet badala wangeweka kwenye maeneo ya watu masikini kama Manzese,Temeke,Buguruni na Mbagala wanaweka kwa wanojiweza huko Posta.
 
Aisee wewe mtoa mada hebu acha kuandika unachofikiria kichwani mwako, toka lini kumetangazwa Dar ni Jimbo na lina kamishina? au ni cheo kingine alichonacho
kamishina wa mkoa......regional commissioner(RC)
 
Hii habari niliiona BBC...Naona mwandishi wa BBC anasema "Jimbo" badala ya "Mkoa"...Anasema "Kamishna" badala ya "Mkuu wa Mkoa" japo kwa kingereza ni "Regional Cammissioner"!!!
Sasa BBC watunze Kiswahili kwa kujua kwetu "Kamishna wa Mkoa" tamuita "Mkuu wa Mkoa"

Huduma itatolewa na TTCL...Wakati mwingine akitaka Wi-Fi kila mahali,mwingine anatamani malaika wenzake ambao siku moja alisema akifanya kazi vizuri ataenda kuwa Rais wa Malaika waje wazime mitandao Tz.
 
Jamani hizi khabary za interner bure maeneo ya wazi ni za kweli au ndi udaku!!
 
Back
Top Bottom