Dar kumenishinda, nataka nihamie Mbeya

Manunu

New Member
May 17, 2021
2
6
Habari zenu wapendwa, mwenzenu maisha ya Dar yamenishinda nataka nihamie mbeya mjini, nipeni ushauri hapo wadau
 
Mkuu hili jiji linataka uwe na kipato cha uhakika kama ni mfanyakazi uwe na mshahara unaoeleweka na kama biashara sio za kuunga unga madhara yake ni kwamba ili kwenda sawa inabidi ukaishi kwenye makazi ya makapuku a.k.a uswazi ambapo mvua zikinyesha dawasco inaamia ndani kwako unakuwa chanzo cha maji, utapata sana shida za usafiri, yaani utakuwa wa kutamani majumba ya watu na kukomaa kwa kukimbia kuvuka barabara ili wenye pesa zao wasikugonge na magari yao.Rudi nyumbani kakomae.
 
Back
Top Bottom